Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 667
- 1,467
Muonekano wa mwezi ukionekana na mashimo katika maeneo yake mbalimbali hata ukiwa huku duniani pia unaweza ukayashuhudia haya mashimo kama siku mwezi ukionekana wote (Full moon) na anga likiwa limetulia.
Mashimo hayo yamesababishwa na asteroidi na vimondo mbalimbali vilivyoweza kuushambulia mwezi wetu na vinavyoendelea kuushambulia mwezi wetu kila siku kila baada ya muda.
kwakuwa mwezi wetu hauna anga hewa (atmosphere) au tuseme kwakuwa mwezi wetu hauna uwezo wa kushika anga hewa kutokana na uwezo mdogo wa kani yake ya uvutano (gravity), ambayo kwa kawaida husaidia kushikilia matabaka mbalimbali kuendelea kubaki katika gimba na kuzunguka gimba lote kwa ujumla.
Sasa kwenye mwezi wetu kitu hicho hakuna kabisa na hupelekea vinasaba vyote vya anga hewa kupotelea angani. Anga hewa hucheza katika nafasi ya ulinzi wa vitu mbalimbali vinavyoweza kushambulia gimba.
Sasa kama gimba litakuwa na wingi wa anga hewa mbalimbali au matabaka ya anga hewa mazito basi ndipo ulinzi wa gimba unavyokuwa mkubwa kwakuwa vitu vyote huunguzwa na wakati mwengine husambaratishwa kabisa katika kipindi cha kuingia kwenye magimba yenye matabaka ya anga hewa mazito.
Kama mwezi wetu ungelikuwa unauwezo.wa kushika matabaka ya anga hewa mazito na mengi basi kusingekuwa na mashambulizi mengi ya vimondo na mawe makubwa ya astreroid.
Moudyswema Tanzaniascienceyetu AstronomyKiswahili