Chombo kikipita katika matabaka ya anga hewa za dunia

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Chombo cha Orion kikioneka kikikatiza katika matabaka mbalimbali ya dunia yetu wakati wa kurudi duniani kutokea katika safari za anga za mbali.

Chombo hupitia katika hali ngumu sana ya joto kali linalopeleka kuwa moto mzito sana na kumbuka kadri chombo kinaporudi kutokea safari za mbali basi ndipo hatari ya chombo inavyokuwa kubwa sana kwasababu kadri unavyotoka mbali ndipo hutumia muda mrefu sana katika kupita kwenye matabaka mazito haya ya hewa na ndipo joto linavyokuwa kubwa sana na kupelekea moto mzito.

Kikawaida kwa watu wanaotoka katika kituo cha anga za mbali hutumia kiasi cha dakika 4 kuweza kumaliza kupita katika hali hii mbaya mpaka kufika chini duniani.

Gamba gumu linahitajika ili kuweza kukabiliana na hali kubwa ya joto kali sana kumbuka material yanayotengeneza gama hili gumu huwa ni material ya carbon ambayo ni magumu sana kuruhusu joto kupita.

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu

AstronomyKiswahili

FB_IMG_1675150804181.jpg
 
Back
Top Bottom