Munisi na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Munisi na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chiefthinker, May 11, 2011.

 1. c

  chiefthinker Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  [FONT=Arial, Arial Black]
  Sijuti kugombea kiti cha urais Tanzania, Bali namshukuru Mungu kuniwezesha kufanya hivyo. Mungu ni HAKI tupu na ndani yake hakuna hata chembe ya udhalimu. Hatuwezi kudai kumcha Mungu huku tukiunga mkono udhalimu wa CCM. Wanaoiunga mkono CCM dhalimu, watuambie wanamwabudu nani kama siyo shetani baba wa udhalimu wote. Tusidanganyane. Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu na ukose kuyaona MAOVU ya CCM. Watumishi wa shetani ndio wanaoyafurahia maovu kwani, yanatimiza lengo la shetani la kuchinja, kuharibu, na kuua. Tunaipinga CCM Tanzania sawa na tunavyompinga shetani duniani kote. Dunia ni mali ya Mungu, na Tanzania ni sehemu ya dunia. Hatuwezi kumpinga shetani duniani huku tukimruhusu aweke kambi Tanzania, akitumia Chama Cha Majambazi CCM. Haiwezekani, Tumekataa, Hatutakubali, na hatutaki.

  Ni agizo la Mungu kwamba wale wanaomtumikia, Wayahubiri maneno yake kwa walimwengu wote. Kila atakaeyaamini maneno ya Mungu, Sifa ya kwanza ni kuyakataa maovu yote. Atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuwasaidia, Kuwatetea, na kuwakomboa wanadamu wanaonyanyaswa chini ya utawala dhalimu wa CCM. Akifanya hivyo, anatimiza agizo la Mungu. Akifanya kinyume na hayo, Atakuwa hajatimiza wajibu wake kama mtumishi wa Mungu.

  Watumishi wa Mungu ni wale wanaomwamini Mungu. Haijalishi wanatoka dini gani, hata kama ni dini za kienyeji, Ilimradi wanamwamini Mungu, Basi wamehitimu kuitwa watumishi wa Mungu. Hatuwezi kuwahukumu watu kutokana na tofauti za kidini, Badala yake tunawahukumu kutokana na matendo yao. Wakitenda mema ambayo asili yake ni Mungu, Tutawaita watumishi wa Mungu. Hata kama dini zao ni za kiasili. Huwezi kuwaita vinginevyo. Ni watumishi wa Mungu. Wakitenda maovu ambayo asili yake ni Shetani, Tutawaita waabudu Shetani hata kama dini yao inatoka Marekani. Katika hilo watumishi wa Mungu ni dhahiri. Yaani wale wanaochukia maovu na kuyakemea, hata kama maovu hayo ameyafanya Mkapa na serikali yake inayowaua wale wanaosema kwamba CCM imezeeka, Iliharibu Tanzania, hawaitaki. Kuna kosa gani kusema hivyo wakati ni ukweli usiopingika?

  Wakati umefika kwa watumishi wa Mungu kuwakomboa watu wa Mungu. Wameteseka vya kutosha. CCM imewaibia, na hata wengine imewaibia uhai wao. Mungu anasema "IMETOSHA. LAZIMA WATANZANIA WAKOMBOLEWE KUTOKA MAKUCHA YA CCM." Kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Mungu siyo sawa na mwanadamu. Akisema saa imefika Watanzania wakombolewe ANAMAANISHA NA ITAKUWA HIVYO. Nilianza kuyasema haya mwaka 2000, wengine wanauliza mbona ni muda mrefu na hakuna dalili za njia ya kuwakomboa watanzania? Mungu hatawaliwi na muda. Muda wote ni wake. Kifupi ni kwamba Mungu hachelewi wala hawahi. Hufanya vitu kivyake ili abaki Mungu nasi tubaki wanadamu. Mwaka elfu mbili nilisema ole wao wanaosimama kuyazuia mapenzi ya Mungu Tanzania. Mkapa alisema yeye ni mbabe na akashupaza shingo. Leo hii anatembelea magongo akielekea kaburini. Haijalishi watatumia pesa ngapi kujaribu kumtibu, Lakini lazima mapenzi ya Mungu yatendeke ili iwe funzo kwa wengine wasijaribu kushindana na Mungu. CCM mwisho wake umefika. Mungu anajua atatumia njia gani kuzima kiburi cha CCM. Kazi yangu ni kuwatayarisha watanzania wawe tayari kuyaona makuu ya Mungu Tanzania. Baada ya kila kitu kutendeka na CCM iwe ni historia, Watanzania tutayainua macho yetu juu na kumtukuza Mungu aliyetenda maajabu machoni petu. Kuna wengi hawataishi kuyaona hayo.

  Sera za Mungu ni "ANZENI NA MIUJIZA ITAWAFUATA." Ni vigumu watu kuifuata miujiza ya Mungu, Lakini ni rahisi watu walioamua kufuatwa na miujiza ya Mungu. Kwanza wanaihitaji kuliko wale ambao hawajaamua. Tangu tulipoamua kuipinga CCM na sera zake mbovu, Mungu ametenda miujiza mingi. Mkubwa kuliko yote ni ule wa kumwangusha mbabe wa CCM DIKTETA Nyerere pamoja na Nduli Benjamin Mkapa ambae atafuatia karibuni.

  Kwa sasa CCM ni sawa na nyoka aliyekwisha pondwa kichwa na kilichobaki ni kutikisika kwa mkia. Suala kama la kuibadili katiba ili iniruhusu kugombea bila chama cha kisiasa, siyo tatizo kubwa kama linavyoonekana. Wengine wanaliona hilo kama bahari kubwa mbele yetu.

  Yangu ni kuwaambia kwamba waamini tu na watauona muujiza wa Bwana. Kama wana wa Izraeli walivyopita katikati ya bahari ya Shamu kama nchi kavu, Ndivyo Watanzania tutakavyolivuka tatizo la
  [/FONT]
   
 2. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Huyu munisi si ndo yule alikuwaga mwizi akaokoka??
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Koukoka ndio kuvua gamba. Duh lakini huyu bwana mkali kweli. Tuiombee Nchi yetu Tanganyika:A S cry:
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ghriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ni FAUSTINE MUNISHI na si munisi(kama sijakosea)...aliimba MALEBO.....YESU NI MAMBO YOTE....n.k
   
 6. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuwekeeni ule wimbo wake 'CCM IMEZEEKA'
   
 7. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni heri yule aliyetenda dhambi na kutubu kuliko yule ajuae kuwa anatenda dhambi na bado anaendelea kutenda dhambi
   
 8. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Munisi ni shetani tu katika rangi nyingine. Kama yeye ameokoka kwa niji yeye amhukumu mwenzie wakati biblia takatifu inakataza? Anasema Mkapa anatembelea magongo kwa hiyo hata wamtibu vipi atakufa! Sasa mimi nimuulize Munisi kwani yeye ameambiwa ataishi milele? Asiyekufa ni yeye tu Mwenyezi Mungu aliyehai, munisi kumbuka uliumbwa kwa udongo na utarudi kwa udongo. Jambazi mstaafu huyo Hana aibu
   
 9. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli etieee! Jambazi! Mwivi wa kuku kuganga njaa yake anaitwa jambazi mkubwa! Mwivi wa milioni 150 kwa siku anaitwa nani ndugu?
   
 10. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  Anaitwa gamba, na anaombwa kuondoka kwenye chama pindi akijisikia. Hii ndiyo nchi yenye domokrasia
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tusiwe wajinga wa kumhukumu mtu aliyekiri makosa yake na kutubu! Hawa mafisadi tulionao sasahivi hatuwezi kuwalinganisha na Munisi kwasababu hawakubali ni mafisadi na wala hawataki kutubu. Wanawatuma nyie kwa malipo ya kuganga njaa kuwasafisha! Ndio maana hatuwezi kuwasamehe. Pole ndungu yangu maana na wewe umeingizwa kwenye mkumbo na hutasamehewa! Vitabu vitakatifu vinasema, TUBUNI nanyi mtasamehewa!
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Kama yy alitubu awape na wengine muda wa kutubu kuliko kuwaombea kifo. WTF!
   
Loading...