kanyela mumo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,034
- 2,119
Nimepaki gari mtaa mmoja kuna duka, nikashuka kwenda kununua maji ya chupa.
Nimerudi vizuri mpaka kwenye Gari, nikaweka gia ya kurudi nyuma. Aisee nimemburuza mtoto mdogo wa kiume, nikajua nimeua.
Nikainama kwenye sterling, nikamuomba Mungu wangu kwa dhati na unyenyekevu. Wakati huo vijana zaidi ya ishirini wamezunguka Gari pamoja na wazazi wa yule mtoto.
Mungu mkubwa mtoto katoka mzima na bahati nzuri kuna watu wazima waliona lile tukio hivyo wakathibitisha mimi sijafanya makosa, ila mtoto na wazazi wake ndio wenye makosa. Wakazidi kusema wazazi wa sasa hivi hawako makini na watoto kabisa.
Nikawachua mtoto na wazazi wake mpaka Polisi, kisha hospital bahati mbaya walikuwa hawana bima hivyo elfu arobaini zimenitoka.
Namshukuru Mungu kwa sababu sasa hivi hata kuchinja kuku siwezi sembuse kumtoa uhai mtoto.
Ndugu zangu yatupasa tuwe makini uswahili na magari yetu haya mkopo.