Mungu uko wapi: Mabomu ya nini-Tulipokukosea TUSAMEHE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu uko wapi: Mabomu ya nini-Tulipokukosea TUSAMEHE

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by We can, Nov 2, 2010.

 1. W

  We can JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mungu wetu;

  Ulitupatia Tanzania na watu wake (nikiwemo mimi, na wengine), mbona sasa unaruhusu watu wako wapigwe mabomu kisa wamechagua UPINZANI? Je, wapinzani si wa Tanzania? Je, hakuna sehemu mume na mke wana vyama tofauti? baba na babu vyama tofauti? Shangazi na mjomba vyama tofauti? Islaam na Ukristu vyama tofauti? Wahindi na wajaruo vyama tofauti?

  Kwani polisi hawana ndugu zao wapinzani? Kwani JWTZ hawana ndg zao CCM na CHADEMA? Mungu, uko wapi uzuie mabomu kwa watu wako maskini? Tazama, waliambiwa, mkichagua upinzani mtaleta vita, kumbe ndo hii vita? Sikuwahi kuijua? Nilichokuwa nadhani ni kuwa wapinzani wakishinda tu wanaanza kutupiga mabomu, ndiyo maana siku zote nilisita kuwachagua; maskini kumbe ndo wanaoonewa! Maskini Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, SHUKA SASA uzuie mabomu haya. Hata kama tumekutenda dhambi, tunaomba utusamehe.

  Kuna watu wanatulazimisha tuamini kuwa sisi wa Tanzania ni wadini. Nilianza kuamni hivyo; kumbe ni ujinga wangu. Nilianza kumchukia jirani yangu bure; mbona ndo kawa wa kwanza kuja kuniangalia jana hospitalini nilipopigwa mabomu nikidhaniwa nimeandamana! Shuka Mwenyezi Mungu uzuie mabomu na umweke RAIS mwenye uchungu na Taifa hili...Amina.
   
 2. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hata ukombozi wa Israel ulikuwa kwa njia ya vita. Hata ukombozi wa miji mitakatifu katika Uislamu ulipatikana kwa njia ya vita. Unalijua hilo?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Yana mwisho haya...2015 is just around ze corner!
   
 4. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Paka Jimmy do not jump to the future!!! Talk about what can you do today. What we do now will determine our future. If nothing is done today the future will be just like today because the cause of events was not diverted.
   
 5. m

  mbombongafu Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sure omulangi
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  AMeni
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ZEKARIA 10 : 2 - 5
  Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo;
  nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda za kama kondoo,
  wateswa kwa sababu hapana mchungaji.+ 3 Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji,
  nami nitawaadhibu mbuzi waume, kwa maana Bwana wa majeshi, ameliangalia kundi lake, yaani,
  nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake vitani.+ 4 Kwake yeye litatoka jiwe lile
  pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye utatoka
  kila mtawala mmoja.+ 5 Nao watakuwa kama mshujaa, wakanyagao adui katika matope ya
  njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.+
   
Loading...