Mungu tunusuru na balaa hili maana hatujui hatima yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu tunusuru na balaa hili maana hatujui hatima yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Jan 17, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mungu tunusuru na maisha haya,maana hali ni gnumu hatujui nini hatima yetu.Kila kukicha heri ya jana,maisha yetu yamegubikwa na kila aina ya shida.Nchi yetu imejaliwa ardhi nzuri yenye rutuba nzuri tena iliyosheheni madini mbalimbali lakini hatujui nani ameturoga,na kama kuna mkono wa mtu basi ni nusura yako tu ndo itakayo tunusuru.Maisha yetu yaliyokosa dira na mwelekeo hatujui siku mmoja ya kesho tutaimudu vipi!Misingi imara iliyosimikwa na waasisi wa taifa hili imepotea,kila mtu anachukua chake mapema.Wenye meno wanatafuna mpaka imekuwa israfu ndo maana tunaomba nusura toka kwako.

  Ni kawaida kwa taasisi za kidini kurudisha maadili kwa jamii iliyopotea lakini kinyume chake taasisi hizi zimegubikwa na kashfa nzito tena zenye kupoteza nguvu ya vijana ambayo hapo awali tulikuwa tunajivunia kuwa vijana ni taifa la kesho.Kitendo cha viongozi wakuu wa dini kuhusishwa na kashfa ya biashara ya madawa ya kulevya ni mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii husika.Haiwezekani hata siku mmoja sheikh/kasisi akawa kinara wa maovu jamii hiyo ikabaki salama,ndo maana tunaomba nusura kwa Jala Jalali.Uongozi siku zote huanzia ndani ya majumba yetu,ikitokea nyumba kuw na migogoro ya mara kwa mara juwa kuwa muundo wa familia katika nyumba hiyo una mapungufu makubwa.Chama tawala kina mgogogro mkubwa wa kimadaraka,tunategemea nini zaidi ya kuwa na serikali legelege.Alama ya jembe kama nembo ndani ya bendera mbona imepoteza maudhui kutokana na dhana iliyokusudiwa.Leo hiii ukiwa ndani ya CCM ukahoji uadilifu wa viongozi wa chama lazima kutatoka kauli nzito kuwa umetumwa nani,wamesahau kuwa katiba inasema kiongozi akubali kukosoa na kukosolewa.leo hii ukikosoa unaonekaana msaliti ndani ya chama.

  WANANCHI
  Wananchi wa nchi hii wamesahau wajibu wao na haki zao za msingi,wamepoteza uzalendo uliozalishwa ndani ya mioyo yao na waasisi wa taifa hili.Zamani kabla ya kuharibika kwa taifa hili linalojivunia amani bandia,watu walikuwa wazalendo wa kweli.Hata nyimbo tulizoimba mashuleni zilihamasisha uzalendo miongoni mwetu,Tuliimba tunaipenda sana Tanzania kwa moyo wetu wote leo hii upendo huu tulioamini kuufia upo wapi?Vijana wamepoteza imani na taifa lao,tena hatari iliyoje kumsikia kijana akisema ni bora angezaliwa mbwa Amerika kuliko binadamu nchini mwake.Nini kilichotupata mpaka uzalendo unapotea miongoni mwetu.Zamani ukimkuta mtu anaharibu miundo mbinu kama madaraja ulikuwa unahoji,ikibidi kumfikisha mhalifu huyo kwenye chombo cha dola,lakini leo hii ukimuona unauliza vipi dili hilo unapeleka wapi ili naye ajumuike kuharibu ili kujitafutia mkate wa siku,hii ni hatari kubwa.Tatizo lingine linalo wakumba vijana ambayo athari yake ni kubwa katika kuleta maendeleo ya taifa hili ni kitendo cha kukubali kuuza haki yake ya kuishi kwa ujira mdogo.Kitendo cha kuuza kitambulisho chake cha kupigia kura ni kitendo cha kidhalimu,ni ukosefu wa uzalendo ndani ya taifa hili.Nchi imeingia kwenye biashara ya kuuza haki za wapiga kura bila hata kumuogopa Mungu.Mwenyezi hakujalia utaratibu wa kuchaguana kwa kununua haki za wapiga kura,hili ni janga la kitaifa linalohitaji nusura toka kwa Allah.

  WAKULIMA
  Wakulima wa taifa hili ambalo limepoteza dira na mwelekeo nao wamepoteza matumaini.Hakuna njia mbadala ya kuweza kujikwamua na jembe hili la kupinda mgongo ukitegemea mavuno bora.Hakuna kiongozi mwenye dhamira ya kweli juu ya asasi hii ya kiraia iliyojiajiri kwa wingi.Asasi hii imesahaulika lakini watu wana implement ideas zao kuhusiana na asasi hii kwa kujinufaisha na posho za vikao bila kupata suluhisho kwa mkulima huyu anayeinama toka jua linachomoza mpaka jua linazama!Kila siku utasikia kauli mbiu mpya toka ndani ya vinywa vyao laikini kauli mbiu zisizo na tija wala mashiko,utasikia kilimo kwanza oh mara mapinduzi ya kiljani, mbona hatuoni impact za hizo slogan zao.Ni kama miaka miwili iliyopita dunia ilikubwa na mtikisiko wa uchumi,kutokana na mtikisiko huu wa uchumi, maneno mengi yalisemwa ikiwa ni pamoja na kuwa Tanzania imejidhatiti katika kukabiliana na hali hiyo,tukajua serikali yetu imedhamiri kumkomboa mkulima huyu,lakini kinyume chake serikali ikaamua kuwasaidia wafanya biashara wakubwa katika sekta hii ya kilimo kwa kuwafidishia hasara waliyoipata kwa kushindwa kuuza mazao yao huku ikimwacha mkulima akitaabika na hali ngumu ya kiuchumi ndani ya familia yake kutokana na kukosa wa kuwatetea.Sipendi kuamini alama ya jembe imewalisha mazishi ya mkulima japokuwa hali ndivyo ilivyo.Ikiwa mkulima anakopwa na halipwi pesa yake kwa kuuza mazao yake kidogo aliyoyapata kwa gharama kubwa na kupoteza muda wake mwingi,tena bado anapangiwa hata sehemu ya kuuza wakati wengine wanafidishiwa hasara,nani ambaye atayemtetea mkulima huyo kama si nusura ya Mungu tu inahitajika katika kumkomboa.Wakishavuna, wanapangiwa na bei bila kujali wamepata hasara au faida tena mbaya zaidi vikao vina kaa kwa kulipana posho za vikao kutokana na kodi ya mvuja jasho huyo.Mungu inusuru sana tu nchi yetu.

  BIASHARA
  Serikali ilitamka hakuna soko la ajira katika sekta za serikali,ajira zilizoko ni kujiajiri,lakini je serikali inazisaidiaje asasi hizi kama si kuzikandamiza?Rais alipotamka mabilioni ya JK kila mmoja aliamini sasa serikali imeamua kuwaona walalahoi hawa,matokeo yake uliza kama kuna mlalahoi aliyewahi kuyaona mabilioni haya,ndo maana sema serikali inawakandamiza walalahoi hawa ambao ndo wengi.Biashara zenyewe ni mashaka matupu,kodi nyingi zimerundikwa katika vijibiashara hivi kama una guest na bar utasikia mara hotel levy,oh kodi ya mapato ya serikali,mara leseni ya biashara watakuja na watu wa zima moto nao wana ada zao kwaajili ya majanga ya moto,tena viwango vimepangwa kisheria kutokana na sheria iliyotungwa na wawakilishi wetu sheria inayoitwa fire and rescue force act number 14 of 2007 made under section 32(g).Hivi kweli watabaki salama,bado serikali ya mtaa inakusanya kodi ya kuzoa uchafu,huyu mlalahoi atabaki salama katika kuendesha maisha yake ya kila siku?Tunasubiri itakuja na sheria nyingine ya police force act nayo itahitaji malipo japokuwa yapo lakini hayajapasishwa kisheria.Nasema yapo,kutokana na polisi akikukamata umechelewa kufunga biashara akikupeleka kituo cha polisi huwezi toka bure.Hivi ni Taifa gani tunalojenga kwa vizazi vijavyo?

  SERIKALI
  Mungu uliye juu serikalii yetu inahitaji nusura tena nusura kubwa,kwani inapotupeleka uvumilivu maji yamefika shingoni.Serikali ya watu huendeshwa kwa matakwa ya watu wake,ndo maana utasikia serikali ni watu.Huwezi kuwa na serikali kama huna watu.Shetani mwenyewe ana serikali yake kwa vile ana mashetani wenzake anaowaongoza.Serikali imesahau watu wake,inawaburuza,imeweka pamba masikioni haina mwenyewe.Serikali imekuwa pango la wananyang'anyi.Pango la wanyang'anyi kwa kushindwa kuwafikisha mbele ya sheria waliosababisha nchi kuingia gizani na kusababisha mifumuko ya bei kila kukicha.Serikali inayogopana kila mmoja ana muogopa mwenzake kwa kuwa tu anajua madhambi ya mwenziwe.Serikali inayowafumbia macho mawaziri wake kwa kushindwa kuwajibika katika sehemu zao za kazi.Rais utadhani yupo likizo,migogoro kila sekta.Serikali isyothamini haki za wataalamu wake kama madaktari,Serikali isiyoheshimu taaluma za watalaamu wake ni serikali ya ajabua sana iliyowahi kutokea katika karne hii.Sipendi kuamini kama wananchi wamerogwa kiasi cha wananchi kushindwa kutambua hawana serkali.Nusura tu ya Allah ndo suluhisho la utambuzi huu,migogoro iliyopo inalenga nani atayesimama mwaka 2015 katika mchuano wa urais,shughuli za maendeleo zimesimama anayeathirika ni mwananchi wa kipato cha chini,gharama za maisha zimepanda wakati mishahara haikidhi mahitaji ya lazima.Wafanyakazi wakitaka kugoma wanatishiwa na kiongozi wa nchi tunakwenda wapi.Serikali iliyofungua milango kwa wakoloni kuingia ndani ya nchi yetu kwa jina jipya la wawekezaji na kupora kila kilicho haki yetu na kuondoka wakituachia mashimo.Serikali inashindwa kusimamia wakoloni hawa kuweza kutoa zile social facilities katika maeneo waliyokwenda kuyanyonya.Ni hatari sana tena kubwa kwa viongozi kutoka na kauli za kuwakumbatia wageni kwa kauli oh wawekezaji wote si kwamba ni wabaya wakati wananchi wetu wanapiga risasi za moto.Hatari iliyoje ikiwa hata serikali nayo imepoteza uzalendo kwa wananchi wake.Wanyarwanda waimbaji walipata ajali maeneo ya mkoa wa Shinyanga,lakini kwa uzalendo wa serikali ya Rwanda kwa watu wake helikopta ya serikali ilituwa pale tinde na kuwachukua raia wake,kwanini sisi hatuigi kwa wenzetu?Ndo maana na support sana kauli alizozitoa Ehud Barak kuwa Tanzania is irrelevant.

  Najua sana kuna watu watasema huu ni uchochezi,ila kwa wale wenye kuona mbali watagundua ni sauti iliyo nyikani inahitaji nusura ya Mwenyezi Mungu azidishe imani na uvumilivu mioyoni mwetu,kwani mtu akiwa na njaa hukosa nidhamu,Watanzania uvumilivu na nidhamu imeanza kupotea miongoni mwetu.Kamwe hatuwezi kuwa bulldozer la kuwasafishia njia walafi wa madaraka kwa kura zetu kutibia ilihali nchi inazidi kupoteza dira na mwelekeo wake.

  BUNGE
  Mwisho na malizia kwa kusema bunge likiwa legelege husababisha kusimamiwa na serikali,bunge limeshindwa kuisimamia serikali matokeo yake serikali inafanya inavyotaka.Wanao umia ni wananchi.Labda tuwakumbushe kuwa ipo siku tutaamu kusimama kidete na kuingia mjengo tuwafungie ndani mtueleze ni kazi gani tuliyowatuma na nini mnachofanya.Hatari iliyoje leo hii mbunge anasimama kuitetea serikali kuendelea kuwakandamiza wananchi,hiyo ndo kazi tuliyomtuma,Ipo siku isiyo na jina.South Africa waliamua kumng'oa mkoloni kaburu kwa vile walitia nia,na sisi tunasema ipo siku Tahriri itaanzia Dodoma mwisho wake hatujui utakuwa wapi.Tunaomba Mungu uwatoe fikra mgando, wafanye kazi kama walivyokula viapo vyao.Kama wameshindwa bunge zima lijiudhuru tena tunategemea wabunge wazalendo wa kweli wapeleke hoja binafsi ya kujiuzulu kwa bunge zima kwa kushidwa kuisimamia serikali na kuchukua posho zisizostahili kwani hawafanyi kazi tuliyo watuma.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ameen....
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Haleluyaaaaa!
   
Loading...