illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Mitandao imetuharibu sana watu wanatukana, wana andika maneno ya uchochezi bila kuelewa athari zake Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo hazina travel advisory nimefanikiwa kutembea nchi kadhaa kukuta maiti nje ya nyumba ni sehemu ya maisha nashangaa kuna mtu anadiriki kusema eti tumechoka amani ya kise...... nakumbuka wakati mabomu ya mbagala na gongo la mboto yalilipuka tena kwa bahati mbaya ilitokea taharuki watu walivurugana jiji zima watu walikimbia kwa miguu wakielekea muelekeo wa morogoro bila kujua wanaenda wapi nashangaa hii mitandao mtu anadiriki kuandika post yenye uchochezi sababu tu ya kulipwa au ushabiki naomba uangalie video hapo chini ni nchi jirani tu ya Kenya Mungu hakupi kila kitu tuna mapungufu yetu lakini amani yetu tuililie mpaka mwisho