Mungu, Siasa na Maisha

hipocampus

Member
Sep 14, 2020
89
104
Mwenye enzi MUNGU(The omnipotence,the omnipresence,the omniscience )atusamehe sana.

NITANGULIZE salamu zangu za dhati kwa wakuu wangu wote ndan na nje ya nchi hata kwa wale ambawo hatuonani kwa mboni zetu za Macho, ila n kweli uso shaka huwa napata faraja sana nikitazama juu ya mbingu natambua kuwa bado tunatumia mbingu moja kwa matumizi mbalimbali kama vile mvua ,jua ,mvuke nk.

Nimejitahidi kugusa nyanja nyingi ikwemo jamii ,uchumi ,siasa na michezo_Ombi langu kwa wadau ambao hawapendezwi na maandiko marefu nao wajitahidi kufuatilia naimani wataokote "LULU" kwa kuwa WANA "CEREBRUM NA HIPPOCAMPUS" nzuri naimani hawatoasi tutakuwa pamoja wote

ili tuelewane kwa atakayebahatika kuyasoma hayo maandiko hadi mwisho nahitaji kutoka kwako ni
UTULIVU,UTULIVU,UTULIVU ili tuingie wote kwenye ile Behewa ya kutafakari kwa kina tena tukiwa salama wa salmin .

Nimeona mengi na kusikia mengi na vile vile sijaona mengi na kusikia mengi pia ,ruksa kunifunza kwani inasemwa ishi duniani ukiwa mwanafunz wa kudumu utayapata mengi sana ..rejea kitabu cha "THE MONKEY WHO SOLD HIS FERRARI" kilichoandikwa na mtunzi ROBIN SHARMA

Tafadhali tafakari yafuatayo,

Tunaishi katika Dunia ambayo watu wengi wanamtaja MUNGU kila muda lakini hawamuofii hata kidogo! Vibweka tupu !, uchawi madhabauni! ,uchawi kibla!..kuna muda unaweza sema baadhi ya hawa watu wamesomea hizo dini ukristo,Uislamu,bohora,baniani ,Budhism na dini nyinginezo ili kuwavuruga watu tu tuwe makini tuombe msamaha.

Hakuna jambo zuri Duniani kama kujua kusudi lako la kuishi na ukaliishi Hilo kusudi utajuaje? .Tafadhali isikilize sauti yako ya ndani(inner voice) kisha uifuate lazma utakuwa bora tu kwa sababu hio n sauti ya MUNGU .Watazame kina Leonard da Vinci,Rockfeller ,albert einstein,Mwalimu Nyerere,Martin luther, Ronaldinho Gaucho, Jeff bezos ,Warren buffet

Asilimia 9% ya maisha n namna ulivyoyatengeneza na asilimia 91% ya maisha n namna ambavyo unavyoyachukulia na hapo ndio twapata tofauti mfano ;

kuna mwengine Utajiri kwake ni PESA ,kuna mwengne Utajiri kwake n Maarifa, Mwingne Utajiri kwake N furaha ,Mwengine utajiri kwake N haki,Kuna mwngne utajiri kwake n Amani ,Mwengne utajiri kwake n Afya,Mwengine utajiri kwake Busara ,Mwingne Utajiri kwake N Fitna ,Mwngne utajiri kwake n uovu n.k kimsingi kama hupati jawabu vile tafadhali fanya marejeo kwa zile asilimia utazidi kuelewa nasema nini.

Dunia ya sasa aihitaji ufanye kazi kwa bidii tu ili upate utajiri bali inataka zaidi matumizi makubwa ya akili ili Upate utajiri ..rejea kitabu cha "THINK AND GROW RICH" kilichoandikwa na Napoleon hills

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia "usiangalie utajiri wa mtu bali angalia alipoanzia..,kuna wengne kwao walikuta uchumi imara wakauendeleza,kuna wengne walianza moja ,Wengne utajir wao walidhulumu wengne ,Wengne utajiri wao wa masharti eti hawaruhusiwi kuvaa viatu watembee peku mwiba ukimchoma na utajir unaongezeka ,mtu Ana donda kubwa mwilini kwamba Donda likitoa usaha basi mali inaongezeka,Wengne wamefuga mazezeta likitema udenda na mali inaongezeka"

Pamoja na mengineo uwepo wetu dunian tupo kwa kutegemeana sana Biology inatuambia kuhusu (Ecosystem).. wengi wanasema tajiri anamtegemea maskini na maskin anamtegemea tajiri,Mwenye Elimu anamtegemea Asiye na elimu na Asiye na Elimu anamtegemea mwenye Elimu .Pengine Dua la huyo unayemuona hana maana ndio mafanikio yako. TUSIBEZANE !

Swali fikirishi ,Hivi ulishawahi kujiuliza n Nani atafuta hizo picha zako ziso "staha na soni" katika mitandao yetu ya kijamii siku ambayo roho zetu zimeacha mwili ? Nafahamu mwili tu ndo unakufa ILA roho inabaki maandiko ya baadhi ya imani yanasema huko makaburini Maisha yanaendelea kama kawaida watu wanakula ,wanakunywa n.k

Mwana wa Adamu ! Enda tezi na Omo ila tambua kuwa kuna mstari mwembamba sana Kati ya hvi vifuatavyo , Uzima na kifo ,Afya na Magonjwa hivyo hatuna budi kujiandaa kwa lolote wakati wowote

Kwa hakika Moyo wa mtu n Msitu wenye Giza nene sana kuna muda mtu anaweza kupa tabasamu la kirafiki kumbe huko moyoni kwake anakuchukia na kukunenea mabaya mda mwngne hapendi hata kivuli chako.

Kuna muda watu wako wa karibu tu mfano rafiki ,ndugu,Wazazi, wake kwa waume ambawo tumetoka nao mbali tu tena katika ile kamba ya umoja wanakugeuka wanakuwa NYOKA tena zaidi ya yule wa Nabii MUSA kupitia ile fimbo yake.

Tayari kwa kukugonga muda wowote bila kujali madhara yake .. utamjuaje huyo mtu ..kimebaki "kitendawili" lakn Sio kile alichokiimba Mtunzi JUSTINE KALIKAWE wa kule kagera "ile kitendawiliiiii tegaa ,kitendawiliiii tegaaa oyaayaaa"" itafute nyimbo hio mwalimu kitaaluma huwa anatoa 25% ya somo zima na 75% mwanafunz awajibike kutafuta maarifa .

Usimlaumu MUNGU kwa kumuumba Chui fikiria kama angemuumba na mabawa je ingekuwaje?,ukitafakari unaona kuna haja ya kushukuru sana! hiv unajua hio barabara unayopita kila siku kuna mwenzako kashawahi pata ajali,hio hospital unayoipita katka matembezi yako kuna mwenzako kalazwa humo ndani mwezi wa 8 huu .

Neno THINK & THANKS yote originate in Latin rejea kitabu cha "Impossible to possible"kilichoandikwa na JOHN MASON

Kwamwe Mzazi hawezi kumlaani mtoto wake wa damu au asiye wa damu haiwezekani .Ni kama JUA ,eti lizame Kusini kisha lichomoze KASKAZINI .Bali matendo ovu atendayo mtoto juu ya mzazi ndio kinasababisha mtoto apate Laana umenipata!.

Kinachokutukana wewe sio lile tusi ulilotukanwa bali n Tafsiri yako katika lile tusi ..ukipuuzia halitokuumiza na ndipo busara inakuanza.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika(world clock population) vinasema Watu ambao tupo hai mpk sasa n takribani bilions 7,820,173,665

Miezi kadhaa iliyopita shirika la afya la Dunia , W. H.O (WORLD HEALTH ORGANIZATION )Lilitangaza kuwa tumetembelewa na ugonjwa wa CORONA (covid 19) au kitaalamu (Saris Cov-19) kirefu chake ni (Severe Acute Respiratory infection sydrome ,Corona virus 2019)..

ilifika mahali
Katibu mkuu wa umoja wa kimataifa (UNITED NATIONS) Bwana Antonio Guterres akatangaza kuwa hilo no janga la kimataifa n kweli limetikisa ,limeua(R.i.p) na mpk sasa bado linasumbua kwa nchi nyngi tu ila hofu yake imekuwa tofauti na awali
Mpaka kufikia sasa takwimu za CovId19 zipo kama ifuatavyo

Waathirika Dunia nzima n milioni 41,487,185

Waliopona ni milioni 30,914,158

VIFO VIKIWA N milion 1,136,341

Tarehe 16 Oct kila mwaka huwa ni maadhimisho ya SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Hili inawekewa mkazo na mikakati hii miwili mfano;

1)Shirika la chakula na kilimo Dunia kwa kimombo ni Food and Agriculture organization of the United nations (F.A.O)

2)Programes ya Chakula Dunian kwa kimombo n World food programmes (W.F.P)

Hivi karibun katika takwimu zao walikuja na haya yafuatayo,

1) Takribani chakula chote kinachozalishwa Duniani kina uwezo wa kulisha zaidi ya watu wote hai katika hii Dunia

2) Takribani watu milion 690,000,000 Dunia nzma wanalala na njaa kila siku.

3)Takribani chakula cha kulisha watu hai bilioni 2 Duniani huaribiwa yan hutupwa

4)DUNIANI Watoto millions 14 chini ya miaka mitano wanasumbuliwa na hali mbaya sana ya njaa(malnutrition)na idadi inakadiriwa kuongezeka kwa 20% kufikia 2050 .

5)Takribani Kila BAADA YA DAKIKA 5 Dunia nzima MTOTO mmoja hufariki kwa upungufu wa CHAKULA(NJAA)

Lakini pamoja na yote hayo ILA mtandaoni utaisikia COVID19 .lakini Hayo madhara ya ukosefu wa chakula tena ndo yanaua sana Hayazungumzi sana..UNAJUA KWA NIN ? Pengne N kwa sababu hayawagusi Wenye Uwezo !

Pongezi sana MARCUS RASHFORD(Man united)Kwa kuliona Hili kupitia ile programe ya chakula na fareshare hapo milestone UK.

Hivyo Hashim rungwe anavosema Ubwabwa na njaa hataniii yupo serious!

Poleni sana ndugu zetu wa huko Qatar taarifa zenu za kunyanywaswa kijinsia,kingono,kuteswa taarifa zenu tumezisikia Kupitia shirika la kutetea haki za kibinadamu la AMNESTY INTERNATIONAL ORGANIZATION.Nafahamu hamkujua ama kweli kesho kimebaki kitendawili kwa kila Mja.

Poleni sana Wana wa nchi wa Beni kule Congo munayofanyiwa Dunia nzma inajua .kila jeshi kutoka umoja wa Maarifa Lipo hapo linawalinda lkn kila siku n mauaji ,manyanyaso inamaana hayo majeshi yameshindwa kukomesha uhalifu .au ndo yale ya kuku kaponzwa na rangi kwa MGANGA ..husikii africa waakisema black live matters hapa .kimya ! Wanafikiri hayawahusu

Poleni sana WANAIGERIA kwa yanayoendelea tunayaona na Dunia nzma inajua Cha ajabu nchi nyngi Za africa zimekaa kimya! Hakuna cha black live matters wala nini wanadhani hayawahusu na wapo salama ..Je upo salama kwa kiasi gani? .Leo kwake Labda kesho kwako.. TUPAZE SAUTI !ili yasijirudie rudie .

Poleni watu wa hiz nchi zifuatazo Syria,palestina,Libya ,Somalia ,Sudan kusini ,Iraq na pengne pote panapomwagika Damu za bure !. hakuna marefu yasiyokuwa na ncha Dhulma hizo zitalipwa tu .

Unaweza kuta anayewauzia wenzake silaha ndio huyohuyo anaunga mkono vikundi vya kiuhalifu,anaunga mkono fujo ktk jamii,anatufarakanisha bila kujijua tunaingia mtegoni tunamalizana

Unaweza kuta anayetengeneza Ugonjwa ndiye huyohuyo anayetengeneza Dawa za kuponya ugonjwa husika lakin sio wote

Unaweza kuta Anayeuza Madawa ya kulevya(cocaine) ndiye huyohuyo anayetoa methadone(dawa za kupunguza makali ya matumizi ya unga) kwa wale waathirika ili wapone , polen na mpone haraka nafaham sio wote waliingia kwa kupenda.

Wana wa Nchi Naomba tuizungumze Siasa kwani ndio hio hio tu Dunia nzma ila watendaji wa siasa tu ndo hutofautiana

Kuna rafiki yangu alishawahi kuniambia nami nakubaliana nae ya kuwa Siasa ni Maisha na Maisha ni Siasa na kama inatokea mtu hataki kushiriki Siasa basi atashirikishwa kilazima hivi unajua kuwa hata "MAITI" inashiriki Siasa ndo maana kuna kamati ya Mazishi na ina MWENYE KITI.

Plato myunani anakoleza "gharama atakayolipia mwerevu ambae ashiriki siasa ni kuongozwa na asiyemwerevu ambae atakupangia kila kitu kwenye maisha yako".

Vijana wengi wamebaki "Empty set" juu ya historia za nchi zao na nchi nyngne hivyo kubakia kuwa washabiki tu so sad! Fuatilia upate Maarifa na sio taarifa ! Rejea kitabu cha "KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU" Cha Harrithy Ghassany .

Hivi karibuni nchi ya Tanzania itaenda kutekeleza lile tendo muhimu la katiba ibara ya tano(5) ya jamhuri ya muungano wa Tanzania..Yaani uchaguzi,kisha teuzi nk

Japo kuna mstari mwembamba sana Kati ya siasa na fitna lakini mpaka sasa nayaona yote tambarare na sarakasi Viongozi wengne wanaambiwa hawajafanya kitu, wengne wanatuahidi watatufanyia Vitu,hoja nyngne za wakuu za miguu kuwa juu na vichwa Chini ndo siasa hizo! porojo humo humo .Muhimu tuache udodoki ,tujitahidi kuchuja mwenye masikio na asikie na mwenye macho na aaone ..
Muhimu zaidi Tujitokeze kwa wingi tu kwa kila mwenye sifa kupiga kura na sio kula.

Na kuna baadhi wanaizungumza HAKi kuna wengne AMANI ..Mie nitavizungumza vyote kwa uchache kwa sababu yamesemwa sana ili AMANI na HAkI vipatikane baada ya uchaguzi Basi tupande Gari la "UADILIFU" tu vinginevyo n Giza tupu! aliloliandika Mwalimu Nyerere kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania".

Hatupo peke yetu kuna watu nje huko wanatutazama sina uhakika na kheri za Macho yao .Wawili kati yao wameanza kukohoa kwa mbaali tujitafakari sana , rejea kitabu cha "The New confession of economic hitman"kilichoandikwa na John Perkins , vile vile rejea kitabu cha "UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI" kilichoandikwa na Yericko nyerere utaelewa namaanisha nini .

HITIMISHO KWA UCHACHE (first 11 hio)

1) MWENYE ENZI MUNGU N mwngi wa kusamehe WANA wa Adam ,tufanye toba ya kweli ,tokea enzi hajawahi kumficha Mnafki.

2)UPENDO ni Suluhisho la matatizo yote Kwenye hii Dunia, Mother Theresa kalizungumza vizuri sana Hili .

3)Maisha n fumbo lisilo na majibu sahihi cheza kwa kusudi lako

4)kuna laana kubwa sana kwenye kutupa chakula jitahidi umpe hata jirani yako

5)Jamii zijenge utaratibu wa kusoma vitabu chanya na vya kijinga eeh ndio kwani hujui hata kwenye ujinga kuna kitu cha kujifunza pia soma japo kurasa nne kwa siku itakusaidia kuna masuluhisho mengi sana kwenye vitabu

6) Natamani kila mtu asome vitabu vifuatavyo

A)"UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA" & "TUJISAHIHISHE" mtunzi ni MWALIMU NYERERE

B)"KWAHERI UKOLONI,KWAHERI UHURU" mtunzi Harrithy Ghassany

C)"THE NEW CONFESSION OF ECONOMIC HITMAN" mtunzi John Perkins

D)"HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE" Mtunzi Dale carnegie

E)"UNANSWERED CRIES" mtunzi Osman Conteh

7)Kwa mbaalii nayaona haya Serikali ya mseto au Serikali ile ile au AMANI na Haki au machafuko Baada ya uchaguzi huu.

8)Mshahiri MUYAKA BIN HAJI alituambia "Tusikidharau kimya, kimya kina mshindo mkuu ,kimya kina moshi mbele ,kimya kina angusha mwanzi"
Hivyo kimya sio ishara ya AMANI .

9)Tunafahamu nyie Viongozi sio malaika ila tambua kuwa UONGOZI n koti la kuazima ukiwa nalo litumie vizuri,Tujitahidi sana kuwa Waadilifu tupende kuchuja,Tuwe wazalendo Zaidi.

10)Japo kuwa nguvu ya Umma haijawahi kushindwa ila Sisi Watanzania tunachotaka n Maendeleo tu na sio kumwaga Damu kuna maisha baada ya uchaguzi.

11) Watanzania ! Watanzania ! Watanzania! Nawaita mara tatu,Tusijisahau Tuna nchi Moja tu ya Tanzania hakuna nchi nyngne yoyote ulimwenguni inayoitwa Tanzania.

NAKUPENDA TANZANIA NA DUNIA .
 
Shukran kwa uzi.
Nakushauri unapoweka idadi, weka tarakimu tu, wana JF wana akili timamu na watajua kuzidadavua. Ila unaposema kwa mfano milioni 300,000,000 wakati unachomaanisha ni 300,000,000 unakuwa umepotosha. Ukiinyumbulisha milioni 300,000,000 ina maana ni 300,000,000,000,000 ambalo si kusudio lako.
 
Why Africa and not the entire World? I didn't see anything specific regarding Africa in the thread.
the situation in the country is getting worst youth are tired with political lie and propaganda To be fair the ruling party is a disgrace to Tz and Tanzanian the lives of the citizens was in danger, some are dying with penury may Allah rescue Tanzania
 
Nakupenda Tanzania, Mungu ibariki Tanzania asante kwakunijenga kifikra
 
Nakushukuru sana Mkuu kwa kunirekebisha .Binafsi nitalifanyia Kazi na ndio maana nafarijika kuwepo humu JF .kuna watu makini sana ukiwemo wew sijui kwanini nilichelewa kuingia humu JF.

Turudi kwenye Mada kuu kama waafrica tunapaswa kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya kuendea pwani yetu ya maendeleo ikiwemo pwani ya elimu ,pwani ya siasa ,pwani ya uchumi,pwani ya kijamii

Tunafahamu sio rahisi lakin Tutajaribu kwa kishindo Mungu yu pamoja na Mwenye Haki .
 
the situation in the country is getting worst youth are tired with political lie and propaganda To be fair the ruling party is a disgrace to Tz and Tanzanian the lives of the citizens was in danger, some are dying with penury may Allah rescue Tanzania
True naked something tremendous must done!
 
Nakupenda Tanzania, Mungu ibariki Tanzania asante kwakunijenga kifikra
Tupo pamoja mkuu, Tusiishie kuipenda Tanzania Pekee Bali Tuipende na DUNIA nzima pia .mfano; cheki hizi nchi Syria ,Beni ,palestina nk mwanzoni mwa janga la Covid 19 . G.S wa U.N Mario Guterres aliomba Vita visitishwe ili kupisha janga hili na kweli vita ilitulia .

Maswali fikirishi hivi kumbe kuna uwezekano wa kumaliza vita?

Je Kuna ulazima wa kusubiri CovId 19 kisha ndo kuwepo kwa kusitisha vita?

Nani yupo nyuma ya hizo vita au vurugu ambawo wanashindwa kudhibitiwa na DUNIA?

Nani anayesupport hizo silaha hatarishi kwa hivyo vikundi ?

Je vita hivyo n kwa maslahi ya nani ?

Maswali n mengi kwa hawa Watesi kuliko majawabu yao kwetu ..
 
the situation in the country is getting worst youth are tired with political lie and propaganda To be fair the ruling party is a disgrace to Tz and Tanzanian the lives of the citizens was in danger, some are dying with penury may Allah rescue Tanzania
Amen!
 
Why Africa and not the entire World? I didn't see anything specific regarding Africa in the thread.
Mkuu uchawi na unafiki so ndii uneatamalaki Afrika. Umwagaji chakula so tunaongoza Afrika! Nenda sokoni angalia matunda mengi huwa yanakaribia kuoza.Nenda dampo la sokini urajionea.
 
Back
Top Bottom