Mungu na vifo vya binadamu

Mungu na vifo vya binadamu

Nameless-

Member
Joined
May 21, 2009
Posts
47
Reaction score
1
Wakuu kuna misemo naisikia mara nyingi hususan katika misiba na sielewi hasa maana yake, mwenye uelewa eneo hili naomba anieleweshe. Mfano, mtu anaposema "Tulimpenda zaidi huyu (yaani marehemu) lakini Mungu kampenda zaidi" Hivi Mungu anapenda mauti yatukute wanadamu? Hii kauli huwa inanitatanisha na hasa ninapoambiwa ktk misiba niliyopoteza ndugu zangu.
 
mmh Nikitoka Lunch nitakuja ...
Nadhani mungu anakuwa ameamua kuvuna katika shamba lake
 
"...kuvuna katika shamba lake", mmmh, msamiati mwingine.
 
tukiwa matumboni mwa wazazi wetu, tunaweka ahadi na mungu juu ya vifo vyetu, hivyo tunapokufa ni ahadi tulizoweka zimetimia tu, ndio maana wanasema tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi. na huu ni msemo kuwafariji ndugu wa marehemu.
 
Bwana AMETOA na bwana AMETWAA jina la bwana libarikiwe......
 
tukiwa matumboni mwa wazazi wetu, tunaweka ahadi na mungu juu ya vifo vyetu, hivyo tunapokufa ni ahadi tulizoweka zimetimia tu, ndio maana wanasema tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi. na huu ni msemo kuwafariji ndugu wa marehemu.

Duh uongo mtakatifu hahahahahaaaa......
 
hii thread ni mahsusi kwenye jukwaa la 'dini'.
 
Back
Top Bottom