Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,097
Inafundishwa ndani ya Kuran tukufu kuwa Mungu alipowaambia malaika habari za ujio wa binadamu walikataa. Walimwambia Mungu: "Je, unataka kuleta binadamu ili wamwage damu?"
Mungu alipenda sana uwepo binadamu duniani. Injili takatifu (ndani ya Biblia) inafundisha kuwa binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu, ingawa Kuran inapinga kuwa Mungu hafananishwi na chochote.
Turejee kwenye ujio wa binadamu. Mungu aliwahoji malaika: "Mnaposema binadamu wabaya na watamwaga damu duniani, je mnamjua Adam?"
Ni kwamba malaika walikuwa wameshaona mbali kuwa binadamu ni wazinguaji. Uwepo wao ungeifanya dunia kuwa na hekaheka nyingi. Mungu aliamua kutumia mamlaka yake na kumuumba Adam.
Baada ya Mungu kumuumba Adam, alimpa elimu ya vyote vilivyomo duniani, hivyo akawa anajua kila kitu kwa majina. Mungu alitaka kuwathibitishia malaika kwamba alifanya uumbaji bora kwa kiumbe mwenye kuitwa binadamu.
Basi Mungu aliwaita malaika na kuwauliza majina ya vitu vilivyomo duniani, kuanzia mimea mpaka wanyama, bahari, maziwa, mito, mabonde na milima. Hakuna malaika aliyejua japo jina moja. Adam alipoulizwa, akataja majina yote kwa ufasaha.
Adam alipotaja majina yote kwa usahihi, Mungu aliwaambia malaika: "Si niliwaambia binadamu ni kiumbe mwenye daraja kubwa?" Baada ya hapo akawaambia malaika wamsujudie Adam. Malaika wote walisujudu isipokuwa Ibilisi.
Katika Kuran, inafundishwa kuwa Shetani alikuwa malaika na jina lake ni Ibilisi. Yeye ndiye aligoma kumsujudia Adam. Shetani alimgomea Mungu kwa kuona kuwa anamkweza kiumbe ambaye hana msimamo. Kiumbe ambaye ni mwepesi kudanganywa.
Kwa kifupi ni kuwa Mungu alimuumba binadamu kwa imani kubwa. Hata hivyo, Shetani (Ibilisi), alimdharau binadamu tangu siku ya kwanza. Shetani alimuona binadamu ni kichwa kidogo, kichwa cha panzi. Akishawishiwa kidogo anamuasi Mungu.
Kwa kosa la Ibilisi kumgomea Mungu kumsujudia Adam waziwazi, ilikuwa dharau kubwa. Mungu alimlaani Shetani na kumfunga minyororo ili amuangamize. Hata hivyo, Shetani aliomba kuwekeana ahadi na Mungu.
Shetani aliomba apewe uhuru wa kuwadanganya binadamu ili kumthibitishia Mungu kwamba binadamu anaowapenda na kuwaamini, uwezo wao wa kuchanganua mambo ni mdogo.
Shetani aliomba kwa Mungu jukumu la kuwapotosha binadamu ili kudhihirisha kweli alikuwa sahihi kukataa kumsujudia Adam. Mungu akakubali ombi hilo. Shetani akaingia kazini kuwadanganya binadamu.
Mafanikio ya kwanza ya Shetani yalianzia kwa Adam na ameendelea kufanikiwa kwa kishindo zaidi.
Utaona kuwa dhambi na thawabu ni maafikiano ya Mungu na Shetani. Mungu aliamini binadamu ni bora na watakuwa kwenye mstari siku zote. Shetani akasema binadamu ni sifuri, atawaingiza wote dhambini.
Unaweza pia kujiuliza; kama si mapatano ya Mungu na Shetani kuhusu dhambi, dunia ingekuwaje leo? Upande mwingine dhambi ndiyo zinaleta umaridhawa wa dunia. Binadamu wote wangekuwa watakatifu ingekuwaje? Bila shaka ingekuwa salama ila isingekuwa maridhawa.
Nipo..