Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Anaandika Robert Heriel,
Mtibeli.

Kuna Mungu Muumba wa mbingu na nchi halafu kuna miungu. Mungu Mkuu ambaye hajawahi kuonekana na kamwe hatokuja kuonekana Daima milele, hawezi kufanya wala kuwaza huo upuuzi wa kuchoma watu, hilo haliwezekaniki!

Miungu hii inayoabudiwa ndio inaweza kufanya hivyo, lakini yule Mungu wa miungu huo muda hana, na hawezi kufanya hivyo.

Mungu Mkuu ni Upendo, na kamwe upendo haulazimishwi. Yaani, ati Mungu aliyekuumba akulazimishe umpende (umuabudu) wakati alikuwa na uwezo wa kukuumba automatic ukawa unampenda!

Kwanza umpende (umuabudu) ili yeye apate nini? Halafu usipompende ati akuchome, wewe kosa lako lipo hapo? Yaani moyo wako haumpendi Mungu aliyekuumba, unapenda jambo jingine nini kosa lako, iko wapi haki hapo?

Mungu mwenye Upendo na muweza wa yote, anataka mtu apende anachokipenda! Kwanza yeye ndio aliyekufanya uwe hivyo ulivyo, upende unayoyapenda, achana na yale unayoyatamani na kuyachukia.

Huwezi lazimisha kupendwa bhana, na kamwe Mungu hawezi kukulazimisha umpende. Kukulazimisha haibadilishi ukweli kuwa haumpendi. Kumbuka Mungu ni Haki na Kweli.

Mchongo ukoje? Ipo hivi;

Jinsi uonavyo Ulimwengu wa nje (huu unaoonekana) ndivyo katika Ulimwengu wa ndani usioonekana, Ulimwengu wa Nafsi.

Itazame Dunia, Dunia ni moja lakini inamazingira tofauti tofauti, kuna sehemu zenye baridi kali mpaka barafu, kuna sehemu za jangwa, kuna sehemu za hali ya hewa ya kati, kuna sehemu zenye mvua nyingi, na zipo zenye mvua za Waarabu.

Kuna milimani na mabondeni, sehemu zenye maziwa, mito na bahati, sehemu yenye misitu mine, nyasi na vichaka, sehemu yenye wanyama wa aina hii sehemu nyingine hakuna.

Sasa ni uchaguzi wa mtu kutumia kile akipendacho, ukitaka kuishi kwenye baridi ni wewe, Mungu hawezi kukulazimisha uishi sehemu isiyo ya baridi wakati wewe unapenda. Haipo hiyo. Ukitaka kula chakula au wanyama fulani ni wewe mwenyewe.

Ila elewa kuwa vipo vitu ni sumu na cool vitu sio sumu. Ni wewe mwenyewe unachagua ule sumu au usile. Nasema ni wewe mwenyewe, ni kutokana na upendo wako.

Kama unavyoishi hapa Duniani kulingana na umri wako, jinsia yako, kipato na hadhi yako, mtazamo wako ndivyo nafsi yako itakavyoishi baada ya mwili wako kuondoka.

Mfano huwezi ishi Masaki, Mikocheni, Upanga wakati kipato chako na daraja lako ni kuishi kwa walalahoi huko.

Kunguru na njiwa hawawezi kaa pamoja, wanasema ndege wafananao huruka pamoja. Nenda hata wodini huko mahospitalini utaona kabisa kuwa mgonjwa wa akili hawezi lazwa wodi ya wazazi au mgonjwa aliyemahututi hawezi lazwa wodi ya wagonjwa wa meno.

Maisha ni uchaguzi wa mtu mwenyewe. Mungu kamwe hana huo muda wa kukuamulia nini chakupenda. Kuku hawezi zaa bata, kila mmoja atakaa sehemu yake. Vivyohivyo hata ukifa roho yako itaenda mahali inapopapenda, na wala hautachomwa moto.

Kama unapenda uzinzi na kuchukua wake za watu na kuua watu basi nafsi yako itaishi katika Ulimwengu wa watu wa aina yako ili mchukuliane wake na waume zenu kwa jinsi mpendavyo, ili muone utamu wa kile mnachokipenda.

Sheria siku zote sio upendo, Sheria hizi za nchi zipo kwaajili ya kudhibiti matendo ha mwili na sio nafsi. Upendo upo kwenye nafsi ya mtu wakati sheria ipo katika mwili wa mtu. Mtu anapoua akahukumiwa jela kinachoadhibiwa ni mwili wake lakini nafsi yake haiadhibiwi.

Utalipwa sawasawa na matendo ya nafsi yako, Dhamiri na utapelekwa kwenye Ulimwengu unaofanana na nafsi yako. Hiyo ndio tafsiri ya moto wa Jehanum na sio kuchomwa kama wengi walivyotafsiri au wanavyojua.

Mungu Mkuu hukupa na anatoa kitu kulingana na mtu au kiumbe husika, Ulimwengu wa wapenda haki, wapenda dhulma, wenye upendo, wenye chuki, wasema uongo na wauaji, ulimwengu wa wasema kweli na watoa uzima.

Ni wewe tuu unachagua wapi unapenda na hayo ndio yatakuwa maisha yako mpaka Mungu Mkuu atakapoona imetosha. Ukitaka kubadili vitu upendavyo ni wewe, lakini mpaka Mungu atakapoona inatosha, uende katika Ulimwengu mwingine.

Ni kama hapa Duniani, vile unavyoishi ndivyo ulivyoamua kuishi au wazazi wako walivyotaka uishi (kumbuka ulikuwa katika mwili wa wazazi wako). Hakuna kulaumiana wala hakuna wakumlaumu. Hayo ndio maisha!

Acha nipumzike sasa,
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Ngoja wazee wa thibitisha waje...

😀😀

Waliumbwa hivyo.
Hawatakuja Kupata uthibitisho Kwa sababu hakuna aliyewahi kumuona huyo Mungu Mkuu, Kwanza Hana mfano, alafu hafanani na chochote, yaani Kwa Lugha nyepesi ukisema hayupo haujakosea na ukisema yupo haujakosea.

Na kusema Mungu Mkuu hayupo haibadilishi chochote kuwa yupo au hayupo, haimuumi Kwa sababu hata Hilo wazo la kusema hayupo au yupo linatoka kwake.
 
Mungu ni upendo, na anataka tumpende na tumtii pasipo sababu yeyote ile, hana vitisho wala ubaguzi wa aina yeyote kwa wanaomtii na wasiomtii, mbele yake ni wote tupo kwenye kapu moja.

Mkuu moto unaozungumzwa hasa kwenye biblia ni lugha ya picha tuu, wala sio huu moto tuujua sisi kama matokeo ya fuel, heat na oxygen hewa. Huo moto ni HALI tu, wala sio MAHALI, au MOTO wa kuonekana kwa macho kwamba huo au ule pale unachoma watu.
 
Unaposema Mungu anataka tumtii alafu kuna Watu hawamtii sijui unaielewa hiyo statement? Haipo Logically Kwa level na sifa za Mungu.

Mungu angetaka tumtii na tufanye Yale ayatakayo kama yaliyoagizwa na miungu(ya kwenye hizi dini tulizonazo) tungefanya pasipo kuhubiriana wala hizi hadithi.

Mungu anataka Dunia iwe hivi kama ilivyo na sio vinginevyo.

Mungu atake alafu kuna viumbe havitaki na vinashinda matakwa ya Mungu, hiyo inawezekana?
Kwa mfano Mungu ndiye anataka Watu wale chakula, uliwahi sikia wapi mtu akilazimishwa Kula chakula? Labda awe mgonjwa au amepewa chakula asichokitaka.
Kula ni amri na matakwa ya Mungu, kulala,
Kuvaa sio lazima,
Kufa ni matakwa ya Mungu,
Takwa la Mungu ni lazima.

Yaani unazaliwa nalo
 
Muombe Mungu akusamehe kwa Uzi Huu, Kisha waombe Mods waufute Uzi Huu!!.

Ni Mungu huyuhuyu muumbaji na Upendo, aliwachoma moto sodoma na gomora sijataja zama za Nuhu, huyu Mungu alompa Samson nguvu awauwe wafilisti na maadui wa Israel, ni Mungu huyohuyo alokua anawaagiza Wana isarel wawaue maadaui zao kuanzia Watu mpaka Kuku !!.

Ni Mungu yule yule alombariki Eliya, Ayubu, Daudi,

Ni Mungu yuleyule alomponya Jenerali Naamani na wengine.

Ni Mungu alomfufua Lazaro ,na wengineo !!.

Ni Mungu yuleyule anayeturuhusu tupumue Hata Sasa tunapoandika hapaa !!!.

Kwa sisi tuonafanya kazi Ma Hosp, tunaelewa Kifo ni nini !! Na kwamba, Huchukua Sekunde Moja tu kubadili Historia ya mtu kutoka mtu kuongea, mpaka mtu kushindwa hata kufungua jicho !!.

Ni Mungu huyuhuyu aloruhusu uwe hapo ulipo.

Ni huyohuyo Mungu, aloiweka ahadi ya kutoigharikisha Dunia Kwa maji badala yake akasema, NITAICHOMA DUNIA NA WADHAMBI WOTE KATIKA ZIWA LIWAKALO MOTO.

Njia pekee ya kuukumbia Huu moto ni Kutokufanya dhambi, na tutaliweza Hilo Kwa kumuomba Mungu ili atupe Uwezo na neema zake, huku wenyewe tukichukua Jitahada binafsi.

HAKIKA, KICHWA CHA MWANADAMU KINAWAZA UPUMBAVU,,,, ILA MWANADAM ANAPOFIKIA HATUA YA KUFANYA KUFURU KWA MUNGU, NI ZAIDI YA UPUMBAVU !!.

UWEZO NA UKUU WA MUNGU, KAMWE HAUCHUNGUZIKI !!! NI MUNGU ATABAKI KUA MUNGU !!.
 
Mungu ni upendo, na anataka tumpende na tumtii pasipo sababu yeyote ile, hana vitisho wala ubaguzi wa aina yeyote kwa wanaomtii na wasiomtii, mbele yake ni wote tupo kwenye kapu moja.

Mkuu moto unaozungumzwa hasa kwenye biblia ni lugha ya picha tuu, wala sio huu moto tuujua sisi kama matokeo ya fuel, heat na oxygen hewa. Huo moto ni HALI tu, wala sio MAHALI, au MOTO wa kuonekana kwa macho kwamba huo au ule pale unachoma watu.
Hata kama sio moto bali ni hali tu iweje iwe ya mateso? Yaani kwanini atutese?
Yeye achukue watu wake wanaomwamini na wasiotenda dhambi, hao wengine aachane nao , iweje iwe lazima kufata anavyotaka yeye?

Hapo hapo katumwaga humu duniani tumejikuta tunatofautiana kiimani tunapigana vita wenyewe kwa wenyewe, ili iweje sasa?
Alishindwaje kufanya tuwe na imani moja anayoitaka yeye?
Anatuchanganya haeleweki
 
Mungu anaeleweka Kwa kiasi, Ila kuna Watu wanaumba miungu Yao na kulazimisha Watu kuwa waifuate.

Hakuna atakayeishi na Mungu au atakayechukuliwa na Mungu. Kila mtu ataishi vile apendavyo na watu wenye tabia kama zake. Hiyo ndio HAKI.

Lakini kuwakataza Watu waache Pombe au Kula Nguruwe au kuzini Wakati huenda ndio wanapenda hiyo haitakuwa upendo tena. Watu wapewe wanachotaka na wawekwe kimakundi yao
 
Muombe Mungu akusamehe kwa Uzi Huu, Kisha waombe Mods waufute Uzi Huu!!.

Ni Mungu huyuhuyu muumbaji na Upendo, aliwachoma moto sodoma na gomora sijataja zama za Nuhu, huyu Mungu alompa Samson nguvu awauwe wafilisti na maadui wa Israel, ni Mungu huyohuyo alokua anawaagiza Wana isarel wawaue maadaui zao kuanzia Watu mpaka Kuku !!.

Ni Mungu yule yule alombariki Eliya, Ayubu, Daudi,

Ni Mungu yuleyule alomponya Jenerali Naamani na wengine.

Ni Mungu alomfufua Lazaro ,na wengineo !!.

Ni Mungu yuleyule anayeturuhusu tupumue Hata Sasa tunapoandika hapaa !!!.

Kwa sisi tuonafanya kazi Ma Hosp, tunaelewa Kifo ni nini !! Na kwamba, Huchukua Sekunde Moja tu kubadili Historia ya mtu kutoka mtu kuongea, mpaka mtu kushindwa hata kufungua jicho !!.

Ni Mungu huyuhuyu aloruhusu uwe hapo ulipo.

Ni huyohuyo Mungu, aloiweka ahadi ya kutoigharikisha Dunia Kwa maji badala yake akasema, NITAICHOMA DUNIA NA WADHAMBI WOTE KATIKA ZIWA LIWAKALO MOTO.

Njia pekee ya kuukumbia Huu moto ni Kutokufanya dhambi, na tutaliweza Hilo Kwa kumuomba Mungu ili atupe Uwezo na neema zake, huku wenyewe tukichukua Jitahada binafsi.

HAKIKA, KICHWA CHA MWANADAMU KINAWAZA UPUMBAVU,,,, ILA MWANADAM ANAPOFIKIA HATUA YA KUFANYA KUFURU KWA MUNGU, NI ZAIDI YA UPUMBAVU !!.

UWEZO NA UKUU WA MWANADAMU, KAMWE HAUCHUNGUZIKI !!! NI MUNGU ATABAKI KUA MUNGU !!.

Wakati Tsunami inatokea nafikiri ilikuwepo.
Embu tuambie wale waliokuwa Kwa tsunami na Sisi Nani waovu Sana na Nani wema Sana?

Kufa haijawahi kuwa adhabu, Kufa ni asili ya kiumbe Chenye mwanzo(kilichoumbwa)
Unaweza ukafa Kwa Moto, au maji, au Jambo lolote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom