Mungu kwanza mambo mengine ni baraka

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania !

Leo napenda kushirikishana nanyi kuhusu habari juu ya Mungu sambamba na maisha kwa ujumla.

Nawaombeni sana wa Tanzania mjitahidi kumtafuta Mungu zaidi kuanzia kwenye moyo wako, akili yako, roho yako na nguvu zako ulizonazo aidha kubwa au ndogo. Hapa ndugu msomaji, kuna faida nyingi sana ukiweka jitihada na uwezo wako wote kumuhusu Mungu.

Faida

(a) Huwezi kuhofia maisha kabisa maana utakuwa unajua umuhimu wa kushukuru na kukana lawama.

(b) Huwezi ogopa chochote maana utayaweza mambo yote hakuna kitakachokushinda ukiongozwa kukifanya au kukitenda.

(c) Msamiati wa kifo kwako hautakuwepo hutakaa upoteze muda kuwaza au kuzungumzia huo msamiati maana kwako haupo.

(d) Utakuwa na utu sana pamoja na amani kuu ndani yako. Hapa utajua umuhimu wa utu kwa kutofautisha na vitu.

(e) Mungu atakufungulia milango na kukupatia baraka tele zisizopimika.


NB

Watu wote wanaohangaika na maisha na mambo ya hii dunia wanatawaliwa na kutaka sifa, hawana amani moyoni mwao, wanahofu na kifo, wanathamini vitu kuliko utu ili hali wanatamani kutendewa utu, wanawaza kesho zao ambazo hawazijui na mwisho kila kitu walichokipata kwa kuviangaikia huwa haviwasaidii.
 
Cha ajabu ni kwamba bandiko hili haliwezi kuwa na comments nyingi kwasababu wanadamu wengi wa zama hizi hasa vijana tumefungwa ufahamu na yule mwovu shetani.

Sasa weka bandiko lenye kichwa cha habari : NAMNA YA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI KWA HARAKA..halafu uone huo utitiri wa comments!

Mungu atuhurumie sana kwa kweli.
 
Back
Top Bottom