fukuza huyo dada yako bora lawama kuliko kuishi na majonzi moyoni
bora aumie mtu mmoja kuliko roho 100 zipotee
pole sana kwa kupoteza mke jamani... ila sio vizuri kumtuma huyo mchumba wako kwa sasa tafuta ndugu mwingine akusaidie hadi muoane
Pole sana kaka,chukulia yote kama mitihani ya mwenyezi mungu na inshallah mungu atakupa uhai mrefu uweze kuwalea watoto wako kwa mapenzi na imani ya dini yako,bila kusahau kumuombea dua mzazi mwenzako alie tangulia mbele ya haki..
Kuhusu huyo mdogo wako anaglia sana sababu ndugu wengi hawaelewani na mke ambae hapendi kufuja vitu,huyo mchumba wako angekua mfujaji kama yeye au angekua kamtafuta yeye wangeiva lakini hapo ameshaona kitumbua chake nishaanza kutiwa mchanga ndio mana maneno mengi yatasemwa,chamsing ni wewe kua na mamuzi yakiume,sababu huwezi huwezi kuridhisha wote.
basi kwa muda huu ambao una ubavu wako jitahidi kufanya mambo yako mwenyewe. si unajua wanawake hatupendani? yaani kaka amtume mpenzi wake nyumbani kuleta hela home yaani hilo liwivu halibebeki bwana.Niliwahi kumtumia kaka yangu mkubwa hali ndio ikawa balaa, kazi ya milioni 2 ilifanywa kwa milioni 8 na nusu na haikuisha hadi leo!
Undugu si kuzaana, undugu ni kufanana. Inaonekana unafanana na huyo binti mwingine na si dada yako. Ondoa haraka huyo dada ambatana na huyo mnayefanana (kimawazo) ili ujenge maisha yako, yake na ya watoto wakoMke wangu alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita, alifariki kifo kibaya sana maana aliniachia mtoto mchanga wa wiki tatu. Baada ya kuhuzunika sana sikuwa na jinsi, nikamuomba Sister wangu ahamie kwangu ili maisha ya pale home yasisimame maana nina mtoto mwingine mkubwa kidogo. Yule mdogo alichukuliwa na Bibi yake.
Sasa sister kanigeuka yaani, amekuwa ni mtu wa kujiachia mno na maisha, bahati mbaya kazi zangu ni za kusafiri safiri sana sasa kila ninaporudi nyumbani ni kukarabati vitu tu maana hakuna usimamizi kabisa, mwanangu huyo mkubwa ni kama anajilea mwenyewe akifanya homework ni sawa asipofanya ni sawa pia! Muda mwingi sister anakuwa kazini na kwenye mishe mishe. Kila nikianzisha kaujenzi fulani pale home au chochote pesa inaishia kwenye castle lite tu sasa hata pesa nayotoa ya kula inaishia kwenye castle lite na viwanja, mtoto anakula 'kinachopatikana'.
Nikapata mwenzangu nikaanza kumshirikisha na maisha yangu, kama kununua chakula na kuwapelekea pale home au kama kuna ka project namtumia pesa awalipe mafundi sasa kumewaka moto! Sister anani mind ile mbaya na anazambaza maneno hasa kwa ndugu na jamaa, wamemchafua mno binti wa watu kuanzia kuambiwa mshirikina na mengineyo ila mimi, baba yangu na baadhi ya ndugu hatuuoni huo ubaya wake, nifanye nini waungwana wa JF? lengo langu ni kumuoa huyu binti na kujaribu kujenga upya familia yangu, hadi sasa sijaona kosa lake na anaonekana kumjali mtoto wangu(?).
"Bwana(Mungu) ametoa na Bwana ametwaa..."
Hayo ni maneno ambayo pasi na shaka umekuwa ukiyasikia.
Mungu alimchukua mkeo kwa kuwa ndiye aliyemuumba.
Pili, huyo dada yako uliyemwalika nyumbani kwako, kipi kinakushinda kumuondoa??
ustaarabu wa kumtoa hapo ni kumtafutia mume aolewe tu basiLait noir ("maziwa meusi"!?) kwanza pole kwa kuondokewa na mkeo.
Je hakuna namna ya kumwondosha (kistaarabu!) huyo dadako na kuweka mtu/ndugu mwingine kwa muda? Kwa jinsi ulivyosimulia huyo dadako ni hatari maana ameshindwa kutunza nyumba na bado anataka kukuzuia usio mtu unayempenda!
Kama huyo binti umempenda, muoe fasta ili akae hapo nyumbani na kuweka mambo sawa. Huyo dada yako mrudishe kwa wazazi wake akaendelee kujifunza maisha kwanza.
ustaarabu wa kumtoa hapo ni kumtafutia mume aolewe tu basi
Nikimuondoa kwa sasa nani atabaki na nyumba sasa kiongozi?