JumaKilumbi
JF-Expert Member
- Sep 7, 2022
- 432
- 507
Dini zilikuwepo tangu enzi na enzi, jamii za wanaadamu zimekuwa zikiabudu vile wanavyoviita Mungu kwa miaka mingi sana hili halina ubishi.
Uwepo wake miaka mingi haina maana ni sahihi kuwepo wake maana hata uongo usipodhihirika huonekana ukweli miaka yote mpaka ukweli utakapofahamika.
Ila kuna sehemu ya watu kwenye jamii wamekuwa wakitilia mashaka na kukosoa wazo lenyewe la kuwepo kwa huyo anaeitwa Mungu. Wanaoamini (imani yoyote tu ‘as long as’ wanamuabudu wanachokiita Mungu) wanasistiza kuwa yupo na uwezo wake ni Mkuu sana.
Hoja za waumini nazifahamu baadhi, ila hoja za Atheist sijazielewa.
Ningependa kuwaelewa zaidi Atheists, Karibuni hapa Atheist walau mthibitishe (kama mtaweza) kuwa huyo wa kuitwa Mungu hayupo.
Lakini kwanza ni lazima tufafanue nini maana ya MUNGU, kwa maana kukurupuka kujibu swali ilhali hatujui maana ya dhana ya msingi wa swali itakuwa ni uhayewani wa kiwango cha juu sana.
Karibuni sana!