Ni hivi, hawa wanaojiita hayo majina wanajua kwamba mitume na manabii waliteswa na kupitia kwenye tanuru za moto. Sasa tuwapelekee moto kama hawataingia mitini?
Yesu wa Kenya anaenda kusulubishwa, manabii na mitume wa mchongo wakae kwa tahadhari
Amani iwe nanyi, Kazi ya Mungu siku zote ina upinzani mkali. Tumeona Yesu OG, mitume na manabii walivyo uwawa, teswa na kudhihakiwa. Soma maandiko kwa urahisi wa rejea. Huko jirani, wadau wanataka kumjambisha yule yesu wa mchongo, wanataka kumsulubisha kwa kadiri ya maandiko wakitarajia...www.jamiiforums.com
Hawa watu wanafanya mzaha na Mungu. Mwenye enzi Mungu si wakufanyiwa mizaha. Watubu na kuomba huruma yake
You are not mentally enough to argue with me.Mwendawazimu ni Yule anayekataa asichokijua na kumtukana asiyemjua
KUMBUKUMBU 13:1-4
Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Sijawahi sema uachane na Mungu, mpende bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, mpende na jirani yako kama nafsi yako.Hao wa udongo wako tangu enzi. Kapambane nao lakini usituambie tuachane na Mungu ati sababu ya hao wadanganyifu wachache
Ningekuheshimu kama ungesaidia wale wanaua watoto zao, wazazi wao, albino sababu ya kutafuta mafanikio. Vinginevyo nakuchukulia kama wewe ni agent wa Yule malaika wa sifa aliyetupwa kuzimu
Mkuu huwezi bishana na mwanamke wa kiafrika mwenye itikadi kali za kidini.Sijawahi sema uachane na Mungu, mpende bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, mpende na jirani yako kama nafsi yako.
Shida yangu ni kwa hao wachumia tumbo, wanaojifanya mawakala, madalali au wasemaji wa Mungu.
Kwa uelewa wangu, Mungu haitaji dalali, wakala au msemaji kwenye operations zake. Ametupa maandiko, yasome ujiratibu.
Twende naye hatua kwa hatua, ataelewa tuMkuu huwezi bishana na mwanamke wa kiafrika mwenye itikadi kali za kidini.
Hawezi kukuelewa.
You are not mentally enough to argue with me.
Tuishie hapa.
Sijawahi sema uachane na Mungu, mpende bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, mpende na jirani yako kama nafsi yako.
Shida yangu ni kwa hao wachumia tumbo, wanaojifanya mawakala, madalali au wasemaji wa Mungu.
Kwa uelewa wangu, Mungu haitaji dalali, wakala au msemaji kwenye operations zake. Ametupa maandiko, yasome ujiratibu.
Kuna upotofu gani katika kumuheshimisha Mungu? Mwenye enzi Mungu ni mwenye mamlaka na hana ubia na mtu yoyote, haitaji msaidizi wala wakala, wala dalali au msemaji katika operations zake.Tumia akili zako vizuri ujue jinsi ya kudeal na hao unaowaita wachumia tumbo ila usipotoshe watu
Kuna upotofu gani katika kumuheshimisha Mungu? Mwenye enzi Mungu ni mwenye mamlaka na hana ubia na mtu yoyote, haitaji msaidizi wala wakala, wala dalali au msemaji katika operations zake.
Alituumba kwa mapenzi yake na atatuchukua kwa mapenzi yake. Hana shirika na kiumbe chochote wala haitaji ushauri au msaada wowote kutoka kwetu wanadamu. Mungu hamtegemei mwanadamu kwa jambo lolote.
Hao vilaza wanajitukuza na kujitakafutiza kwa kujifanya kuwa na ubia au access na mipango ya Mungu, kwamba wanaweza kumfanyia Mungu uchawa ili wengine wapate msaada, pathetic
Hakika mkuu, lazima tuwarudishe kwenye utimamu wa akili, kama wanazoNi ukweli Mungu Hana dalali hapa duniani , uritiri wa madhehebu na dini ni miradi ya watu wachumia tumbo , Yesu kufa msalabani alivunja hii Aina ya utapeli , inashangaza mtu mzima na akili unakalisha tako kumsikiliza sjui mtume , mara nabii mara mchungaji ......
Walimu wa dini na madhehebu wanachukiana na kupondana , huku kila mmoja akijiona ni sahihi , hakuna Mungu anayeweza kubaliana na huu upuuzi ...
Yesu alikufa msalabani ili mataifa yote bila kujali tamaduni na matabaka waweze kumfikia Mungu direct onspot wanapomhitaji , wewe kazi yako ni kuwa serious tuu kuomba Kwa jina la Yesu na Mungu anasikia popote pale ulipo na mazingira yyte , cha msingi uwe na nia ya dhati ....
Ni upuuzi kutegemea dini na madhehebu , wachungaji na mitume Sjui manabii ni total ridiculously, yeye mwenyewe alisema Mimi ndimi mchungaji mwema , ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe , inakuwaje unamfata mtu aisee anakudanganya umpe hela ili Mungu akufanikishe how comes ?
Huna hoja zaidi ya propaganda za kidini.Huna base ya argument
Kwa mambo usiyoyaelewa Tulia kabisaa
Hao wanaojiita wachungaji, sijui kitu gani, wanafikiri wanaweza wakamfanyia Mungu uchawa? They must think criticallyWewe una shida sehemu, either Hujui unayoongea au hujui unalotaka!?
Kumheshimisha Mungu ndio kunapatikana kwa kufundisha na kuhubiri neno lake
Kama kuna wanaopotosha deal nao wao ila usigeneralize mambo
Huna hoja zaidi ya propaganda za kidini.
Nakubaliana na wewe mkuu.Nawafokea kwa karipio kali watu wote wanao tumia maandiko kuwahadaa walimwengu
Wapo watu wanaodhani ni ujanja au uwerevu ku-take advantage ya ujinga wa wenzao kwa kuwahadaa kwamba wao ni mitume au manabii au madalali au mawakala au wasemaji wa Mungu
Wanakusanya makundi makubwa ya watu wapumbavu na kuwachosha kwa ibada ndefu na kuwaaminisha kwamba wanawapa revelations au baraka za Mungu kwa imani ya kupata maisha ya furaha mbinguni au kwa njia ya kupata mali na heri hapa duniani.
Huu upumbavu umeenea kwa kasi na unachangamkiwa na watu wenye IQ ndogo wanao hadaa wajinga na wapumbavu wenzao. Unfortunately, nchi yetu ina mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu wapumbavu na huo ndiyo mtaji wao.
Nawafokea tena kwa karipio kali zaidi. This nonsense must stop. Mungu hana wakala,dalali ama msemaji huku duniani. Mungu haitaji hao watu kufanya shughuli zake. Hao watu ni viumbe tena dhaifu na kiufupi hawana mastahili yoyote mbele za Mungu.
Maandiko yako wazi, muombe Mungu wako na atasikia maombi yako. Hautaji mtu wa kati. Makinika na chukua tahadhari.
WajiratibuNakubaliana na wewe mkuu.
The warning must go to Pope as well. He must stop calling himself a representative son of God.
Utaratibu wa kutubu kwa binadamu mwenzetu ni batili
Mkuu acha hasira na popeNakubaliana na wewe mkuu.
The warning must go to Pope as well. He must stop calling himself a representative son of God.
Utaratibu wa kutubu kwa binadamu mwenzetu ni batili
Huyu kasema msitume sadaka lakiniView attachment 2606910
Kuna huyu mwingine