5th Estate
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 310
- 273
Majibu mepesi kama haya ndio yanafunga akili za watu. Ujiulizi kwanini kizazi kimoja kina pewa vitabu na kingine hakipewi.Wakijua au wasijue wewe inakuhusu nini na imani au wokovu wako?
Let the dead bury their dead. Acha wafu wazikane wao kwa wao. Sio kazi yako kujua walikula nini walichamba na nini wakati karatasi laini za kuchambia hazikuwepo.
Wakati wako ni sasa unaposoma andiko hili wala sio dakika moja ilopita.
Usiniulize habar za babu yako aliishije. Ukitaka kijua aliishije katambike kaburini kwake na sijui hata kama ana muda wa kukusikiliza kwani hatujui huko alipo anafanya nini na wala yeye sidhani hata kama anajua wewe unaishije leo.
Huwa sijadili habari habari za wafu kuwa waliishije.
Usijikane Jinsi ulivyo wewe una Mwili na Ndio ulivyo na Mungu ndio kakuumba Hivyi hivyoTatizo lako unadhani huo mwili wako ndiyo wewe.
Utakesha unamtafuta Mungu na hautamwona kamwe.
πππππ DaahKama imani ya mtu ina nguvu kiasi hiki Mungu wa nini sasa.
Mkuu napenda sana watu wanaofikiri Kwa akili huru, Mimi nishaanza kuamini shetani kwa maana ya kiumbe hayupo, ila mambo yote negative ie wizi, uzinzi, uuaji, matusi etc ndo shetani, yaani shetani ni vitendo na sio kiumbe. Kwasabu nafikiria Yana Lucifer (shetani) kaumbwa na Mungu (kama tunavyofundishwa) alafu baada ya kumuasi, Mungu anapigana vita na yeye. Yani Mungu anapigana vita na kiumbe chake??? Je malaika Michael, au Gabriel naye akiasi itatokea Tena vita huko mbinguni, je wakipigwa wataenda kuungana na Lucifer (shetani tunayehadithiwa) au watantengeneza nao ufalme wao??Sijakataa Unaposema Hayo kwamba Mungu ameumba ila Unaposema Amekuumba kwa Mfano wake. Je malaika na Majjini wameumbwa kwa Mfano wa nani!
Maana Unaposema Una Mfano wa Mungu basi Mungu wako ana Upendeleo
Mawe, Kokoto, dhahabu almasi zina Uhai ndugu yangu. Au zenyewe hazijaumbwa
Mungu hana Sifa hizo ulizoziweka Hapo. Mungu hasemi na yeyote yule. Kuwaza na Kuchanganua ni Viumbe ndio wana Sifa hizo
Kitu kilicho na uhai lazima Kife. Kuishi ni sifa za Viumbe ndugu yangu. Mungu hana Uhai na Wala haishi
Majini ndo Nini mkuu?@mbususu zenye mijicho mijubwa kama bakuli, si ni majini hayo?
Kwahiyo kuwa na Imani ni lazima umjue Mungu?[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Daah
Kwa hiyo chombo kama chombo unaweza kukila bila msosi ndani yake? Imani na chombo ni sawa. Chombo kidogo msosi kidogo, chombo kikubwa msosi mwingi. Hakuna chombo hakuna msosi.
Imani.
Kitabu kilichoandikwa na Binadamu au Mungu!Kwenye vitabu husika.
Swali zuriKitu kisicho na uhai kinaweza kuumba viumbe vyenye uhai na kuvisimamia katika kupata riziki zao au kuendesha maisha yao?
Kwahiyo wewe akili inakwambia Mbingu ipo juu ya mawingu??Mwanadamu kumuwaza Mungu hutaweza kumpatia picha mwisho unaweza ukajikuta unakufuru tu.
MWENYEZI MUNGU YU HAI MILELE DAIMA.
Hivi ulishwahi kujiuliza hizi mbingu zimewezaje kuwa juu yetu pasi na kuwekewa nguzo yoyote ile unayoiona?
Ni nani anaezishikilia hizi mbingu zisitufunike tulio chini yake?
Vp huyo anaezishikilia akisinzia sisi tuliochini yake tutakuwa katika hali gani?
Ukishajiuliza swali hili ndio utajua kuwa MUNGU yupo hai au amekufa!
Kila Kiumbe kilichoumbwa na Mungu kilipewa mahali pa kukaa na Uwezo wa akili. Kutokana viumbe kupenda Kutawala mfano mzuri ni Ukoo wa Majini (shetwani ), malaika, elians na wengine upotoshaji ndipo unapoanza
Na hata Binadamu sasa tunataka kwenda Sayari zingine. Hao viumbe wengine wao walishakuja duniani muda mrefu na wakatupotosha na kuleta Teknolojia zao huku(kumbuka kuna Mambo yapo Duniani wanasayansi hawana Majibu yametokea wapi na Yamejengwa na Nani)
Viumbe hawa ndio wameleta mpaka hzii dini za upotoshaji zilizopo leo hii ambazo ndizo zinakuambia Mungu anataka Hiki na Ukimnyima anakulaani
Ndio hawa hawa wanawatokea manabii walioandikwa kwenye vitabu wanamwambia wasome kwa jina la Mola wao. Ndio hawa hawa wanakuja kwa njia ya Moto kuwaka kwenye Kichaka na Kuwaambia wavue viatu ni sehemu takatifu
Usijikane Jinsi ulivyo wewe una Mwili na Ndio ulivyo na Mungu ndio kakuumba Hivyi hivyo
Rudi kwenye post yangu hapo juu nilipoelekeza imani inavyofanya kazi.Kwahiyo kuwa na Imani ni lazima umjue Mungu?
Mungu kama hana sifa ya kuishi basi hayupo, ili awepo lazima awe na sifa ya kuishi. Na kuhusu kutokuwa na sifa ya uhai. Embu tuambie uhai ni nini? Na kinyume cha neno uhai ni nini? Kama Mungu hana uhai atakuwa ni mfuSijakataa Unaposema Hayo kwamba Mungu ameumba ila Unaposema Amekuumba kwa Mfano wake. Je malaika na Majjini wameumbwa kwa Mfano wa nani!
Maana Unaposema Una Mfano wa Mungu basi Mungu wako ana Upendeleo
Mawe, Kokoto, dhahabu almasi zina Uhai ndugu yangu. Au zenyewe hazijaumbwa
Mungu hana Sifa hizo ulizoziweka Hapo. Mungu hasemi na yeyote yule. Kuwaza na Kuchanganua ni Viumbe ndio wana Sifa hizo
Kitu kilicho na uhai lazima Kife. Kuishi ni sifa za Viumbe ndugu yangu. Mungu hana Uhai na Wala haishi
Mungu hafanani na kitu chochote alafu hapo Mungu kaumba mtu kwa mfano wake. Inafikirisha sanaPole sana ndugu, maadam umeamua kuanza safari ya kumjua Mungu atakusaidia uendelee kumwelewa zaidi. Safari ndio umeianza lakini weka akili yako wazi kupokea michango ya wadau upate uelewa zaidi.
1. Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake. (Udongo jumlisha pumzi ya Mungu).
2. Mungu aliumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo.
Inawezekana vipi kisicho na uhai kiumbe vilivyo na uhai.
Mungu akasema......na ikawa. Kabla ya kusema nini kinatangulia. Ni kuwaza au mawazo. Kwahiyo mawazo (niite consciuosness kwa kizungu cha Uingereza) ndiyo kiini cha uhai. Leo wewe ukipoteza consciousness umekwisha.
Endelea kujifunza ndugu. Mungu yu hai na anaishi milele.
Hata malaika na Majini yanazaliana kama Wewe na Mimi Mkuu ingawa Wewe huyaoni kwa Macho.Fikiria hivi! Kilichasababisha wewe ukawepo ni wazazi wako. Na wao wazazi wao, ukienda hufiki mwisho ila utagundua kuna kisababishi cha mwanzo. (First cause) Hicho hakina ihai? Huenda ni uhai usiokuwa na mwanzo au mwisho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya shule ulikuwa unajua kuna herufi A?Kitabu kilichoandikwa na Binadamu au Mungu!
Na je kabla ya Kitabu hicho ulikuwa unajua kuna Mungu? Maana kitabu hivyo unavyoviamini ni vya Juzi tu. Maana Wengine mmejua kwamba Kulikuwa na Gharika Baada ya Kitabu kuja Kwenu. Hata Babu yako Inawezekana hajui kama Kulikuwa na Magharika
Ndio maana nakwambia imani ni kitu binafsi hakitegemei Mungu maana hata wasio amini Mungu wana imani na zinafanya kazi.Rudi kwenye post yangu hapo juu nilipoelekeza imani inavyofanya kazi.
Kwa imani yakoMungu hafanani na kitu chochote alafu hapo Mungu kaumba mtu kwa mfano wake. Inafikirisha sana
Hayo yote nimeelezea kwenye post yangu ya imani. Rudi ukasome vizuriNdio maana nakwambia imani ni kitu binafsi hakitegemei Mungu maana hata wasio amini Mungu wana imani na zinafanya kazi.