Mungu awalinde madaktari wote

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
MADAKTARI (DOCTORS);

1. Ili uwe kama wao lazima usome miaka mingi sana darasani, kushinda mhandisi, rubani, mwanasheria n.k.

2. Kazi yao ni kuokoa maisha ya kila mmoja wetu baada ya kila kitu kushindikana, hawaogopi miili ya waliokufa, hawatishwi na miili iliyoharibika na hawana wasiwasi na majeraha makubwa yanayotisha.

3. Madaktari hufanya kazi kwa dharura bila kupumzika, daktari anaweza kufika kwake akapigiwa simu “treni imepata ajali” watu mia tano wamefariki, hhurudi kazini kuokoa maisha yetu bila kujali kuwa hakulala saa 24 zilizopita.

4. Na baada ya kazi ngumu sana, na kukosa usingizi kwa siku kadhaa – akizidiwa hulala popote pale na hulala usingizi, hata waliookolewa maisha yao huwa vitandani – kitanda chake kipo pale usingizi mkuu utakapomfika.

5. Na, bado kusoma kote, kufanya kazi usiku na mchana wakati wote wa mwaka, kukosa usingizi na kulala popote – Daktari analipwa fedha zisizolingana na kazi yake. Inambidi ajitafutie hospitali 2 au 3 za ziada kufanya kazi kwa muda ambao angelipumzika ili ajiongezee kipato na aishi maisha ya hadhi yake.

Leo natunuku UKUTA huu kwa ajili ya madaktari wote!
Mungu awabariki sana.
 
Wale majeruhi wa ajali ya moto au za barabarani ambao ww hata kuwaangalia ni kazi wao ndo kwaanza wana washika kabisa kuwahudumia....

Wajawazito wa hali zote bila madakatari hakuna kitu

Magonjwa kama saratani, HIV,na mengine kama hayo wao lazima waku face na kukufanyia uchunguzi na kukupa matibabu..

Mara zingine hata hamu ya kula inatoweka kabisa. Kweli hiyo ni kazi ya moyo na wito.. Nadhani pia kwa Mungu watapatiwa Cr ya ziada.
 
Tena mtu asikudanganye ukasomea udaktari, wewe unahangaika miaka mitano kusoma na mmoja wa intern mwenzako wa fani zingine kama human resources au sheria au biashara anakuwa kaisha Maliza masters na mkija kazini unakuta ana mshahara mkubwa na ni boss wako.
 
umegusa secta nyeti nipo kcmc apa daa watu wanamagonjwa jaman madocta wanafanya kazi hii kazi ni wito
Unakuta mtu ana Liver Cirrhosis, Heart Failure, Renal failure, HIV Stage IV n.k

Watu wanateseka sana.....
 
Tena mtu asikudanganye ukasomea udaktari, wewe unahangaika miaka mitano kusoma na mmoja wa intern mwenzako wa fani zingine kama human resources au sheria au biashara anakuwa kaisha Maliza masters na mkija kazini unakuta ana mshahara mkubwa na ni boss wako.
ww u docta ni wito ww Acha use....... hawa ni watu muhim sana
 
Mpe dk heshima yake ht maandiko yanasema
 
Attachments

  • 1460274054607.jpg
    1460274054607.jpg
    72.5 KB · Views: 34
  • 1460274161795.jpg
    1460274161795.jpg
    60.8 KB · Views: 33
Tena mtu asikudanganye ukasomea udaktari, wewe unahangaika miaka mitano kusoma na mmoja wa intern mwenzako wa fani zingine kama human resources au sheria au biashara anakuwa kaisha Maliza masters na mkija kazini unakuta ana mshahara mkubwa na ni boss wako.
Mungu aliumba viumbe tofauti tofauti na kila mtu na wito na karama zake..kila mtu akisomea hicho unachosema dunia ingekuwaje...
Ndio maana kuna majani..kuna miti..maua..matunda.kuku..tembo..simba...binadamu
Tungeumbwa wote tembo ingekuwaje...
Jua kila kiumbe dunian kina thaman na umuhimu so usione kimoja bora kuliko kingine
 
Mnawarubuni kwa Maneno matamu huku ukweli unabaki vilevile kuwa nchi yetu haiheshimu mishahara ya madaktari
 
Ni kazi ya wito kuwa Dk, na kama ni wito wako hata kulala kazini huoni shida, raha unayoipata ni kuwa umeokoa maisha.
 
Tunategemeana bana wote tunastahili kuheshimiana. ....Ikiwa mwili wote utakuwa jicho kusikia ku wapi?.....
 
Mkuu wahudumu wa afya ni muhimu lakini dunia unaiona iko hvi ni kwa ajili ya engineers sisi tunamfanya docta ajisikie fahari kumuhudumia mteja kwa advanced technology, Doctor anaweza kufeli kumhudumia mteja na madhara ya kifo yasimsumbue ila engineers muda wote ni kuwa attention system ikifeli ni hatari mfano nuclear reactors, system za bank
 
Back
Top Bottom