kimsingi kuna mashaka juu ya uwepo wa mungu!
hiki unachokishangilia kweli wewe unadhani ni uwepo wa mungu? mungu gani huyo uliye naye ambaye unashangilia eti mwenzako kafukuzwa kazi? na haya ndiyo watu wanashuhudia makanisani eti mungu kanitendea muujiza.
leo hii ukibishana na mtu kuhusu mambo ya imani anasema subiri na katika kusema subiri mungu atajidhihirisha anategemea upate matatizo na ndio uje kutambua uwepo wa mungu.
tunaamini mungu ni the creator of everything sasa nguvu ya creation umewahi kuiona wapi? yaani kiumbe aliyetengeneza ulimwengu huu au viumbe vyote leo hii anakuja kumfukuzisha kazi bosi wako anayekuchukia bila wewe kujua sababu? huko ni kusema kiumbe huyo amefilisika. lakini wewe unayeshangilia kufukuzwa kwa mwenzako je atakuacha huru?
ninachotaka kukueleza kuna uwezekano wa imani kutokutoka unakokudhani na kule imani zinakotoka wanatake advantage ya matukio au kuchochea baadhi ya matukio alafu unaletewa mawazo mungu kafanya kazi. kwa logic ya kawaida mungu hawezi kufanya hilo unalolishangilia ila kitu kinaweza kujifanya mungu kikafanya upumbavu ukashangilia na chenyewe kikabaki kinakucheka. kama wengine wanavyodanganywa kuwa ukichinja albino utapata mali basi wanachinja na kinachowadanganya kinabaki kuwacheka.
Elli