Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,201
- 99,936
Inapokuja suala la imani hegeuka na kuwa kitu kigumu sana! Niliajiriwa kwenye International NGO, ilionekana nafasi nzuri kwa baadhi ya watu lakini kwangu mimi ilikua ni post yenye changamoto sana.
Baada ya kupata post ile ghafla sana mambo yaligeuka, Boss wangu ambaye alikua si Mtanzania alianza kunichukia sana sana. Ikafika kipindi hata kwenda kazini kwangu ikawa kama vile nakwenda kituo cha Polisi. Yaani ikifika saa kumi na moja asubuhi nakosa usingizi kabisa. Kwa ukweli hakua na sababu yoyote ya msingi ya kunichukia.
Nilianza kusali na kumuomba MUNGU sana kwamba kama kweli kuna jambo baya nimemtendea huyu Mama basi MUNGU anisamehe lakini pia niliomba sana AMANI na huyu Boss wangu, niliomba upatanisho, sikutaka kuweka visasi.
Nilijitahidi sana kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi, baada ya miaka mitatu ya maumivu makali hatimae Boss wangu huyu alipandishwa cheo na kupelekwa Marekani yalipo Makao Makuu ya NGO.
Mwaka mmoja baadae aliachishwa kazi ghafla sana, tena akiwa kwenye Mkutano tu, lakini kitu cha kushangza siku moja nikiwa nyumbani nilipokea text kwenye namba yangu ya Whatsapp, sikuifahamu ile namba kwakua ni ya Marekani na kwenye Profile ilionekana picha ya Binti, nikaijibu tu lakini sikuhangaika kujua ni nani. Week mbili baadae nilipokea text nyingine kwenye namba ile ile ikinisalimia! Kucheki kwenye Profile Photo nikakuta ni yule Mama.
Nilimjibu na nikamwambia nimefurahi kusikia tena toka kwake. Kilichofuata baada ya hapo aliniomba kama nitasikia Opportunity yoyote hapa Tanzania nimshikirikishe! Nikamjibu nikamwambia sawa!
Nimeandika hivi kuonyesha kuwa ile miaka ya maumivu yote nimefurahi imekwisha, niliomba AMANI na hakika tumepatana! Moja ya mistari kwenye text yake aliandika hivi Get Ride of Bitterness!! Nikajua amejua ukweli kuwa sikuwahi kumtendea baya! Tafuteni kuwa na AMANI na Watu wote......Waebrania 12:14
SIKUOMBA AFUKUZWE NA SIKUFURAHISHWA NA KITENDO CHA KUFUKUZWA NILIOMBA NIPATE KUWA ANA AMANI NAYE. NA SASA TUNAONGEA NA SASA ANAWEZA KUNIOMBA NIMTAFUTIE FURSA HAPA BONGO. NAAMINI NIMEELEWEKA.