Mungu amjalie moyo wa subira Rais Samia kwa maumivu makubwa aliyopata kutokana na maafa ya Hanang

Ukute nae kuna watoto wanamuita Baba nyumbani kwake,Wazazi wengine walipoteza sperms zao tu
Baada ya kusoma hii post nimejiwa na mawazo hivi huyu Lucas angekuwa ni sperms zangu ningejisikiaje na hii aibu?
Nimeishia kumwonea huruma mzee mwenzangu aliyezimwaga na kupata huu mzigo!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mwenye picha ya Lucas Mwashambwa, anitumie!
Huyu hapa
tapatalk_1570946898001.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Rais wetu mpendwa ameumia na kuumizwa sana na maafa yaliyotokea mkoani Manyara wilaya ya Hanang mji wa kateshi yaliyo chukua roho na maisha ya watanzania wenzetu 76. Nimemtizama kwa umakini na utulivu mkubwa sana tangia kuwasili kwake eneo la tukio.

ambapo alioonyeshwa eneo na madhara yaliyo tokea na kusimuliwa na kupewa picha ya eneo lililokuwa na makazi na kubakia kama uwanja, wakati alipozungushwa angani kwa helkopta kujionea hali halisi mpaka muda ule alipotoa hotuba yake kwa wananchi na Taifa zima kwa ujumla wake.

Kiukweli moyo wa Rais samia kama mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu, kiongozi wa serikali,mama wa watoto,bibi wa wajukuu na faraja ya Taifa ameumia sana tena sana mama yetu. Ukimtizama usoni unaona namna ambavyo moyo wa mama yetu umebubujikwa na machozi mengi ya uchungu na maumivu makali sana.

Ni ujasiri tu wa kiuongozi anaopaswa kuwa nao kiongozi ambapo yeye anatakiwa kuwa msitari wa mbele kutoa faraja kwa wahanga, lakini katika hali halisi mama yetu ameumia na kuhuzunishwa sana mpaka nimemuonea huruma sana Rais wetu.

Ndio maana mmeona Rais wetu namna alivyokuwa akizungumza kwa unyonge na hisia kali sana,ndio maana mnaona alitoa hotuba fupi ambayo kila mtu aliyekuwa akifuatilia alijikuta akiguswa na akiingiwa na simanzi na huzuni moyoni ya kuondokewa na watanzania wenzetu.

Ndio maana hata macho yake, paji la uso wake na muonekano wake mzima usoni ulikuwa umeelemewa na maumivu na machozi katika moyo wake japo usingeweza kuyaona yakitiririka katika macho ya kawaida kwa kuwa yeye ni kiongozi ambaye anatakiwa kuwafuta machozi na kuwatia moyo wahanga wanaoendelea kububujikwa na machozi ya kupoteza wapendwa wao.

Watanzania wote kwa pamoja na umoja wetu sote tumeumia na kuumizwa sana na kile kilichotokea kule Hanang. Ndio maana tumeunganika kama Taifa kuelekeza maombi, sara na dua zetu kwa watu wa Hanang. Ndio maana tumeona michango ikitoka kila pembe ya Taifa letu kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania wenzetu.

Kwa upekee kabisa namuomba Mungu mwingi wa Rehema na Fadhila amtie nguvu na kumpa moyo wa subira Rais wetu wakati huu ambapo Taifa limeondokewa na watanzania wenzetu, natambua kwanini msiba huu umekuwa mzito moyoni mwa Rais wetu.

Ni mzito kwa kuwa Rais samia ndiye mfariji wa watanzania wote na ndiye mwenye dhamana na maisha ya watanzania, ambaye ana jukumu la kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa salama muda wote, Lakini kwa kuwa hili lilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu na serikali yetu.

Ndio maana Rais wetu ametusihi tumuachie Mungu na kumshukuru kwa yote na kuendelea kuchukua tahadhali wakati huu ambao mvua zinaendelea kunyesha, lakini pia kumuomba Mungu sote kama Taifa ili Mungu atupatie mvua zenye baraka na neema kwa Taifa.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Hivi Maumivi yanapimwa kwa kioimo gani? Halafu Tena ya mtu kwingine ambaye Wala hajafiwa hata na Mendez wa nyumbani kwake.

Wanaombusu wako zao huko nchi jirani ya Zanzibar.
 
Hivi Maumivi yanapimwa kwa kioimo gani? Halafu Tena ya mtu kwingine ambaye Wala hajafiwa hata na Mendez wa nyumbani kwake.

Wanaombusu wako zao huko nchi jirani ya Zanzibar.
Rais ndiye kiongozi namba moja mwenye dhamana na maisha ya watanzania.kwa hiyo ni kiongozi anayekuwa na uchungu mkubwa sana moyoni mwake inapotokea kuna mtanzania amepoteza maisha kwa majanga au ajali au chochote kile
 
Back
Top Bottom