Mungu ametuacha watanzania?

bemg

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
2,799
642
Ni jambo la kushukuru Mungu na lakupendeza kuona jamii inaishi kwa umoja na kwa upendo.Lakini kwa hali sasa inavyoeonekana katika nchi yetu imeshakuwa kama tunaelekea kupoteza umoja wetu na upendo wetu.Matukio yanayoendelea kutokea katika jamii yetu inaonyesha dhaihiri kabisa Mungu ametusahau watanzania na pengine hasikii hata maombi tunayofanya watanzania juu ya kulinda umoja na amani tuliyo nayo.Miaka ya 1990s ilikuwa ni vigumu kusikia katika jamii mtu fulani kasukiwa mipango ya kupotezea furaha kwa kuharibu mali zake au kusababisha kifo kwa sababu tu ya dini, koo,kabila au rangi ya mtu.Majanga ya kutisha ya meliandama taifa letu,umaskini,ukame,njaa,ajali,mauaji,ufisadi,magonjwa,n.k na haya yote ni dalili ya kwamba Muumba wetu ametuacha tuzidi kuumizana sisi kwa sisi na huku wachache tu ndo wakiendelea kufurahia kwa yale mabaya wanayowatendea watanzania.
Ni ombi langu kwa wana JF na kwa kila mtanzania kwa dini yake,kabila lake na hali yake ya umaskini au utajiri tumlilie Mungu aweze kuturudia na kuiponya nchi yetu.Tumechoka kuendelea kuishi kwa huzuni na mashaka kila mara katika jamii yetu.Atuponye na mabaya yote ili tuendelee kuishi kwa umoja ,kwa amani,kwa kuvumiliana,kwa upendo na pia bila ufisadi wa mali ya umma.

Mungu turehemu na usituache tuzidi kuteseka na kuteswa na watanzania wenzetu hapa duniani.
 
Miaka ya 1990's vyombo vya habari vilikuwa vichache kwahiyo tulikuwa hatupati habari nyingi jinsi mambo yanavyoendelea kila siku. Katika Biblia kitabu cha Mhubiri kinasema kwamba hakuna jambo jipya chini ya jua. Kama ni maovu yapo mengi tu tangu zamani. Naamini Mungu hajatuacha maana imeandikwa pia kwenye kitabu cha Isaya Mungu anasema mwanamke anaweza kumsahau mtoto aliyemzaa ila siyo yeye. Ametuchora katika vitanga vya mikono yake.
 
Lakini kwanini basi kipindi hiki tunazidi kupata huzuni katika taifa kwa matukio mbalimbali yanayotokea na yanazidi kutokea kila kukicha.Mimi nadhani imefika mahali tubadili njia zetu kuanzia kwa watawala wetu wa nchi na kwenye dini.
 
Back
Top Bottom