wadau kwa nia ya dhati niliweka bango la kuhitaji mchumba hapa jf na kweli nilipata,kwa muda mfupi tu baada ya kukutana nilibaini hatuwezi kuishi,na kwa kuwa lengo ilikuwa nipate mke basi nikaamua kujinasua mapema ili nisimpotezee muda wake na mimi nisipoteze lengo langu la kupata mke wa ndoa.
Siku ya kwanza na dakika ya kwanza kukutana nae aliniomba nimtoe kwa lunch pamoja na rafiki yake,nilikubali bila kinyongo lakini ktk notebook yangu nikatia x kwa kitendo kile,wakati tunakula mimi nikiwa sivuti hata sigara mwenzangu akaitisha Tusker nikatia x nyingine.
Wakati tunaendelea kupata mara akapita chinga na viatu akaitisha na wakati tunaagana nikapewa ombi nimnunulie simu yenye fast internet,nilichoka mwili na roho Nilivotoka hapo nikajisemea mwenye kwamba huyu si tu kwamba hatoshi kuwa mke bali hafai hata kupajua nyumbani kwangu.namshukuru mungu nilifanikiwa kujinasua na japo bado sijapata mke nimelazimika kujipa muda zaidi na tafakuri mpya maana hali ile ilinitia hofu na kunichanganya hasa ikizingatiwa hitaji langu ni mke wa maisha na sio gonga niondoke.
Karibuni wadau tusaidiane mawazo.
Preta kwani kuna ubaya gani mwanamke kuomba atolewe lunch yeye na rafiki yake?, Je kuna ubaya gani mwanamke akiomba anywe Tusker bariiiiidi moja tu? Kuna ubaya gani ukimnunulia mwanamke viatu vya WAMACHINGA?ooooh no....hebu nitafute tuongee vizuri....huyo mwanamke hakufai.....ni gubegube......
na kwa nini akufanyie hivyo....hustahili kabisa.......
Ha ha ha ha unatafuta mke kwa ininternet wewe umechelewa Kabisa aisee. Ndo ukome umeshindwa kutongoza wale unaokutana nao mpaka utafute hapa? Pole wewe umefundishwa vizuri sana.
Halafu acha ubahiri wewe Lu nch tu unapiga Kelele ukiambia Mark II itakuwaje?