Mume wangu kazaa nje mtoto wa kiume

Mume wangu kazaa nje mtoto wa kiume

Hapo haujashauri, bali umebomoa na kuchonganisha.
Tunashauriwa mambo ya unyumba tushauri kwa kadri, tukae kati kupatanisha.
Kwanza mleta mada haujamhoji ni kwa nini tokea '02 kaishi na mwanaume ki-kimada?
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria za ndoa za mwaka '71,bila ndoa ya aina yoyote hasa upande wa kinamama, mwanamke hauna haki.
Labda ukute zinaingizwa blah blah za ustawi wa jamii ama siasa.
Lakini pale hakuna haki, bila kujali umeishi naye miaka mingapi.
Hilo la kwanza.
La pili, unavyoshauri akurupuke kuachika bila kushauri akaanze upya na nini na watoto zake, wakati muda wake mwingi kaupoteza kwenye ukimada ni kumuumiza zaidi na si kumjenga.
Hivi ni kwanini binadamu huwa tunadanganyika kuanza maisha kihunihuni kwanza, kabla ya kufikia maamuzi sahihi ya kufunga ndoa?
Huwa tuatafuta nini hasa cha maana kusubiri ama kusubirishwa?
Mwanamke unafanywa kama test tube ya kupimia mkojo, unakenua meno na kuridhika ukiamini umepata!
Cha kushauri hapo ni kwamba, akae chini na huyo kimada wake wapangiane na kukubaliana na maamuzi ya "mjanja" aliye mpumbaza miaka nenda rudi kama karai la zege, kwa kuwa yeye pamoja na ukristu wake hajafungwa na ndoa za mitaala kwa maana hajawahi kufunga ndoa ya kikristu.
Alishajitenga kwa matendo yake bila ya kutengwa.
Aendelee na maisha ya kuungaunga ili aweze kulea wanaye pamoja na huyo kimada mzazi mwenziye, kwa kuwa aina hiyo ya maisha tayari alishakubaliana nayo tangu mwanzo.
Tunapokuja na ushauri wa kumpotosha, tunakosea sana. Maana mtu mwingine waweza kuta ananyanyasika na kipigo na mambo kadhaa wa kadha, lakini kichwani mwake anatafsiri kuwa matendo hayo ndio upendo wenyewe.
Vurugu za unyumba zitokeapo, chukua jembe ukalime. Vinginevyo ukiingilia, kesho wewe ndiye utaonekana mbaya na wao kuendelea na maisha yao waliyoyazoea.
Sasa ndugu mbona na wewe ushauri wako ni wa kuumiza tu?
ulikuwa na haja gani ya kumkosoa huyo uliyemkosoa?
Mleta hoja kaishakosea, maneno yako haya hayamsaidii kitu
bali kumuongezea huzuni,weka ushauri wa kumsaidia kuvuka
maana kama ni kuumia kaisha umia weka ushauri wako ili avuke.
 
Duh, nimesoma mitandaoni kuna binti ana mtoto wa kiume katolewa utambulisho sijui mahali weekend hii imeisha. Wadaku wanasema ni mwanaume ana mke. Natumaini sio wewe.. nimejisemea tu. Pole sali ufate muongozo wa Mungu, maana magonjwa nayo tabu yakimuingia mtu. Lingine huyo mumeo maneno aliyokuambia ni mabaya sana kwa kweli, kama mlitoka mbali na mipango yenu. Muache aende kuisoma namba huko.. ila wewe siku 3 na yule 4 duh!!! Tatizo lingine haukwenda kanisani kufunga ndoa, huyo ataweza kupelekwa. Hili ni funzo kwa wasichana msijisahau kwa kunogewa na kuwaamini wanaume.. wanaume mmmmmh

Kimila ni ndoa ila inauma, anza kujipanga na kuwa unasevu pesa na kujiendeleza mwenyewe upae. Usikae kumtegemea yeye kama zamani kivyovyote.
 
Sasa ndugu mbona na wewe ushauri wako ni wa kuumiza tu?
ulikuwa na haja gani ya kumkosoa huyo uliyemkosoa?
Mleta hoja kaishakosea, maneno yako haya hayamsaidii kitu
bali kumuongezea huzuni,weka ushauri wa kumsaidia kuvuka
maana kama ni kuumia kaisha umia weka ushauri wako ili avuke.
Dah! Niivyo?
Lakini lazima uelewe mfumo na tafsiri sahihi ya maisha yetu sisi binadamu.
Mfumo wa maisha ya binadamu unaongozwa na "mwanzo".
Ukikosea mwanzo, saazingine hata ukishauriwa huwa ni ngumu sana kurejerea nyuma.
Kwa mfano utotoni usipopata malezi mema, usisomeshwe, waweza kusumbuka maisha yako yote, hata kama ungelipata ushauri nasaha wa namna gani.
Kwa mfano huo ni kwamba, uanzapo maisha, hasa haya ya kiunyumba, usipopata ama kufuata mwanzo mzuri,waweza kupata majuto maisha yako yote.
Sisi tunashauri mazingira aliyomo mtu. Hatuwezi kushauri nje ya wigo.
Kwa mfano kama ninatoa ushauri kwa mfungwa, siwezi kumshauri atoroke, bali nitamshauri nidhamu na usafi ndani ya jela na kumtia moyo wa uvumilivu kumalizia kifungo nk nk.
Sasa na suala la huyo mama, yatupasa tumshauri kuhangaika na kurekebisha mazingira aliyopo na si kuondoka.
Kwa kuwa mwanzo aliukosea yeye mwenyewe kwa kutokujua ama kwa mapenzi yake.
Yeye aelewane tu na huyo mzazi mwenziye na si kuondoka, mwisho watafikia maridhiano.
Sisi watu wa mila tunaghadhabikia sana mfumo wa kilaana unaopendwa sana na vijana siku hizi.
Mtindo wa "kuonjana". Huu ni ukiukwaji mkubwa sana wa maadili kwa watu waliostaarabika.
Matokeo yake ni majuto hasa kwa watoto wa kike.
Anaonjwa kulala naye, anaonjwa kuishi maye, anaonjwa kuzaa naye.
Tabia hiyo inaleta malalamiko mengi sana na tunajaribu kukemea kadri tuwezavyo.
Ndugu yangu, niwie radhi kwa kutumia lugha kavu igawa pointi ni ndogo sana. Tena ni moja tu, kwamba asiondoke kwa mzazi mwenziye alipo, bali akomae na kuweka mazingira rafiki ya kumalizia maisha yake.
Kwa kuwa mwanzo aliukosea yeye mwenyewe.
 
Tena ni moja tu, kwamba asiondoke kwa mzazi mwenziye alipo, bali akomae na kuweka mazingira rafiki ya kumalizia maisha yake.
Kwa kuwa mwanzo aliukosea yeye mwenyewe.
Ungeweka ushauri huu toka mwanzo wala
usingeona nitie neno.

Kuna ushauri na kuna hukumu,ukienda gerezani
kumwambia mfungwa kuwa ulikosea ndo maana
umefungwa hapa unaongeza hukumu juu ya ile ya hakimu
maana tayari kosa lake limeishampeleka jera na hiyo haimsaidii.
Ila ukimshauri kuvumilia na ukimtia moyo
kwamba wapo na wengine walifungwa kama wewe lakini
baada ya kutoka walijifunza kuwajibika na hivyo
kwa sasa wanaendelea vizuri atajipa moyo
na kumalizia kifungo chake kwa matumaini.
 
Fanya vile moyo wako unataka

Meanwhile fanya yako..... jikite kupambana kiuchumi huku ukitafuta furaha ya moyo wako

Fanya kama haexist...hata akitaka kuhamia huko akatafute watoto vizuri mwache aende
Yaan amfanye baba watoto wake kama haexist????
Dah... Kuwa na huruma.
 
Japo mtoto wa kike ndiye atakayekuja kuwasaidia baadae. Wa kiume tunazalia wenzetu.

Hilo la kulala zamu hapana. Akitaka ahamie huko moja Kwa moja.

Anza maisha kama mjane sasa. Lia sana na Mungu wako. Japo utajibiwa baada hata ya muda mrefu. Usiache kuomba.

Jitahidi sana somesha wanao.

Usiogope. Yana mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maamuzi ni yako. Acha kusononeka, nyanyuka jikung'ute na uendelee na maisha, watoto watakuwa faraja kwako.
Masononeko hayatasaidia na bahati mbaya huna ndoa halali..akili kichwani mwako.
 
Tatizo langu linafanana mumeo, ingawa naona mumeo ana afadhali...[emoji14] [emoji14]
Hivyo naomba niwe msomaji tu, pengine nitapata lakujifunza
Real? Pole.
Wana jf nimeolewa na mume wangu kwa ndoa ya kitamaduni toka mwaka 2002 na tumejaliwa watoto wawili wote wakike (kwa sasa ni wakubwa tu) Kila nikimuomba mume wangu tuongeze baby wa mwisho ananikatalia anasema hao wawili wanatosha wakati kabla hatujazaa tulipatana tuwe na watoto watatu.

Sasa jana kanikalisha chini akaniambia mama mimi nimezaa nje ya ndoa na nimebahatika kupata mtoto wa kiume ambae nilikua namtaka kila siku hivyo basi huyo mwanamke niliezaa nae lazima nimtolee mahali ili mtoto achukue jina langu la mwisho.

Mbaya zaidi mume wangu kasema inabidi nizoee kuwa sasa yeye ana wake wawili na itabidi atufanyie zamu siku tatu kwangu siku zilizobaki kwa mke mdogo.

Pia aliniambia ukweli kuwa alikua anaogopa kuzaa na mimi tena asije kupata mtoto mwingine wa tatu wa kike.

Sasa wana jf nifanyeje nikubali kuwa na mke kwanza au niendelee na maisha yangu? Maana sisi ni wakristo haturuhusiwi wake wengi.

Je huyu mtoto wa kiume wa mume wangu si ndio atakuwa mrithi mkuu wa mali tulizochuma wote?

Naumia sana kwa nini sikuweza kupata mtoto wa kiume maana huyu mtoto wa nje ni copyright na mume wangu pia kapewa jina la baba mkwe yani naumia naona kama sina changu istoshe mtoto kashatambulishwa mpaka ukweni

Kwa nini wanaume msipokuwa na mtoto wa kiume hamridhiki mpaka mkamtafute kwa mwanamke mwingine? Kwani ukiwa na watoto wakike tu unapungukiwa nini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mwanamke una busara sana, labda kwa vile umri wako umeenda. Tulia na mmeo linda heshima ya ndoa
fatu2010
 
Wewe ndo kichaa kweli. Unajikanyaga ww mwenyewe.
Umesema umefynga ndoa ya kimila. Now unaseama ww ni mkristo hamruhusiwi wake wengi.
Sasa ndoa yenyew uliyo funga haipo recognized kwenye serikali wala dini. Na sijui kanisa gani unalo sali. Nadhani hisali ila unahudhuria kanisani.
Sina cha kukushauri by the way.
Tena sasa mwenzie ndio anaenda kuolewa ndoa ya kikristo....yeye si aliridhika na ya kimila
 
Hapo haujashauri, bali umebomoa na kuchonganisha.
Tunashauriwa mambo ya unyumba tushauri kwa kadri, tukae kati kupatanisha.
Kwanza mleta mada haujamhoji ni kwa nini tokea '02 kaishi na mwanaume ki-kimada?
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria za ndoa za mwaka '71,bila ndoa ya aina yoyote hasa upande wa kinamama, mwanamke hauna haki.
Labda ukute zinaingizwa blah blah za ustawi wa jamii ama siasa.
Lakini pale hakuna haki, bila kujali umeishi naye miaka mingapi.
Hilo la kwanza.
La pili, unavyoshauri akurupuke kuachika bila kushauri akaanze upya na nini na watoto zake, wakati muda wake mwingi kaupoteza kwenye ukimada ni kumuumiza zaidi na si kumjenga.
Hivi ni kwanini binadamu huwa tunadanganyika kuanza maisha kihunihuni kwanza, kabla ya kufikia maamuzi sahihi ya kufunga ndoa?
Huwa tuatafuta nini hasa cha maana kusubiri ama kusubirishwa?
Mwanamke unafanywa kama test tube ya kupimia mkojo, unakenua meno na kuridhika ukiamini umepata!
Cha kushauri hapo ni kwamba, akae chini na huyo kimada wake wapangiane na kukubaliana na maamuzi ya "mjanja" aliye mpumbaza miaka nenda rudi kama karai la zege, kwa kuwa yeye pamoja na ukristu wake hajafungwa na ndoa za mitaala kwa maana hajawahi kufunga ndoa ya kikristu.
Alishajitenga kwa matendo yake bila ya kutengwa.
Aendelee na maisha ya kuungaunga ili aweze kulea wanaye pamoja na huyo kimada mzazi mwenziye, kwa kuwa aina hiyo ya maisha tayari alishakubaliana nayo tangu mwanzo.
Tunapokuja na ushauri wa kumpotosha, tunakosea sana. Maana mtu mwingine waweza kuta ananyanyasika na kipigo na mambo kadhaa wa kadha, lakini kichwani mwake anatafsiri kuwa matendo hayo ndio upendo wenyewe.
Vurugu za unyumba zitokeapo, chukua jembe ukalime. Vinginevyo ukiingilia, kesho wewe ndiye utaonekana mbaya na wao kuendelea na maisha yao waliyoyazoea.
Ukweli mtupu..
 
Namfaham Huyo mmeo vizuri kiufupi nawafahamu nyie vizuri kwa tarifa Sio Huyo tuu anao wengi na Huyo ulieambiwa amezaa nae mtoto wa kike ana miaka 6 Huyo ni wa pili wa kiume Huyo ulieambiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana, nakuelewa sana ila vuta subra hakuna mwanzo usokua na mwisho,kua na watoto wakiume sio tija sana ila wako wengine wenye tabia hizi,hata mzazi wangu alikua anasema mtoto wa kike Bidhaa mbovu ilikua ukiniuma sanaa sababu tulizaliwa wakike wa4 wakiume wa3 ikawa shule wakiume ndio lazima sisi wa kike wala mda alikua hana,ila Mama akatuambia silaha yenu ya maisha ni kusoma,leo hii hao wanaume walokua wanapewa maisha ya na shule za hali ya juu Baba akitaka kitu wanasema Dad tuna majukumu wakati sisi Bidhaa mbovu ndio tunamtizama,ila sikuweza kuka na dukuduku rohoni i had to tell him,ivi Dad ulifikiria nini mpaka kutuita Bidhaa mbovu?
sasa usife moyo kisa uko na watoto wa kike nao pia ni watoto na ashukuru mwenyezi hata hao wakike anao kuna wengine hata kuitwa baba wa mtoto wa kike anataka, chamsingi focus na Elimu yao,na kuondoka au kuachana sio sawa hao watoto bado wanamuhitaji mzazi wao,ila mwisho wa siku maamuzi ni yako lakini fikiria sanaa tena sanaa bala huja chukua maamuzi magumu usije ukajutia..
 
Back
Top Bottom