Mume wangu kazaa nje mtoto wa kiume

Mume wangu kazaa nje mtoto wa kiume

The Woman

Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
6
Reaction score
19
Wana JF,

Nimeolewa na mume wangu kwa ndoa ya kitamaduni toka mwaka 2002 na tumejaliwa watoto wawili wote wa kike (kwa sasa ni wakubwa tu) kila nikimuomba mume wangu tuongeze baby wa mwisho ananikatalia anasema hao wawili wanatosha wakati kabla hatujazaa tulipatana tuwe na watoto watatu.

Sasa jana kanikalisha chini akaniambia mama mimi nimezaa nje ya ndoa na nimebahatika kupata mtoto wa kiume ambae nilikua namtaka kila siku hivyo basi huyo mwanamke niliezaa nae lazima nimtolee mahari ili mtoto achukue jina langu la mwisho.

Mbaya zaidi mume wangu kasema inabidi nizoee kuwa sasa yeye ana wake wawili na itabidi atufanyie zamu siku tatu kwangu siku zilizobaki kwa mke mdogo.

Pia aliniambia ukweli kuwa alikua anaogopa kuzaa na mimi tena asije kupata mtoto mwingine wa tatu wa kike.

Sasa wana JF nifanyeje nikubali kuwa na mke kwanza au niendelee na maisha yangu? Maana sisi ni wakristo haturuhusiwi wake wengi.

Je huyu mtoto wa kiume wa mume wangu si ndio atakuwa mrithi mkuu wa mali tulizochuma wote?

Naumia sana kwanini sikuweza kupata mtoto wa kiume maana huyu mtoto wa nje ni copyright na mume wangu pia kapewa jina la baba mkwe yani naumia naona kama sina changu isitoshe mtoto kashatambulishwa mpaka ukweni.

Kwanini wanaume msipokuwa na mtoto wa kiume hamridhiki mpaka mkamtafute kwa mwanamke mwingine? Kwani ukiwa na watoto wa kike tu unapungukiwa nini?
 
Duu pole mpendwa tuliza kwanza kichwa mpe Mungu shida zako atakupatia jibu, aliye kupatia hao watoto wakike ndiye aliye mpa huyo mtoto wakiume mwambie Mungu atakupa jibu, ndugu wa kiume sio wakuaminiwa sana kumwambia ndugu yao oa mwingine hawashindwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndo Unajikanyaga ww mwenyewe.
Umesema umefynga ndoa ya kimila. Now unaseama ww ni mkristo hamruhusiwi wake wengi.
Sasa ndoa yenyew uliyo funga haipo recognized kwenye serikali wala dini. Na sijui kanisa gani unalo sali. Nadhani hisali ila unahudhuria kanisani.
Sina cha kukushauri by the way.
 
Pole sana usitoke kwa nyumba yako kaa hapo hapo. Usiwe na kisirani kuwa karibu sana na Mungu. Usifirikie sana Mali haya ni ya dunia yanapita. Watoto wako wa kike Mungu atawapa maradufu. Ombea sana watoto wako wawe na tabia nzuri na wawe mfano kwa jamii. Najua unaumia lakini ukifuatisha haya subiria kipigo cha Mungu, hicho kinaweza kisimwache salama yeye na huyo Kijana wake. Hivi vitu tumeviona sana kwa jamii so usijali Mungu yuko pamoja nawe.
 
Kwa taarifa tu, sisi Me tuna kromosomu XY na nyinyi Ke mna kromosumu XX. Tukigegedana na kama mimba itatungwa, basi sote tunachangia nusu-bin-nusu. Sisi Me tukichangia X basi mtoto atakuwa wa kike na tukichangia Y, mtoto atakuwa wa kiume. Nyinyi Ke mnachangia X tu ambayo mliipata toka kwa Baba au kwa Mama.
Kama utabaki kwenye ndoa yako, basi utaamua mwenyewe ila kumbuka ya kwamba huo mchepuko wa mumeo nao unaweza kua unachepuka pia!, hivyo akiukwaa ukimwi basi mtagawana.
 
duh pole sana mamy! heheheh mie mbiti wala nisingeumia namna hyo yako! yaan ningejipa miez 10 naleta mwarabu!chaa!

km una kazi endlea na kazi yako we mruhusu aoe tu maana huna namna! ...yaan mie only 10 mths nazaa huyo wa kiume!aseee! nimekuhurumia! ngj nilale tu!

kati ya mwarabu/mzungu kbs! au msomali kabisaaa! stupid sana wanaume desgn hyo!
Kwa maelezo inaonyesha historia yako na wanaume ulio date nao kuna tatizo somewhere

Na you always make bad choices/decision.
Kwa style hii utaendelea kujikuta unateseka na adhabu ya makosa ambayo wanakufanyia wengine ila maamuzi yako yanakutumbukiza kwenye balaa jingine
 
Kwa maelezo inaonyesha historia yako na wanaume ulio date nao kuna tatizo somewhere

Na you always make bad choices/decision.
Kwa style hii utaendelea kujikuta unateseka na adhabu ya makosa ambayo wanakufanyia wengine ila maamuzi yako yanakutumbukiza kwenye balaa jingine


ewaaa
 
Kwa maelezo inaonyesha historia yako na wanaume ulio date nao kuna tatizo somewhere

Na you always make bad choices/decision.
Kwa style hii utaendelea kujikuta unateseka na adhabu ya makosa ambayo wanakufanyia wengine ila maamuzi yako yanakutumbukiza kwenye balaa jingine


mkuu we fanya yako !siku ungenifaham ungeishia kunisonya!usikose usngz kwa comment yangu,uwe na aman!
 
Kwa maelezo inaonyesha historia yako na wanaume ulio date nao kuna tatizo somewhere

Na you always make bad choices/decision.
Kwa style hii utaendelea kujikuta unateseka na adhabu ya makosa ambayo wanakufanyia wengine ila maamuzi yako yanakutumbukiza kwenye balaa jingine


mkuu we fanya yako !siku ungenifaham ungeishia kunisonya!usikose usngz kwa comment yangu,uwe na aman!
 
Kama unajiweza nakushauri ukatafute maisha yako achana na huyo mumeo, usijali kuhusu mali yote Mungu anapanga, ila usikubali muwe wanawake wawili ndani hii ina maana mumeo amekudharau na kukudhalisha...
Hapo haujashauri, bali umebomoa na kuchonganisha.
Tunashauriwa mambo ya unyumba tushauri kwa kadri, tukae kati kupatanisha.
Kwanza mleta mada haujamhoji ni kwa nini tokea '02 kaishi na mwanaume ki-kimada?
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria za ndoa za mwaka '71,bila ndoa ya aina yoyote hasa upande wa kinamama, mwanamke hauna haki.
Labda ukute zinaingizwa blah blah za ustawi wa jamii ama siasa.
Lakini pale hakuna haki, bila kujali umeishi naye miaka mingapi.
Hilo la kwanza.
La pili, unavyoshauri akurupuke kuachika bila kushauri akaanze upya na nini na watoto zake, wakati muda wake mwingi kaupoteza kwenye ukimada ni kumuumiza zaidi na si kumjenga.
Hivi ni kwanini binadamu huwa tunadanganyika kuanza maisha kihunihuni kwanza, kabla ya kufikia maamuzi sahihi ya kufunga ndoa?
Huwa tuatafuta nini hasa cha maana kusubiri ama kusubirishwa?
Mwanamke unafanywa kama test tube ya kupimia mkojo, unakenua meno na kuridhika ukiamini umepata!
Cha kushauri hapo ni kwamba, akae chini na huyo kimada wake wapangiane na kukubaliana na maamuzi ya "mjanja" aliye mpumbaza miaka nenda rudi kama karai la zege, kwa kuwa yeye pamoja na ukristu wake hajafungwa na ndoa za mitaala kwa maana hajawahi kufunga ndoa ya kikristu.
Alishajitenga kwa matendo yake bila ya kutengwa.
Aendelee na maisha ya kuungaunga ili aweze kulea wanaye pamoja na huyo kimada mzazi mwenziye, kwa kuwa aina hiyo ya maisha tayari alishakubaliana nayo tangu mwanzo.
Tunapokuja na ushauri wa kumpotosha, tunakosea sana. Maana mtu mwingine waweza kuta ananyanyasika na kipigo na mambo kadhaa wa kadha, lakini kichwani mwake anatafsiri kuwa matendo hayo ndio upendo wenyewe.
Vurugu za unyumba zitokeapo, chukua jembe ukalime. Vinginevyo ukiingilia, kesho wewe ndiye utaonekana mbaya na wao kuendelea na maisha yao waliyoyazoea.
 
Hata mimi imeniuma.Ila sio wanaume wote. Pole sana,Mwombe atimize makubaliano kama mlivyopatana kuzaa watoto watatu akikubali,mwombe Mungu si athumani atakupa na wewe mtoto wa kiume.

Kabla ya kuanza mchakato wa kutafuta mtoto soma makala mbalimbali za jinsi ya kupata mtoto wa kiume,fuata ushauri huo utafanikiwa. Jinsia ya mtoto inatokana na baba na si mama maana baba ndo ana X na Y,wakati mama ana X pekee.

Chunguza mambo haya: Kuna uwezekano mkubwa kwamba hamfanyi maandalizi ya kutosha kabla ya Tendo na hivyo mara nyingi wewe hufiki kileleni. Hii husababisha mbegu zenye X ambazo huwa na kasi kubwa ya kuogelea lakini zinakufa haraka, kushindwa kuogelea kwa sababu ya kukosa maji ya kutosha na hivyo kufa mapema huku zile za Y(zenye jinsi ya kike) zina mwendo wa taratibu
lakini zinadumu muda mrefu bila kufa, hizi ndo hufanikiwa kulifikia yai lako na kutungisha mimba ya kike.

Wakati wa maandalizi kama anakuwaga na papara. wewe fanya ujanja wa kumchelewesha mpaka pale utakapojisikia una unyevunyevu wa kutosha ndipo umruhusu. Naamini utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom