Naombeni jamani tusaidiane hili. Mume wangu alikuwa masomoni nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili, amerudi hivi karibuni. Aliporudi kanunua line ya Airtel ambayo ndio ninayoifahamu. Mie sikujua kumbe mwenzangu kanunua line ya tigo, ambayo hakunambia. Sasa siku moja usiku nashangaa msg inaingia:-
YEYE: Darling mambo vipi? Naona tangu jamaa yako arudi umenitosa
MIE: Mbona mie sikufahamu?
YEYE: Hee! kumbe tuko wengi tunaoiba? Njoo basi tukutane hapa Rose garden
Na mengine meeengiiiii.
Mie nkaushtukia mchezo hapo, ila nkasema wacha nione hii movie mwisho wake utakuwaje. Tukapanga hadi kukutana, bahati nzuri sikuwa na papara. ALHADULILAH! mara nafika eneo la tukio ni yeye huyooo!
Nilighafilika kwa kweli, ingawa hisia zangu zishantuma kuwa kama sio yeye basi ameweka watu wanitrace. Hivi ingekukuta wewe mwana JF mwenzangu, ungeliamuaje hili?
Kiukweli wote uaminifu wenu are in question! aliyeuza cheni bandia na aliyetoa pesa nae bandia. Yaaani unatuambia ukiitwa kwa simu tu twende kazi au hukuona hatari yeyote kwenda huko. Labda maelezo hayatoshi, yaani jamaa huko alikokuwa alikuwa anachapa deadly na wewe huku vivo hivyo kama tutasoma between lines
mwanamke wa kuitwa kwa sm na kufunga safari kwenda pasipo kujua nani kamwita ni m.a.l.a.y.a tu!
....whether to play along a little bit further or not siyo? some people are criminals and they would take the slightest opportunity to harm you... kama ulikuwa na wasiwasi na jamaa na ulitaka ku-find out exactly what he was up to, ni afadhali ungemu-alert mtu mwingine akupe cover (behind the scene) ili in case of any problem uweze kupata msaada
Yani ukafunga safari mpaka Bustani ya Rose kwenda kumfahamu tu...? The intention was clearly there bana! ulitakiwa umpe mumeo hiyo number ili yeye ndio ampigie huyo mtongozajiEeh! We kaka/dada ukicheche wangu ni upi hapo jamani? Mie nlitamani tu kumjua huyo anaenitongoza kwa kudai kuwa mie ni mpenz wake. Na mind you huyu mtu alionekana kunifahamu vizuri. Sasa sijui kwa nini umenihukumu hivyo
Ukweli ndo huo huyu mwanamke ni kicheche kwani kama alitaka kukamata mwizi angemtonya mumewe wakamvizie huyu jamaa lakini yeye kaondoka kimya kimya na angekuta ni sio mumewe angejirusha.Yani kama me ndio mumeo nakumwaga mazima unaonekana ni kicheche.
Pole sana umejiharibia menyewe umepoteza uwaminifu kwa mumeo, hapo alipo hakuamin hata chembe anakuona wewe ni kiruka njia anais kipindi yuko nje ya nchi ulimsaliti, ulichotaiwkukifanya ni kumweleza day one ile msg ilipoingia tu ungemshirikisha sasa hadi umfika pahali mmepangana mihadi unakuja kuomba ushauri hapa kwani wakati unatoka ulimuagaje ulimwambia unakwenda wapi.
Yani ukafunga safari mpaka Bustani ya Rose kwenda kumfahamu tu...? The intention was clearly there bana! ulitakiwa umpe mumeo hiyo number ili yeye ndio ampigie huyo mtongozaji
Ukweli ndo huo huyu mwanamke ni kicheche kwani kama alitaka kukamata mwizi angemtonya mumewe wakamvizie huyu jamaa lakini yeye kaondoka kimya kimya na angekuta ni sio mumewe angejirusha.
Nimeshasema huko mwanzo kuwa Hiyo Garden iko jirani na ninapofanyia kazi. Na mume wangu nilimshirikisha toka awali akanpotezea, so mie ningefanyaje?
Ok, asante kwa ufafanuzi ila binafsi sidhani kama ulifanya uamuzi wa busara kuitikia wito wa kwenda RG! though mumeo nae ana wivu na mitego ya kijinga
Dunia ya leo tukiachunguzana kihivyo unaweza pata vichomi tu
Na kama mume wangu ndo jamaa mwenyewe unadhani angekubali kukamatwa?
Hilo lisingehitajika maana ungeshamjibu kwamba "akukome huna muda na wapuuzi". Sasa we umeendekeza mpaka kufikoa kukubali miadi na bado unataka mumeo tu ndo aonekane mbaya.
Kaaazi kweli kweli.
Nilimshirikisha kabla hata ya kuonana naye, just at the beginning ya move yenyewe. Then nlipoanza kushtukia kuwa huenda ni yeye, nkamuuliza kama an line ya tigo akakataaa kabisa kuwa hana. Nkamwonesha na ile namba akasema haijui
alidai kuwa alitaka kunionesha jinsi wanawake wa mjini wanavyolaghaiwa
bombu hapa sasa nimekuelewa vizuri zaidi. Nilidhani hukumshirikisha kabisa, kumbe alikuwa anajua kinachoendelea. Mumeo naye namlaumu kwa mtego aliotumia, kwani ungeweza kumuumiza hata yeye mwenyewe pia. Kuaminiana ndani ya ndoa ni jambo la muhimu sana. Vinginevyo mnaweza kujikuta mnapoteza muda kwa mambo yasiyo na tija. Kama ilivyotokea hiyo siku, mliacha shughuli zenu kwenda kushughulikia jambo ambalo lingeweza kuzua ugomvi na pengine kusambaratisha nyumba. Kwa mara nyingine nakupa pole kwa uchungu ulio nao, I know how it feels. Unatamani afungue moyo wako asome mwenyewe jinsi ulivyo mwaminifu kwake. Vumilia tu, baada ya muda uchungu utakwisha, itabaki historia. Hata hivyo, kama ulivyosema, jitahidi kufuta doubts alizonazo kwako. Kwa jinsi anavyokupenda (nimemsoma from your story) atakuamini na hatokutega tena. Mwombe sana Mungu akuvushe salama kwenye machungu uliyonayo. Najua umejifunza kitu kikubwa sana kutokana na tukio hilo. Nakutakia furaha, amani na upendo wa kudumu katika ndoa yako. Barikiwa!Nilimshirikisha kabla hata ya kuonana naye, just at the beginning ya move yenyewe. Then nlipoanza kushtukia kuwa huenda ni yeye, nkamuuliza kama an line ya tigo akakataaa kabisa kuwa hana. Nkamwonesha na ile namba akasema haijui. Na baada ya hapo sms zikaendelea, nami nkasema huyo mtu ni lazima nimjue kwa sura. Hico ndicho kilisababisha niitikie mwito huo wa kukutana naye. Sasa sijui yeye afikiria nini kwa sababu hajasema anafikiria nini, ila alidai kuwa alitaka kunionesha jinsi wanawake wa mjini wanavyolaghaiwa
bombu hapa sasa nimekuelewa vizuri zaidi. Nilidhani hukumshirikisha kabisa, kumbe alikuwa anajua kinachoendelea. Mumeo naye namlaumu kwa mtego aliotumia, kwani ungeweza kumuumiza hata yeye mwenyewe pia. Kuaminiana ndani ya ndoa ni jambo la muhimu sana. Vinginevyo mnaweza kujikuta mnapoteza muda kwa mambo yasiyo na tija. Kama ilivyotokea hiyo siku, mliacha shughuli zenu kwenda kushughulikia jambo ambalo lingeweza kuzua ugomvi na pengine kusambaratisha nyumba. Kwa mara nyingine nakupa pole kwa uchungu ulio nao, I know how it feels. Unatamani afungue moyo wako asome mwenyewe jinsi ulivyo mwaminifu kwake. Vumilia tu, baada ya muda uchungu utakwisha, itabaki historia. Hata hivyo, kama ulivyosema, jitahidi kufuta doubts alizonazo kwako. Kwa jinsi anavyokupenda (nimemsoma from your story) atakuamini na hatokutega tena. Mwombe sana Mungu akuvushe salama kwenye machungu uliyonayo. Najua umejifunza kitu kikubwa sana kutokana na tukio hilo. Nakutakia furaha, amani na upendo wa kudumu katika ndoa yako. Barikiwa!
sio kweli mkuu sometimes waweza ambulia TEGO pia