Yani we umetoka nje kwanza alafu ndo utafute utatuzi wa tatizo??Kwanini hukuanza na kuomba ushauri..kujaribu kurekebisha mambo yenu na kutatua tatizo mlilokua nalo??MICHELLE UKO WAPI MAMA?Kwa style hamna kudanganyika!
Helw wana jf, tangu wiki mbili sasa nilikuwa nataka nirudi kuwashukuru kwa ushauri mlionipa kwenye thread yangu niliyoipa kichwa cha habari kama hiki hapo juu, kwa kweli napenda kutoa shukran kwanza kwa mwenyezi mungu kwa kutusaidia tatizo lile limeisha, najua ni mungu tu ndie aliyesaidia,jina la bwana lishukuriwe
Napenda kuwashukuru wale wote waliochangia thread yangu na kunipa ushauri mungu awabariki pia wale walionibeza mungu pia awazidishie walipopunguza pia shukrani za dhati ziwaendee wale walioenda mbele zaidi na kuguswa kwa namna moja au nyingine wakani pm na kunipa ushauri zaidi hawa si wengine ni Mu-sir, Fisherscom, Annony, jamal-tanga na kiraka nashukuru sana mungu awabariki sana ushauri wenu wote niliufanyia kazi kwa namna moja au nyingine.
Ilitokea tu amesafiri nje ya nchi aliporudi mambo yakawa poa na nilipomuuliza kafanya nini akaniambia hakuna alichofanya basi sijamuuliza mpaka leo. Nawashauri wote wenye tatizo kama langu, wasikate tamaa mungu yupo na anasaidia wote wenye kuelemewa na mizigo, mwisho kabisa nashukuru ile post ya michell ambayo watu wengi walicomment niifatilie pia na mimi niliipenda na kuifanyia kazi
Oooops at last am free now, nawapenda nyote, muendelee kuwa na upendo kwa wengine wote wenye matatizo, kwa kweli naipenda jf family, mungu ambariki mwanzilishi max na mods wote kwa kazi nzuri,kila siku inayoenda nazidi kufall in love nayo. ahsanteni.
Ngoja 10 wajitokeze kuuliza ni mimi?Angekuwa mwanaume sawa
Ila kwa wadada, ni mmoja tu ambaye namPM humu ndani, wengine wote naogopa
Nakupenda,nimekusoma na kujifunza mengi sana kutokana na posts zako.....nafurahi Mungu amejibu sala zetu mapema kabisa.....naamini utakuwa wa tofauti,mwenye nguvu na imani zaidi baada ya ushindi huu.....kila la kheri,ufurahie ndoa yako na katika gumu lolote,hili lizidi kukukumbusha Mungu yupo na hakupi jaribu kubwa kuliko uwezo wako na kuwa yote yanawezekana kwa wanaompenda na kumuheshimu.nimefurahi sana....Mungu awabariki sana na kuwazidishia furaha na amani!!!
JAMANI MUME WANGU prt 1 hii hapa...www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/104807-mume-wangu-jamani.html
Hongera sana kwa kufanikiwa unajua leo kidogo niku PM ili nikuulize feedback lakini nimefarijika sana kusikia tatizo limeisha. Ushauri wangu tu ni kwamba mweleze awe mwaminifu kwako kama ambavyo naamini wewe ndivyo ulivyo. Thans again.
Tunashukuru dada kwakutuletea feedback. Nasi tupo pamoja katika kumrudishia Mungu utukufu. Ila ningependa kutoa ushauri kuwa tunapoandika jina la Mungu au Yesu basi tutumie herufi kubwa maana haya ni majina na pili ni majina yenye nguvu tofauti kabisa na majina yetu ya kawaida. Kwaweli mtu akitumia herufi ndogo kwenye kutaja Mungu, Yesu Roho Mtakatifu huwa najisikia vibaya nakuona kama tunayashushia hadhi. Mbona majina yetu tunatumia capital letters? Ubarikiwe dada.
Mhimili mkuu wa ndoa ni kujamihiana. Sasa njemba inaposhindwa ku do na maiwaif wake kisha inachomokea kwa hawara kutafuta pumziko hapo jamaa anakuwa hajafumbua tatizo zaidi ya kutafuta maradhi.Nashauri mke awe ngangari amwambie jamaa aache ukware wakae watafute suluhisho la kwa nini ngoma inalala doro.Njia nyingi za kumsaidia jamaa wengi wamezieleza kwenye hii thread na ikibidi kwa pamoja kama couple wafanyiwe counselling.Jogoo kukataa kuwika kwa wanaume ni jambo la kawaida kabisa na tiba ni ya kisaikolojia zaidi.
Amesema hafikii hata robo ya mumewe! Sasa kama mumewe akimgusa tu hisia zinapotea na uume unasinyaa, hiyo robo yake ndio ikoje? Ni kweli hii story haijakaa sawa. Kama anahitaji msaada kweli hapa kwenye forum (na ninaamini wapo watu ambao ni professional na pia wapo wenye uzoefu hapa wanaweza kumsaidia), basi hana budi kuiweka story yake vizuri ili ieleweke.
Ahsante dear. Ila nakushauri endelea kuhudhuria ili Mungu azidishe ulinzi katika ndoa yako nawe pia ukuze imani yako kwa kulijua neno.Hongera sana gaga jipongeze kwa hilo imebidi nifukunyue ili nijue yalokupata, hata mbuzi chinja nyumbani,katoe sadaka kanisani kwani hayo yote ni neema ya mungu imekudondokea,wengi wameikosa na bado wanaitafuta. kwa hiyo sasa burudani kama kaaida, sipati picha nikikosa miezi sita tu naandamana