Mume wangu anachepuka

Mume wangu anachepuka

mrsfulani

Senior Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
113
Reaction score
69
Habari za uchaguzi wakuu,Poleni na heka heka.

Mim ni binti wa miaka24 naishi na mwenzagu hatujazaa bado, tabia ya mwenzagu inanikera kwakeli anatabia ya kurudi usiku sana sa 10 mpk 11 siku nyingne nimeongea nimechoka siku hizi namuanglia tu nshawambia wazee,wazazi lakini mwezangu hasikii kwa madai yake anakuwa na washkaji bar ( sijui wao hawana familia) hii imekuwa tatizo kwangu mpaka nimezoea nimeamua kukaa kimya.

Kitu kingine ni suala la mtoto sote tunahuitaji wa mtoto hospitali wanaseni mim nipo sawa (yeye hajapima) lakini nikimuuliza mwenzgu labda ktk pita pita zake ashawahi kumpachika binti mimba anakaa saivi nikimuuliza anasema yupo ina miezi mitatu Mara nakutania hakuna kitu kama icho nanyamaza tu ikipta kama miezi nkamuuliza tena akakubali yupo anayo baadae anasema nakutania namuaglia tu.

Sasa leo tumewasiliana vizuri tu baadae simu yangu ikaaita kumbe imejipinga naskia sauti anaongea na mke kwenye gari nimewasikiliza sana tu.Nashindwa kumuelewa kabisa huyu bwana.

Wakuu naomba mnisaidie bado sijafunga ndoa mimi ndo nasita sita naogopa mno nahisi hata mimba haingii ni Mungu tu ananiepusha na kitu nimevumilia mno ila moyo unauma mno aisee ( poleni kwa kuwachosha.)

Nahitaji ushauri wa faraja sio matusi
 
pole sana....kama ndoa bado...JIONGEZE...alafu huyo mwenzako analeta masihara kwenye hamna....
 
Toroka uje kama King Kingunge halafu njoo tule Bata Lowassa akiapishwa!
 
Hebu ondokaa fasta, uchumba anakutesa na ndoa je?
Na acha kujipeleka kwa mwanaume kama haupo kweny ndoa, unataka akuoe kwa kipi kipya while kashakuzoea in nd out???
Changanya miguu uondokee
 
We nipm tu kama unataka kupata mimba hapo utasubir sana utaota mvi
 
Hujafunga ndoa
Mwanaume mala.ya
Wewe binti bado


Hivi binadamu wengine mpaka muombewe???????? Unachong'ang'ania hapo ni nini???
 
Usikimbie nyumba yako hata kama bado hamjafunga ndoa jaribu kukaa na mwenzako muongee na pia jaribu kukumbuka ibada kila siku maombi yako yaelekeze kwa mungu atabadilika na mtaishi tu kwa Amani.usichoke omba kila siku usikimbie matatizo tafuta suluhu.

PIA UMRI NDIO UNASABABISHA HAYO. ATAKUA NA ATATULIA
MUNGU ATAKUSAIDIA
AMEEEN.
 
Hujafunga ndoa
Mwanaume mala.ya
Wewe binti bado


Hivi binadamu wengine mpaka muombewe???????? Unachong'ang'ania hapo ni nini???


Mahaba nipoteze kwenye rada nsionekane kabisa hatuwez jua maybe Kuna kitu mwenzetu anapata hapo ndo maana kabakia
 
Hapana aisee... Mwanaume anakujia saa 10-12 alfajiri hata ndoa hamjafunga. Mkifunga atagraduate kabisaaaaa kuja kesho yake ama kesho kutwa.

Hivi hujui nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe???

Ukiona manyoyaaaa.....

Kalaghabahoooo!!!!!!!
 
Mh! Za kuambiwa changanya na zako halafu fanya maamuzi. Huo mda ni hatari sana kwa vjana wadogo. In short tafuta amani kwingineko


Pole
 
Mabinti mna uvumilivu wa ajabu. Sizan kama had sasa ww n binadam wa kawaida. Hujishtukii tu?... Try to check your humanity... Seeeeepa faster ohooooo
 
Back
Top Bottom