Habari za uchaguzi wakuu,Poleni na heka heka.
Mim ni binti wa miaka24 naishi na mwenzagu hatujazaa bado, tabia ya mwenzagu inanikera kwakeli anatabia ya kurudi usiku sana sa 10 mpk 11 siku nyingne nimeongea nimechoka siku hizi namuanglia tu nshawambia wazee,wazazi lakini mwezangu hasikii kwa madai yake anakuwa na washkaji bar ( sijui wao hawana familia) hii imekuwa tatizo kwangu mpaka nimezoea nimeamua kukaa kimya.
Kitu kingine ni suala la mtoto sote tunahuitaji wa mtoto hospitali wanaseni mim nipo sawa (yeye hajapima) lakini nikimuuliza mwenzgu labda ktk pita pita zake ashawahi kumpachika binti mimba anakaa saivi nikimuuliza anasema yupo ina miezi mitatu Mara nakutania hakuna kitu kama icho nanyamaza tu ikipta kama miezi nkamuuliza tena akakubali yupo anayo baadae anasema nakutania namuaglia tu.
Sasa leo tumewasiliana vizuri tu baadae simu yangu ikaaita kumbe imejipinga naskia sauti anaongea na mke kwenye gari nimewasikiliza sana tu.Nashindwa kumuelewa kabisa huyu bwana.
Wakuu naomba mnisaidie bado sijafunga ndoa mimi ndo nasita sita naogopa mno nahisi hata mimba haingii ni Mungu tu ananiepusha na kitu nimevumilia mno ila moyo unauma mno aisee ( poleni kwa kuwachosha.)
Nahitaji ushauri wa faraja sio matusi