Hellow wanaJF,
Leo kuna huyu dada rafiki yangu sana yaani ni kama mwandani wangu tumeshibana sana tuu. Issue iko hivi huyu bibi ana bwana wake wote ni wafanyakazi wa umma ni mwanamke mwenye upeo wa kuona mbali anayejiheshimu na kujielewa sana.
Walichukua mkopo na mumewe ili wajenge nyumba kipindi hicho wakiwa nyumba za kupanga wamehamia last year mwezi December ikiwa haijakamilika vizuri ili kuepuka tu usumbufu wa kodi za upangajini kumbuka hapo bidada na mumewe walichukua mkopo wote.
Dada wa watu anakatwa anabaki na mshahara wa laki mbili tu kwa mwezi
sasa hivi nyumba washaweka na geti na at least sasa ina mvuto wa kuwa nyumba nzuri lakini toka wamehamia mume amekua mkali sana anaongea na kujibu kwa hasira sana jambo dogo tu hata mtoto akilia tu huyu bwana anafoka isivyo kawaida na wakati before wakiwa upangajini huyu mume hakua hivyo.
Mke anaumia sana mumewe anapobadilika kias hicho amevumilia sasa too much akaniomba ushauri nikamwambia ajitahidi kumzoea ila nashindwa kuelewa kwanini mume wake kabadilika hivyo.
Sent using
Jamii Forums mobile app