Mume wa mtu nomaah! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume wa mtu nomaah!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bahaticaro, Jul 22, 2012.

 1. bahaticaro

  bahaticaro Senior Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah! inaniuma sana nilipata boyfriend na nikampenda sana kumbe ana mke na mtoto mara ya kwanza aliniambia kuwa ana mtoto ila haishi na huyu aliyezaa naye nikamuuliza sababu akasema kuwa huyo mwanamke alimdharau na pia hakutaka kumuoa alikuwa anataka mtoto tu.. baada ya muda nikagundua kuwa dada aliyezaa naye anampenda na kuna muda anaenda kwake juz kati tena huyu boyfriend ananiambia et baba yake mzaz huyu boyfriend kamleta huyo dada aishi kwake kwa kumlazimish mim nikamwambia ni vizuri bas tuachane ili yeye aishi vizuri na mke wake et ananiambia kuwa anaish naye nyumba moja ila hamna communication yoyote na huyo dada na kila mtu analala kwake.....inaniuma kwasababu mimi ndiyo ninaye sababisha huyo dada kufanyiwa vituko na nikimwambia tuachane ananitishia.naombeni ushauri jaman nifanyeje?
   
 2. mito

  mito JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,644
  Likes Received: 2,033
  Trophy Points: 280
  Unaogopa kutishiwa tu au una lako jambo?
   
 3. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kiukweli uyo mtu wako anaweza kuwa si mkweli so chapa mwendo na maisha yako.
   
 4. Meljons

  Meljons JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 2,591
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  wewe dada acha hizo! Achana na huyo mwanaume amlee mkewe na mtoto wake.
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Tafuta njia ya kutokea(kimbia)
   
 6. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Fanya maamuzi magumu ya kuachana nae, atakua anampenda huyo msichana huku akikutamani na wewe, kama angekua ni mwanaume mwenye maamuzi yake asingesema eti babake mzazi kamleta huyo mdada aliezaa nae ili waishi wote, bila ridhaa yake, ni muongo na atakupotezea muda.
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Si unaogopa vitisho endelea kuwa naye........siku ukimwagiwa maji ya moto ndipo utajua kwa nini nyanya si matunda
   
 8. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,477
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa anakutishia mwache kimyakimya, hatua kwa hatua. Usimpe tena keki, punguza mawasiliano ya simu na pia ya kukutana ana kwa ana. Akikuuliza mbona hivi? Sema poa tu hakuna lolote. Mbona hujibu msg? Niko bize. Tukutane .... Sema sawa lakini usiende. Zima simu. Mbona hukuja na simu ulizima? Nilipata safari ya ghafla, samahani halafu simu nilisahau nyumbani au iliisha chaji. Fanya tu vitimbi hadi akate tamaa. Usimwache gafla.
   
 9. G

  Geam Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kama umegundua wewe ndio unamtesa dada wa watu acha! Subir mume wako
   
 10. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold hapo...kinachokufanya umuamini huyo muhongo ni nini? Hivi kweli unategemea akuambie nikitoka kuku do naenda kum-do na mwenzio???

  Huyo ni mkewe na anampenda...usikubali cheap lies za eti wazazi wameniletea mke..utashangaa wanaongeza mtoto wa pili na wa tatu endelea na uamuzi wako wa kusonga mbele...acha kuonea huruma watu wasiostahili.

  Maana hata mkiendelea mwisho wenu ni upi? Utakuwa kimada maisha yako yote?

  Afu tembela blog moja ya mwanamke na nyumba uone stori za wadada waliofanyiziwa kwa kutembea na waume za watu.

  Sawa hukujua ...sasa umejua...hakuna excuse tena.

   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  anakutishia?????
  Anakutishia nini?

  Unataka tuamini uko nae kwa kuwa anakutishia??????
   
 12. kashata

  kashata JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Kumbe ndio mnavyotutosa wanaume kwa njia hizi from now sitomuamini tena demu akitoa visingizio kama ulivyovitaja.
   
 13. Collins

  Collins Senior Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nʇɐʍ ɐz әɯnɐʍ ɐu ɐuɐႡɔɐ'әʍәʍ oz!Ⴁ ɐႡɔɐ'ɐ!snʞnႡ !u!uɐʍʞ !Ⴈәʍʞn ɐ!qɯɐnʞ!Ⴈɐ
   
 14. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  aisee, kuna wanaume ni wataalamu wa kufunga kamba si masihara, yaani binti anapigwa fix mpaka anakosa njia ya kutokea
   
 15. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  huyu dem mwenyewe anampenda msela..anatuzuga tu,.
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Dadaangu kwani wewe hujihisabu kuwa una haki ya kuwa na mume? Na akuowe mbanane hapo hapo uone kama hatakuwa mumeo hata kama unashare.
   
 17. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  red- So my dear in other words you are not matured enough to make firm decisions?
  Hata nyepesi kiasi hiki? Sasa kwa nini usisubiri ukue ndo uingie kwenye mahusiano?

  green - Really inakuuma? Just wait ukae upande wa huyo dada ndo utajua maana halisi ya maneno hayo. U should've walked away the minute you realised that. Wadada kama nyie ndo mnapenda sana kupangishwa foleni...
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hapo sasa unataka ushauri gai wakati kila kitu unakiona???? kama unapenda kuwa mtazamaji sawa lakin maamuzi ya msingi unayo naamin ulishayafanya..
   
 19. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Pole shost,lakini mbona kwa maelezo yako inaonyesha wazi unafurahia yanao mkuta mwenzio? kwanza jamaa muongo,kama mie ningesha malizana nae zamani sana,anakutisha inamaana anakubaka humpi Chali kwa ridha yako?
  ebu shosti jikaze kike na kama mwanamke kweli tafuta wako peke yako huto furahi ukijakusikia mumeo anamwanamke mwengine njee,sasa basi kabla hujafanyiwa hayo acha kumfanyia mwezio......
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,510
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Mie hata sijakuelewa unasaka Ushuaia juu ya nini? Kutishiwa, kufanyiwa vituko Hugo dada mwingine AMA kabaka 'the other woman'?
   
Loading...