Mume na mtoto wa nje!!!

Pole sana dada, Jitahidi sana kumwomba Mungu atakuongoza kuamua jambo la hekima kwako na kwa familia yako.
haya mambo huwa yananiumiza sana kichwa, wamama wengi sana wanapolalamika kuhusu kugundua waume wao kuwa na watoto wa nje huwa tunawashauri wavumilie na kuwapenda hao watoto wa nje, kisa watoto hawana makosa. Ni kweli watoto hawana makosa, lakini tujaribu kujiweka kwenye nafasi za hao wamama, ni kweli tungeweza kuwalea kwa upendo hao watoto wa nje kisa hawana makosa?
Kwa mtoto ambaye umemkuta kabla hujaolewa naweza kufikiria, lakini huyu ambaye kazaliwa tukiwa tumeoana, tena mdogo kuliko watoto wangu! hili huwa nakataa kuliwaza. hii inaonyesha dhahili kuwa huyu baba hajipendi hata mwenyewe, pamoja na kumpa mimba mtu huko nje anaweza akapata na magonjwa mengine pia. kama kweli umemtamani mtu huko nje kwa nini ujiachie kiasi kwa kusababisha mimba?
 
Mh,endeleeni kuchangia kwanza,maana na miye nina soo langu kidogo linafanana na hili,labda naweza nikapata majibu kwenye hii thread ila nikikosa ntaiachia ili mnipe mawazo,pole sana mama.
 
Pole sana shost, samahani lakini kwani huyo mumeo dini gani na huyo mwanamke kazaa nae tuu au kamuoa? isitoshe usitoke kwenye ndoa yako ukampisha yeye banana nae mpaka kieleweke,najua kama sio rahisi unahisi kama kuchanganyikiwa lakini jikaze wewe mwanamke na usikubali mwanamke mwenzio akakuzidi kete,kama mume mumeo wewe na unajua nini anapenda zaidi analadha gani na wapi mtamu funga mbeleko umrudishe mumeo nyumbani mlee watoto wenu na kumbuka hakuna ndoa
isiyo kua na misukosuko inshallah mwenyezi mungu atakupa moyo wa subra na ushindi.

sisi wote ni wakristo,na huyo mwanamke amezaa nae tu.asante kwa ushauri.
 
mume wangu mapenzi hajapunguza,na wala anidharau ata kidogo,kunitambulisha hajanitambulisha,kumfahamu huyo dada simfahamu,kumuuliza nimemuuliza ameonyesha kujutia kosa ila siwezi muamini tena.
 
Kazi kweli! Kama unadhani unahitaji mtoto wa 3 na wewe mchakachulie. Formula ni kuwa mna open marriage, na wewe uta-apologise tu yeshe. (Tahadhari, uwe tayari kuachwa. Kama ni tegemezi sana chakachua kwa siri)

mmmmmmmmmh hilo nalo neno KING'ASTI,hivi inawezekana kweli?hahahhahah ngumu sana hiyo kwakweli.
 
Inauma, huyo si mwaminifu kaa mzungumze hayo matatizo kama bado ana mahusiano na mama wa huyo mtoto ama sivyo, usiondoke kwa kuwa una watoto wadogo. Ikiwa ataamua kukuletea huyo mtoto umlee, sikushauri hata kidogo.

ni kweli madame X ila unafikiri ata kama bado anamahusiano nae anaweza kukubali?ngumu sana hiyo!!!!
 
kumbuka kuwa yawezekana unamtimizia yote mumeo,halafu bado kaenda nje,niamini maneno yangu,mwanaume kwenda nje si kwamba umridhishi,ni hulka tu!ila wewe usimnunie hata kidogo ongeze mapenzi zaidi na zaidi,pia muombe sana mungu wako,atakusimamia.

ni kweli mwenzangu unaweza ukajitahidiiiiiiiiiii weeeeeeeeeee ila kama mtu hiyo ni tabia yake kumbadilisha ngumu,mimi sijamnunia ila mwenyewe ajiamini kwa ukimya wangu.
 
pole dada, lakini nadhani kuna vitu umeanza kuhisi ndio ukapelekea kugundua, au sio?
vifanyie kazi na mungu akupe nguvu, hata picha sipati uchungu ulionao sasa
Ila ile honeymoon ndio imeisha sasa uanze maisha! uwe mwanamke jasiri.
 
sikujua kama ndoa inapendwa namna hii.mume aki cheat vumilia,kazaa nje,vumilia,ana nyumba ndogo,vumilia,mmmh.jamani kama mimi sina trust,siwezi kuvumilia.kazi yangu ndio mume wangu.wapo ambao hufanya vitu,hujuta na hawarudii.ila wapo wengine,hujipa break halafu wakaendelea na machafu yao
 
Mmh, pole
Ndo ukubwa, ukiondoka anamuoa kabisa yule aliyezaa naye.

Lakini pima furaha yako na future ya watoto wako.
 
Back
Top Bottom