kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Eti mume na mke waligombana, mwanamke akakukusanya nguo zake kwa lengo la kuondoka: Mume akuuliza' unaenda wapi? Mke akajibu "ninakwenda kwa mama yangu." baada ya kusikia hivyo mume naye akaanza kukusanya mizigo yake ili na yeye aondoke. Mke kwa jeuri akauliza: Unakusanya nguo unakwenda wapi? Mume akajibu kwa tabasamu: Nakwenda kwa mama yangu. Mke akauliza' hao watoto wako watabaki na nani? Mume kwa kujiamini: Nao waende kwa mama yao, kama sisi tunavyokwenda kwa mama zetu!