Nina jirani yangu kanijia kwa masikitiko kwamba mumewe amekuwa ni anayependa kukopa mno. Anadai kwamba tokea wakiwa wachumba amekuwa akimkopa yeye, akikopa kwenye makampuni ya wakopeshaji nk. Tabia hii haijabadilika hadi hivi leo wameoana zaidi ya muongo mmoja. Kinachomuumiza ni kwamba hajawahi kumrudishia hata centi moja. Hizo hela akikopa hata hajui anachofanyia manake mahitaji yote ya nyumba ni mama ndio anatimiza. wote wawili wana kazi na mshahara hautofautiani sana. je afanyeje kumsaidia huyu kidume na tabia yake ya ukopaji?