Mume, mipaka yake kwa mkewe mwisho wapi

Mume, mipaka yake kwa mkewe mwisho wapi

una uhakika na tabia ya binamu yako?usikute ni mcharuko ndo maana jamaa anambana.its not wise to judge based on one side of the argument.mtafute shem mukae friendly na umuulize his side of the story
 
Mipaka hakuna bali panapo bidi waheshimiane kama mke na mume..
 
..ila twende mbele turudi nyuma kuna baadhi ya kinamama yaani hadi keero.. Usitokee msiba/harusi/kicheni pati/mwali anatolewa/shughuli yoyote mtaani anataka awemo! Hata nyingine hazimhusu kivile lakini utashangaa anavyohangaika kwenda.. Mama anaadimika nyumbani kila siku yuko mara kwenye ngoma, mara vikao vya harusi, mara sijui vikundi.. Khaa! Hapo bado hajaingia kwenye mikesha.. Hebu baadhi ya wamama mjiangalie jamani matatizo mengine mwayasababisha wenyewe..
 
Ukihangaika na hili tatizo basi utakuwa unahangaika na matawi ya tatizo na si kwenye shina na mizizi ambako ndio haswa kunahusika. Hayo mnayoona ni matokeo ya matatizo katika ndoa/maisha yao. Huwezi jua cousin wako kamfanyeje mumewe na wala huwezi jua ni nini hasa kilichompata huyo mumewe.

Ongea na cousin wako ili akatafute msaada wa hayo matatizo yake, na kama anayakalia basi ujue na yeye kuna vitu anaficha. Kama mumewe hakuwa hivyo jua kabadilika baada ya kupitia kitu kilichomfanya aone hayo maamuzi yake ni suluhisho hata kama si sahihi. Waache hao wanandoa watafute suluhisho wewe hutaweza kitu. Kuna mahali inabidi kuheshimu mipaka ya ndoa hata kama unaona kuna tatizo
 
Huyo mwanaume tabia yake ni hiyohiyo hata kama anekuwa hajaoa so ndoa isionekane ni mkosi hakuna kitu inanipa raha na furaha kama ndoa!unakuwa na mtu anakuona kama baba wewe ndo kila kitu halafu na wewe unampenda kuliko hata nafsi yako.....hongereni sana wana ndoa wenzagu.....si vizuri mtu aishi peke yake nitamtafutia msaidizi wa kufanana naye.

Umenena mwanakwetu!
 
Ndugu hapo ujue umeongelea upande mmoja, upande wa dada ako kuko sawa? Hayo ni matokeo tu, kuna chanzo cha matokeo hayo.
 
Amsikilize tu mumewe inawezekana vishughuli vimezidi huko ukwen sa kila wiki mke yuko kwao si jambo jema
 
Nilichokihisi hapo kwa haraka sana.

Dada yako ni sharp shooter, amegundulika.
 
asilazimishe asikilize kwani akileta ubeiijingataumia yeye...menginekuwa mtiifu af hatujui undani wake kunani
 
Back
Top Bottom