Mume amuunguza sehemu za siri mke wake

Mume amuunguza sehemu za siri mke wake

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Mwanamke mkazi wa kijiji cha Matui, Wilayani Kiteto, Mkoani Manyara ameponea chupuchupu kuuawa baada ya mume wake kumchoma na chuma cha moto sehemu zake za siri, kutokana na wivu wa mapenzi.
Mwanamke huyo alifanyiwa kitendo hicho juzi usiku kwenye kijiji hicho, baada ya mume wake kumtuhumu kuwa ana uhusiano wa mapenzi na msaidizi wao wa nyumbani.
Akizungumza kwenye Hospitali ya wilaya ya Kiteto juzi, wakati akipatiwa matibabu mwanamke huyo alisema hivi "kwa sasa anasikia maumivu makali sana".
Alisema alipofanyiwa kitendo hicho alipoteza fahamu kwa muda mrefu, kwani alitokwa na damu nyingi na alizinduka baada ya kufikishwa hospitalini hapo iliyopo umbali wa kilomita 32 kutoka nyumbani kwake.
Alongeza kuwa kabla ya kufanyiwa kitendo hicho, kila mara mume wake alikuwa anamweleza kuwa amesikia tetesi kuwa ana uhusiano wa mapenzi na msaidizi wa kazi hivyo atamfanyia kitu ambacho hatakisahau.
"Siku ya tukio hilo, alikoka moto akachukua nondo ya kuweka alama kwenye ng'ombe, akaniambia "ingia ndani mke mwenzako anakuita", nilipoingia ndani naye akaingia na kufunga mlango akaniingizia hiyo nondo ya moto", alisema.
Daktari wa hospitali hiyo Godfrey Mbise alisema mwanamke huyo amepata kilema cha maisha baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili, kwani ameachiwa majeraha sehemu zake za siri, mapajani na mgongoni.
Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Matui, Kidawa Athuman alisikitishwa na kitendo cha Polisi wa Kituo cha Matui kutochukua jambo hilo kwa uzito.
Athuman alisema askari hao wanashindwa kumchukulia hatua mwanaume aliyefanya kitendo hicho, kutokana na nguvu kubwa ya uchumi aliyonayo.

…Source by Mwananchi - Jumapili, Januari 13, 2013
 
Mapenzi yanaua haswa umpendae akitendwa ndivyo sivyo na wengine
 
huyo baba katili sana. Ni bora angemuacha mama wa watu aendelee na maisha yake kuliko kumharibu mgodini wenye madini yote.
Udumelism tanzania kuisha bado sn wapendwa. Ye ana wake wawili je anawatimizia haja zao za kimwili ipasavyo? Km angekuwa anatimiza sidhan km huyo mkewe angegegedana mtu mwingine.
Haya sasa keshamharibu maumbile yake, ye mwanaume ataendelea kugegedana na mke mwingine wkt huyu mama akilia na kovu lake. Hatapata mautamu tena maskini.
Ni kweli sheria ichukue mkondo wake mama wa watu apate haki yake lkn haitarudisha maumbile yake.
 
Tgnp you should follow up these kinds of cases. Tena nyang'au mwenyewe ana wake wawili, ningekuwa hakimu mie!
 
ningekuwa hakimu ningeweza sahau nikatoa adhabu kali hadi mie mwenyewe nikajifunga miaka 10.

Jamani, kisa cha kutengua uzazi wa binadamu mwingine?

Tgnp you should follow up these kinds of cases. Tena nyang'au mwenyewe ana wake wawili, ningekuwa hakimu mie!
 
Hao police wapumbavu sana wanashidwa kumkamata mtu sababu ya pesa zake..
 
Dawa ya huyo mume ni kumkata naaye dudu lake!
 
Hizi ndo kesi za kuamuliwa kwa siku moja na kufungwa maisha sio ile ya mwanajeshi wa Lema na CDM
 
Maskini duh! huyo mwanamme nadhani alikua shoga zamani ndio akawa na wivu kama huo,kwani kama hamuendani si muachane raha tele shida za nini?
 
Yaani kumtuhumu tu bila ushahidi wowote anatoa adhabu kali hivi, ana uhakika gani kama huyo mwanamke alikuwa na uhusiano na huyo msaidizi wao wa ndani? Kama siyo kweli si kampa kilema mkewe bila sababu za msingi? Huyu ndg anapaswa kuadhibiwa kama wahalifu wengine wanavyoadhibiwa!
 
..., yeye kamtuhumu na kufanya ukatili hapo kwa hapo, bila mjadala! Utasikia eti jeshi la polisi linafanya upelelezi na hajakamilika...
 
Wivu...ee mola tupe ujasiri wa kutawala hasira zetu
 
Tgnp you should follow up these kinds of cases. Tena nyang'au mwenyewe ana wake wawili, ningekuwa hakimu mie!
Mungu hakukosea kukunyima uhakimu then maana......

ningekuwa hakimu ningeweza sahau nikatoa adhabu kali hadi mie mwenyewe nikajifunga miaka 10.

Jamani, kisa cha kutengua uzazi wa binadamu mwingine?
i think wanakuwa temporarily insane!! unawezaje kumfanyia mwenzio ukatili kiasi hiki, tena mtu ulieahidi kuishi nae kwa 'shida na raha'
 
Afuvweweh! Ila mi ntafanya law tu, ngoja!
wishing u the best. ingawa ni 100x better wewe ukiwa hakimu kuliko mimi. my past failures will make me too harsh :target: in such cases.
 
Wanafamilia wanatakiwa wadumishe UPENDO WA AGAPE ili waweze kuishi maisha nyenye mafanikio.
 
Back
Top Bottom