DeMostAdmired
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 1,596
- 3,845
Yes habari za masiku ndugu zangu na poleni nyote Kwa kadhia tuliyoipata kwa kusimamishwa Kwa muda Kwa platform yetu pendwa ila hope now tupo sawa.
Happy new year pia nawatakiwa kila lakheri katika huu mwaka mpya wa 2026.
Binafsi nimekaa nikafanya utafiti wa historia mbali mbali na kutafakari kwa kina kuhusu Taifa letu la Tanzania nikagundua vitu flani flani na hatimaye kuja na huu Uzi unaoenda na title ya "MULTIPARTY DEMOCRACY NI SUMU KWA MATAIFA MASIKINI HASA YA KIAFRIKA ".
Niende chap chap ni hivi, kiukweli nimekaa nikafatilia nikaona kabisa Democracy ya vyama vingi siyo mfumo sahihi wa sisi Tanzania kuutumia.
Naomba niainishe sababu kama ifuatavyo.
1. Demokrasia ya vyama vingi ni chanzo kikubwa cha rushwa. Mfumo wa kila baada ya miaka mi5 tunachagua viongozi ni chanzo kikubwa cha rushwa na uwepo wa viongozi wasiyostahili katika safu ya uongozi.
2. Demokrasia ya vyama vingi ni chanzo cha upotevu wa mapato kutoka kwa wafanya biashara na wawekezaji kwenye nchi yetu. Wafanyabiashara hujiweka karibu na vyama vya siasa hasa vyenye nguvu na vinavyounda serikali kuvichangia katika kampeni ili waweze kusamehewa kodi, hii ni mbinu inayotumika duniani kote (mnaweza fanya utafiti) ndiyo maana China waaliamua kujiundia DEMOKRASIA yao ya kipekee.
3. Mfumo huu unaligawa Taifa. Taifa lolote ili liendelee linatakiwa liwe as a single unit, wananchi na viongozi waongee lugha moja kusiwe na mipasuko inayoathiri ushirikiano wa TAIFA HUSIKA na MATAIFA mengine kwani hali hii hupunguza mapato ya kigeni (foreign currency) kitu ambacho ni UTI wa mgongo wa maendeleo ya Taifa lolote.
4. Mfumo huu hufanya vijana wasomi wengi wawe bize na kufatilia siasa na fursa ZILIZOPO kwenye siasa hivyo hupunguza nguvu kazi ya Taifa na kudhoofisha maendeleo katika sekta mbali mbali za muhimu mfano sekta ya sayansi na teknolojia. Hii sekta ndio sekta muhimu katika kuleta maendeleo katika nchi kwasababu dunia ya sasa inaongozwa na sayansi na teknolojia mfano AI na Semiconductors (chip). Vijana wengi wasomi na wenye vipaji huishia kujinoa na kuwa sawa katika umahiri wa kuzungumza na kukosoa serikali badala ya kuwa bize katika kutumia usomi na vipaji vyao katika kulinufaisha Taifa.
5. Mfumo huu unapunguza uzalendo na uwajibikaji Kwa viongozi. Kuchagua viongozi kila baada ya miaka mi5 hufanya viongozi kutumia fursa ya miaka mitano uongozini kujiweka sawa kujiandalia pesa nyingi watakazozitumia kujibakisha MADARAKANI Kwa miaka mingine mitano hivyo rushwa, ufisadi na nepotism vitashamili na hivyo kudidimiza haki na maendeleo ya Taifa.
6. MFUMO huu hupandikiza dhana mbovu juu ya kila uongozi unaokuwepo MADARAKANI kwani huwapo fursa wanasiasa pinzani kuzungumza vitu ambayo hata kama siyo vya lazima Kwa wakati huo na hatimaye dhana hizo huishia KUSHUSHA uaminifu wa wananchi Kwa viongozi walipo MADARAKANI na mwisho kabisa kuharibu mshikamano na umoja wa TAIFA ili kuleta maendeleo.
7. Mfumo huu huwafanya viongozi wajilimbikizie pesa ili kuwahonga wananchi kwa wingi wao ili wawapitishe kwenye kura za maoni na uchaguzi Mkuu hivyo viongozi hawatakuwa bize na kutatua KERO za muda mrefu Kwa WANANCHI bali watakuwa na kazi ya kujiweka sawa kiuchumi wakijiandaa kutatua KERO za muda mfupi sana na ndogo ndogo zinazotatuliwa na vishilingi vichache na hivyo kero za muda mrefu kubakia bila kutatuliwa.
NITARUDI NA MUENDELEZO KUHUSU MAONI JUU YA MFUMO GANI HASA BINAFSI NAONA UNATUFAA WATANZANIA.