Elections 2015 Mulongo anasurika kipigo, kisa Lowassa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
VURUGU zimetekeo katika kikao kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, kilicho wakutanisha watumishi wa Halmshauri ya Kwimba pamoja na walimu wa shule za msingi wilayani humo.

Vurugu hizo zilitokea wakati Mulongo akizungumza watumishi hao wa umma, ghafla kulizuka minong`ono iliyotokana na mkuu huyo kumnanga, Mgombea Urais wa Chadema anayeungwa na mkono na Ukawa, Edward Lowassa.

Inadaiwa kuwa baada ya watumishi hao kubaini mkuu huyo wa mkoa hakuwa na ajenda yeyote inayohusu changamoto zinazowakabili bali ni kampeni za CCM ndipo ilianza minong`ono iliyosababisha kikao hicho kuvunjika.

Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mwalimu mmoja amesema kuwa kilichosabisha wao kuanza vurugu ni kutokana na Mulongo kuanza kampigia kampeni mgombea Urais wa CCM, John Mgafuli.

Amesema wakati akiendelea kumfanyia kampeni mgombea huyo, huku akimnanga Lowassa kwa lugha za kejeli ndipo walimu hao walitaka kuuliza maswali ni kwanini anatoa lugha hizo, ambako Mulongo aling`aka na kusema kwamba ni maelekezo na kwamba hakuna maswali.

"Watu walipogundua kwamba hakuwa na ajenda yeyote zaidi ya kutukana Lowassa, ndipo vurugu zilianza na tulipotaka mkuuliza maswali alikataa, kila mtu anaitikadi zake na watu wamelipa nauli zao kufika kwenye kikao," amesema Mwalimu huyo.

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa wakati vurugu hizo zikiendelea, Mulongo aliagiza Polisi ambao walifika na kumkamata mtumishi mmoja ambaye inadaiwa alilala rumande.

Mkuu huyo wa Mkoa, Magesa Mulongo alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia vurugu hizo, amesema kwamba yeye hafanyi kazi katika Halmshauri hiyo na kwamba huo ni upuuzi mtupu.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Pili Moshi, yeye alipozungumza alidai kwamba yupo nje ya ofisi na kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo na kumtaka mwandishi kumtafuta Jumatatu ya wiki ijayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba (OCD, Athuman Mkilindi alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, alidai kuwa yeye sio msemaji wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza huku akiishia kusema: "Ndugu suala si linafahamika, muulize RPC (Kamnada wa Polisi Mkoa), Charles Mkumbo."


Chanzo: MwanaHalisi Online
 
Jamani huko kwimba mansoori vipi??
Mnamrejesha au mnaenda na ukawa??

Maana pale mjini nilishuhudia mwenyekiti wa chadema akishinda
 
Kama Habari hizi ni kweli kwanini viongozi wanataka kuaribu amani yetu na mwenyeenzi Mungu awaangali Kwa namna ya peekee
 
Ifike Maali Hawa Wa Kuu Wa Mikoa Na Wilaya Wapokwe Mamlaka Hizi Hapazo Wanazitumia Vibaya Kukandamiza Haki Za Wafanyakazi. Jeshi La Polisi Liwe Taasisi Huru Na Sio Kuwa Chini Ya Mkuu Wa Mkoa Na Wilaya Maana Wanalitumia Jeshi La Polisi Vibaya.
 
Atasababisha waalimu wachukie taaluma yao NA kutoa elimu duni kwa watoto
 
Heshima ya walimu inakaribia kurudi.

Kamanda, heshima ya walimu inarudi kwa kasi sana.

Arusha, wiki 2 zilopita, waalimu wa Arusha School walimzomea, walimtukana na wakavunja kikao cha mwajiri wao mkurugenzi mtendaji wa jiji (natumai nimepatia cheo).

Wamechafukwa nchi nzima!!
 
Kwenye hili tukio ni Mwandishi wa gazeti moja tu alikuwepo? Tupate uhakika kutoka vyombo vingine vilivyokuwepo katika tukio hilo ili niweze kuamini. Mi nawafahamu waalimu hawako hivo. Hawawezi kumpiga kiongozi wao. Hata kama hawakubaliani wangekaa kimya ila wangebaki na msimamo wao. Kama walimu wamefika hapo basi taifa limekwisha.
 
Kwenye hili tukio ni Mwandishi wa gazeti moja tu alikuwepo? Tupate uhakika kutoka vyombo vingine vilivyokuwepo katika tukio hilo ili niweze kuamini. Mi nawafahamu waalimu hawako hivo. Hawawezi kumpiga kiongozi wao. Hata kama hawakubaliani wangekaa kimya ila wangebaki na msimamo wao. Kama walimu wamefika hapo basi taifa limekwisha.

Mkuu, soma bandiko langu namba 20. Taifa linazaliwa upya. Walimu ni sahemu ya mabadiliko yajayo maana nao wameteswa sana!!

Kila nyanja watu wamekata tamaa maana wamevumilia sana ila CCMscrow wanagawana tu pesa badala ya kusambaza huduma za jamii na kujali maslahi ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo na kati.

Hata maeneo ambayo usingetarajia, wameamua ni MABADILIKO tu!! So, usishangae walimu kuzodoa mkuu wa mkoa. Ndo mabadiliko hayo.

Kama upo nje ya system ijayo (UKAWA), kubali kudhihakiwa maana ni muda wa wenye nchi kunufaika!
 
Huyo mulongo alikuwa mkuu wa mkoa arusha,lkn alinyoosha mikono,akaomba uhamisho,kila alipopita alikumbana na zomeazomea.
 
Back
Top Bottom