Mulla apora Kiwanda cha Chai, Lupembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mulla apora Kiwanda cha Chai, Lupembe

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MAMA POROJO, Apr 24, 2011.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]MUVYULU ni Muungano wa Vyama vya Msingi toka katika vijiji 9 vya Tarafa ya Lupembe.MUVYULU kilianzishwa mwaka 1998, kimesajiliwa kisheria , na kinaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi, wakiwakilisha vyama vya msingi vilivyounda MUVYULU.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]MUVYULU, kama chama kinamiliki hekta 215 za mashamba ya Chai na kina hisa katika Kiwanda cha Kusindika chai cha Lupembe. Kuna jumla ya wakulima 6036 wanaomiliki mashamba binafsi ya chai yenye jumla ya hekta 4200, nje ya shamba la ushirika. Mashamba haya yana uwezo wa kuzalisha tani zaidi ya 10,000 za majani mabichi kwa mwaka , ambayo yanapouzwa huwapaia wakulima waastani wa shilingi bilioni 1.3. Baada ya kuisindika chai huliingizia taifa dola milioni 3.3 za Kimarekani kwa mwaka.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kabla ya Ubinafsishaji, Kiwanda cha Kusindika chai cha Lupembe kilimilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na MUVYULU ambapo serikali ilimiliki asilimia 25.76% na MUVYULU kilimiliki asilimia 74.24% ya hisa zote.. Tarehe 19/03/2004 MUVYULU na PSRC walisaini mkataba wa kuuza hisa asilimia 70% kwa kampuni ya Dhow Mercantile(EA) Ltd kwa lengo la kuboresha uzalishaji na usindikaji. MUVYULU kilibakia na asilimia 30% za hisa katika ubia huo. Makubaliano yalikuwa kwamba kampuni ya Dhow Merchantile ilipe asilimia 10% mara moja baada ya kusaini makubaliano, asilimia 40% baada ya kusaini mkataba wa mauzo na asilimia 50% ndani ya kipindi cha miezi 12 tangu kusaini mkataba .[/FONT]

  [FONT=&quot]Hadi sasa ni mwaka wa saba unakwisha tangu Dhow Merchantile wachukuwe kiwanda na hawajalipa malipo ya asilimia 50% kama makubaliano ya mkataba yalivyo walitakiwa wawe wamelipa ndani ya miezi 12.. Kwa maana nyingine, Dhow Merchantile wamevunja mkataba . Cha kusikitisha zaidi, Dhow Merchantile wameteka nyara mamlaka yote ya Kiwanda kwa kukataa kuishirikisha MUVYULU kwenye uongozi na udhibiti wa mapato na matumizi ya kiwanda kama mkataba unavyoelekeza. Jitihada zote za PSRC na MUVYULU za kuwataka Dhow Merchantile kutimiza masharti ya mkataba na kuwashirikia MUVYULU katika uendeshaji wa kiwanda zimegonga mwamba.[/FONT]

  [FONT=&quot]Katika jitihada za kuendelea kutafuta suluhu kabla ya kutumia kifungu cha mkataba kinachowezesha kuvunja mkataba kama wanachama hawanufaiki na uendeshaji wa kiwanda,. Bodi ya MUVYULU ilimwita Mwenyekiti wa Kampuni ya Dhow Merchantile,Ndugu Yusuf Mulla tarehe 19/12/2007 ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ili kuzungumza na kutatua matatizo hasa ya kumalizia malipo ya mauzo ya 50% na kushirikishwa katika uendeshaji wa kiwanda.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa masikitiko makubwa Ndugu Mulla aliijibu Bodi kwamba, nanukuu " siwezi kuzungumza na mbwa bali nazungumza na mwenye mbwa!" na kwamba "hamwezi kufanya chochote kwa kuwa IKULU ni sebuleni kwangu".Mwisho wa kunukuu .
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa kuona dharau, kiburi na majigambo ya Ndugu Mulla, tarehe 24/07/2008 MUVYULU ilisitisha mkataba wa ubia wa kumiliki kiwanda cha Lupembe na Dhow Mercantile(EA) Ltd kwa kutumia taratibu na sheria za makubaliano ya awali. Dhow Merchantile walipewa siku saba(7) na Consolidated Holding Corporation (mrithi wa PSRC) kukabidhi kiwanda. Hata hivyo, Dhow Merchantile walikaidi amri hiyo. Wanachama wa MUVYULU walikifunga kiwanda ili kunusuru mali na rasilimali zake.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hadi sasa kiwanda kimeendelea kufungwa kwa kuwa Dhow Merchantile wamefungua kesi mahakamani inayohusu migogoro ya umiliki kati yao wenyewe na kuihusisha MUVYULU. Madhara ya kufunga kiwanda ni mengi na makubwa. Wananchi na wanachama wa MUVYULU wameendelea kuathirika kiuchumi, chai inaharibikia mashambani, kwa wale wanaouza kwenye viwanda vingine wanauza kwa bei ya chini sana, mara nyingine chai inaharibika kabla ya kufikishwa kiwandani kwa sababu ya umbali na serikali inaendelea kupoteza fedha za kigeni ambazo ni muhimu sana kwa ustawi wa uchumi wetu..Aidha uuzaji holela wa majani mabichi ya chai umesababisha kushuka kwa ubora wa chai ya Lupembe kwenye soko la dunia.[/FONT]

  [FONT=&quot]Wananchi na wanachama wa MUVYULU hawana kesi na Dhow Merchantile. Wao ndiyo waliovunja mkataba kwa ujeuri na kiburi chao. Wakulima wa chai wanasikitika jinsi wanavyoteseka na kuathirika kiuchumi na kimaendeleo kwa sababu ya kiburi cha mtu mmoja.Upo usemi unaosema "mwenye pesa si mwenzio". Pengine ni kwa sababu ya unyonge wa wakulima ndiyo maana hawajapata haki licha ya kuwa wabia wa kiwanda cha Lupembe.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]VITENDO VYA HUJUMA[/FONT]
  [FONT=&quot]Kesi aliyofungua Mulla mahakama kuu imekuwa ikihairishwa kila mara bila ya kusikilizwa, ambapo alipata hati batili ya mahakama ikionyesha kuwa ameshinda kesi ambayo anawaita wakulima kuwa ni wavamizi wa kiwanda chake. Baada ya kupata hati hiyo aliomba msaada wa kampuni ya Yono Action Mart tawi la Iringa wapeleke mabaunsa wao Lupembe kuondoa uongozi wa MUVYULU ndani ya kiwanda.[/FONT]

  [FONT=&quot]Yono kwa makubaliano na Mulla alitafuta mabaunsa wengi mjini Iringa na siku waliyokubaliana walipelekwa Lupembe kuondoa uongozi na kufungua kiwanda cha chai. Wakulima walipata habari za mpango mzima wa kuvamiwa kwa kiwanda chao. Wakulima nao walijipanga sawasawa kivita kukabiliana na mtu yeyote atakayeingia kwenye eneo la kiwanda.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mabaunsa wa Yono walifika kiwandani majira ya asubuhi askari wa mlangoni wa kiwanda akawafungulia lango kuu nao wakaingia ndani, walipofika karibu na ofisi, wakajitokeza kundi ndogo la wakulima na wakaanza kuwahoji, madhumuni ya ujio wao, wale mabaunsa waliwadharau sana wale Wabena kwa ufupi wao, na wakawa wanalazimisha kuingia ofisini kwa nguvu kuwaondoa watumishi waliokuwepo, mara lilijitokeza kundi kubwa ajabu la Wabena waliokuwa wamelala chini ya miti ya chai, na mapambano yakaanza, mabausa walizidiwa na hawakuweza kufanya lolote, ikabidi wasalimu amri.[/FONT]

  [FONT=&quot]Lupembe ni nchi ya baridi sana hasa nyakati za asubuhi, wale mabausa walivuliwa nguo, wakabaki na chupi peke yake, waliamriwa kurudi walikotoka wakirushwa kichura na kuchapwa bakora za nguvu hadi walipofikishwa nje kabisa ya kiwanda.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi cha Lupembe alipelekewa taarifa na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji ambao wote walikuwa upande wa Mulla, wakiwa bado wapo kituoni Wabena wakafika na watuhumiwa, mkuu wa kituo cha polisi alichukua funguo za jela ya mahabusu, wakaingia yeye na mwenyekiti wa kijiji na kujifungia, kwa sababu wanajua vita ya Wabena ilivyo, wakati huo wakawa wanaomba msaada wa kikosi cha polisi kutoka wilayani Njombe, lakini walijibiwa hakuna askari yeyote kituoni. Yupo mama mmoja aliona hali ilivyo mbaya, kwa ushawishi wake aliwasihi wananchi watulie, akawa anafanya mazungumzo na mkuu wa polisi aliyejifungia selo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Wananchi walitulizwa kwa kununulia bia na soda na wakawachia watuhumiwa, kisha wakatafutiwa gari lililowapeleka Njombe wakiwa mahututi kwa kipigo.[/FONT]

  [FONT=&quot]JARIBIO LA PILI[/FONT]
  [FONT=&quot]Mulla alifanya majadiliano na baadhi ya wakulima baada ya kuwapa vijisenti, kuwa atandaa maandamano na wakulima watabeba mabango, yanayolaani uongozi wa MUVYULU kwa kufunga kiwanda, kunakosababisha chai yao ikose sehemu ya kusindikia.[/FONT]

  [FONT=&quot]Aliwachukuwa wahandishi wa habari wa channel 10 ambao wangechukua picha na taarifa zote za tukio. Wabena walipata taarifa zote za mpango huo. Siku ya tukio Wabena wakaanza ndoria ya ulinzi tangu usiku, asubuhi zikafika gari mbili toka Njombe, na ndani walikuwepo waandishi wa habari wa channel 10. Walipofika eneo linaloitwa kibaoni magari yalisimamishwa na wananchi, na wakaanza kuhojiwa, walijitetea wamekuja kuchukua taarifa za matatizo ya wakulima baada ya kiwanda kufungwa. Walilazimishwa kufungua sehemu ya nyuma ya gari sehemu ya kuweka mizigo, na walipofungua yalikuwapo mabango mengi sana, yakiwalaumu viongozi wao.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hali ilibadilika ghafula, kijana mmoja subira ilimshinda, mkononi alikuwa ameshika mnyororo unaozungusha gurudumu la baiskeli, aliurusha kichwani mwa kijana mmoja aliyekuwa na kamera, mnyororo ulijizungusha kichwani mwake kisha akauvuta, ulimchana kichwa vibaya sana, walianza kukimbia kuelekea ndani ya kanisa lililokuwa karibu, huku wananchi wakitoa kipigo cha nguvu. Alikuwepo msamaria mwema na gari yake, aliendesha hadi karibu na kanisa wale vijana wakaingia haraka na kuondoka kwa speed kubwa hadi kituo kidogo cha polisi. Kufika pale wakakuta polisi wamefunga kituo na kutokomea kusikoeleweka.[/FONT]

  [FONT=&quot]Mulla ameingia makubaliano na Tanesco na ameshavuna miti ipatayo 1,000,000 kutoka ndani ya shamba la miti la kijiji yenye thamani ya shilingi bilioni nane (8,000,000,000/=)[/FONT]
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hivi Makinda na Jah people mko wapi? Hivi hawa si wapiga kura wenu? Mliapa kutetea na kulinda maslahi ya wapiga kura wenu huko kwenu Njombe,mbona kimya?
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Binafsi nimewahi kufuatilia huu mgogoro kati ya wakulima na kampuni ya Dhow Mechantile. Kwa taarifa inaonekana kulikuwa na uzembe mkubwa wa kusimamia vipengele vya mkataba tokea awali ambavyo ndio msingi wa haki na wajibu wa kila upande. Mulla na Kampuni yake ya Dhow Mechantile anaonekana kuwa na kiburi kwakuwa PSRC haikuwa na nguvu ya kumtaka atekeleze wajibu wake ikiwemo kulipa fedha zote za mauziano pamoja na kuruhusu umiliki wa hisa stahili kwa chama cha wakulima.Niliwahi kusikia pia kuna mgogoro mwingine unaohusu wakulima wa chai kule Rugwe kati ya wakulima kupitia chama chao na makampuni ya ununuzi wa chai. Nilisoma kupitia vyombo vya habari kuwa kampuni ya Mohammed Enterprises inayomiliki kampuni ya kununua chai ya G.D Estate iliyonunua baadhi ya mashamba ya chai, imeshindwa kufufua mashamba hayo kama ilivyopaswa kimkataba lakini mbaya zaidi imekuwa ikiwarubuni wakulima ambao wana mikataba ya kuuza chai kwa kampuni ya nyingine, kuvunja mikataba yao na kuingia kwenye mkataba na kampuni hiyo ambayo inadaiwa kununua chai bila kuwa na leseni wala vibali.kampuni hiyo inadaiwa kuvuruga kabisa ushindani huko Rungwe
   
Loading...