Muleba Kagera: Wananchi wenye hasira Wamuua na kumchoma moto Kikongwe, wamtuhumu kwa mauaji

Ni katika kijiji cha Kishanda. Bibi mmoja anaejulikana kama Makoleta, ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na kuchomwa moto pamoja na nyumba yake pia imechomwa.

Inadaiwa bibi huyo kamuua mtoto wa shule ya msingi alopotea ni siku ya 12 zilizopita.

Inadaiwa Mjukuu wa huyo bibi akiwa shuleni akawaambia wenzake kwamba yule mtoto anayetafutwa kwamba kapotea, yupo kwao bibi yake kamficha nyuma ya mlango

Inadaiwa Kijijini hapo tetesi za bibi huyo kuwa mchawi ni za miaka mingi.

Wananchi waliamua kuanza msako kwenye hiyo nyumba.

Inadaiwa walikuta mwili wa mtoto umezikwa kwenye shamba la huyo bibi na mtoto kashaanza kuoza lkn nguo alizopotea nazo zinaonekana bado

Ndipo walipochukua sheria mkononi. Bado tunasubiri taarifa kamili kutoka mwenye mamlaka husika kwani tukio linetokea jana jioni.
View attachment 1073853
======

Mtoto Ismail Hamis mweye umri wa miaka 7 aliyepotea tangu Aprili 5 mwaka huu akitokea shule, jana usiku amekutwa akiwa amefariki kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo

Tukio hilo lililotokea katika Kata ya Kishanda Wilayani Muleba limesababisha baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yake

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Revocatus Malimi amesema tangu kupotea kwa mtoto huyo hakuonekana tena hadi mwili wake ulipogundulika umefukiwa katika shamba la bibi huyo, ukiwa na sare zake za shule

Aidha, Kamanda Revocatus amesema taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika
Wamejuaje kama huyo kikongwe amehusika!!?? Jeshi la polisi likamate wauaji wa huyo bibi na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Napinga utekaji na mauaji ya watoto lakini makosa mawili hayasawazishi. Mambo ya kuchukua sheria mkononi yanapaswa kupingwa vikali na wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria. Utakuta watu hao waliomchoma huyo bibi ndio hao waliomuua huyo mtoto. Jeshi letu la Polisi likamate majitu makatili hayo ili sheria ichukue mkondo wake.
 
Sababu zamani ujinga ulitamalaki, wengi hawakujua lolote zaidi ya imani za kishenzi na story za kusadikika, ila ajabu Hadi leo wapo ambao wameendelea kushikwa akili na dini na hizi imani potofu. Unakuta mtu zama hizi tena graduate ila bado anaamini uchawi upo. Smdh

Wanaamini hivyo kwani dini zinawaaminisha hivyo.Wanadai kuwa biblia na misahafu inawataja wachawi.
 
Back
Top Bottom