Muleba Kagera: Wananchi wenye hasira Wamuua na kumchoma moto Kikongwe, wamtuhumu kwa mauaji

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Ni katika kijiji cha Kishanda. Bibi mmoja anaejulikana kama Makoleta, ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na kuchomwa moto pamoja na nyumba yake pia imechomwa.

Inadaiwa bibi huyo kamuua mtoto wa shule ya msingi alopotea ni siku ya 12 zilizopita.

Inadaiwa Mjukuu wa huyo bibi akiwa shuleni akawaambia wenzake kwamba yule mtoto anayetafutwa kwamba kapotea, yupo kwao bibi yake kamficha nyuma ya mlango

Inadaiwa Kijijini hapo tetesi za bibi huyo kuwa mchawi ni za miaka mingi.

Wananchi waliamua kuanza msako kwenye hiyo nyumba.

Inadaiwa walikuta mwili wa mtoto umezikwa kwenye shamba la huyo bibi na mtoto kashaanza kuoza lkn nguo alizopotea nazo zinaonekana bado

Ndipo walipochukua sheria mkononi. Bado tunasubiri taarifa kamili kutoka mwenye mamlaka husika kwani tukio linetokea jana jioni.
Screenshot_20190417-080236~2.png

======

Mtoto Ismail Hamis mweye umri wa miaka 7 aliyepotea tangu Aprili 5 mwaka huu akitokea shule, jana usiku amekutwa akiwa amefariki kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo

Tukio hilo lililotokea katika Kata ya Kishanda Wilayani Muleba limesababisha baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yake

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Revocatus Malimi amesema tangu kupotea kwa mtoto huyo hakuonekana tena hadi mwili wake ulipogundulika umefukiwa katika shamba la bibi huyo, ukiwa na sare zake za shule

Aidha, Kamanda Revocatus amesema taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika
 
Sababu zamani ujinga ulitamalaki, wengi hawakujua lolote zaidi ya imani za kishenzi na story za kusadikika, ila ajabu Hadi leo wapo ambao wameendelea kushikwa akili na dini na hizi imani potofu. Unakuta mtu zama hizi tena graduate ila bado anaamini uchawi upo. Smdh
Inatisha sana aisee.
Ila mie huwa najiuliza uchawi na uzee vina mahusiano gani?
Kwann idadi kubwa ya wachawi huwa ni vikongwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto Ismail Hamis mweye umri wa miaka 7 aliyepotea tangu Aprili 5 mwaka huu akitokea shule, jana usiku amekutwa akiwa amefariki kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo

Tukio hilo lililotokea katika Kata ya Kishanda Wilayani Muleba limesababisha baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yake

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Revocatus Malimi amesema tangu kupotea kwa mtoto huyo hakuonekana tena hadi mwili wake ulipogundulika umefukiwa katika shamba la bibi huyo, ukiwa na sare zake za shule

Aidha, Kamanda Revocatus amesema taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika
 
kuna watu wapuuzi kweli, je kama aliuwawa na watu wengine ila wakaona hapo ndo mahali salama pa kumficha!
inakuwaje wamemhukumu huyo bibi kisa tu shamba ni lake!
wananchi wamekuwa na hasira kali zinazoambatana na ujinga mwingi
 
hakuna chanini wlla nini, huyo bibi alicho kipata ni size yake kabisaa,
 
Mtoto Ismail Hamis mweye umri wa miaka 7 aliyepotea tangu Aprili 5 mwaka huu akitokea shule, jana usiku amekutwa akiwa amefariki kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo

Tukio hilo lililotokea katika Kata ya Kishanda Wilayani Muleba limesababisha baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yake

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Revocatus Malimi amesema tangu kupotea kwa mtoto huyo hakuonekana tena hadi mwili wake ulipogundulika umefukiwa katika shamba la bibi huyo, ukiwa na sare zake za shule

Aidha, Kamanda Revocatus amesema taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika

What if huyo mtoto aliuawa na watu wengine na siyo huyo bibi
 
nyie watoto wa wachawi achene utetezi wenu mbuzi, actual bila wananchi kufanya maamuzi magumu na ya kikatili vitendo vya utakaji na uuwaji watoto havita kuja kuisha, ancheni nzengo ifanye kazi yake kwa maana vyombo vya ulinzi vimeshindwa!
 
Rip bibi...
Kama ni kweli huna hatia watabeba laana ya machozi yako ulomwaga ukifa kifo cha maumivu.
Mungu akurehemu
 
nyie watoto wa wachawi achene utetezi wenu mbuzi, actual bila wananchi kufanya maamuzi magumu na ya kikatili vitendo vya utakaji na uuwaji watoto havita kuja kuisha, ancheni nzengo ifanye kazi yake kwa maana vyombo vya ulinzi vimeshindwa!

Yaelekea wewe nawe ni mshirika unayeweza kutoa ushahidi wa namna bibi alivyohusika na ni lazima uwe mshirikina
 
Back
Top Bottom