DOKEZO Muleba inanuka ufisadi, TARURA imeoza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Anaandika Mo Mlimwengu.

Muleba my mother land, Muleba ni nyumbani na Muleba ni mahali ambapo kitovu changu kilizikwa baada ya kuzaliwa. Wahenga wanasema ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni. Muleba punde si punde tena bali punde ni punde kila mtu kaona ni shamba la bibi. Aragobela akacholi aende.

Tukiwa wananchi tunalalamika na serikali inalalamika kwanini Kagera ni mkoa maskini. Kuna watu wameishakuwa visiki vya mpingo wanaifanya Muleba wanavyotaka. Hapa ndio nitaona kazi ya serikali ni nini? Hapa ndio nitamuona RC machachari Mh Chalamila akiwa mkali kwenye mali za umma.

Serikali imetoa taa za mitaani ili ziwashe mji ila Muleba watu wenye akili zaidi kwa kushirikiana na Tarura wametuwashia vibatari. What a joke? Hivi wanatuoanaje? basi msituheshimu sisi wananchi wa Muleba muheshimuni Rais wetu Dr Samia Suluhu Hassan anayehangaika usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanaifurahia nchi yao.

Hivi inakuweje mkandarasi baada ya kuleta zaa za kuwasha mji barabarani anatuleta taa za nyumbani i mean for domestic use. Taa ambazo zipo kwenye tender ni za Government project use.
Basi sawa ninaamini wote hatujui hesabu. Serikali kwenye tender imeibainisha tupate solar panel yenye volt 18 na watt 14o ambayo gharama yake ni usd dollar 500 kwa hela za kitanzania ni kama 1, 150,000/= tshs lakini mkandarasi kaenda kununua solar panel zenye volt 4.5 na watt 18 kwa bei ya usd dollar 23 ambapo kwa gharama ya tanzania ni taa za shilingi 53,820/= tshs . Hivi watu wanatuonaje na inasemekana serikali imetoa 2,500,000/= tsh kwa kila solar panel.

Hivi kwanini tukae kimya kwa hali hiii? Sitaacha kukemea huu uovu. Hao Tarura kazi yao ni nini? Ukipitia document zao unaona kabisa walitaka kitu kizuri na michoro ambayo iko detailed kuiwasha Muleba yetu. Je kwanini wao waidhinishe huu upuuzi uliofanywa na mkandarasi. Simlaumu mkandarasi nawalaumu Tarura ambao wamepewa idhini na serikali yetu kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa ila wameamua kwenda kinyume na maagizo ya serikali.

Muleba kuna nini? Kwanini mnafanya hivyo? Mkaidanganya serikali tena kwamba mmeweka taa kwa interval ya mita 60 ambapo kitaalamu inabidi kuanzia mita 45 lakini nyie mkafanya mita 30 kila baada ya nguzo. Na bado mnataka tukae kimya. Mimi Mlimwengu nikae kimya kwa huu uozo. Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na huu uozo unaofanyika ndani ya Muleba. Kukaa kimya kwangu itakuwa dhambi na kusema ndio itakuwa ahueni ya moyo wangu. Sauti ya chini inaniita inaniambia Mlimwengu usikae kimya, mlimwengu wanachezea hela za kodi za watanzania. Mlimwengu hawa watu wanatumia nguvu kubwa kumuharibia Rais wangu.

Muleba tujitafakari. How comes wilaya ambayo inaongoza kuingiza kwa mapato ndani ya mkoa inakuwa maskini. Mnaipohujumu Muleba mnatukosea wana Muleba.

#mulebatuitakayo
#mlimwengukasema
 
Anaandika Mo Mlimwengu.

Muleba my mother land, Muleba ni nyumbani na Muleba ni mahali ambapo kitovu changu kilizikwa baada ya kuzaliwa. Wahenga wanasema ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni. Muleba punde si punde tena bali punde ni punde kila mtu
Mtag Mama samiah ili afanyie kazi Jambo lako.
 
Huko ndio kuna sehemu wafugaji wakinyarwanda wanapaita Rwanda Ndogo?
 
Picha ingependeza kuleta uhalisia wa kinachoongelewa. Nashauri piga icha Taa zilizowekwa na zilizotarajiwa kuwekwa katika mradi husika. Najua uchungu wako lakin njia rahis ya kulisukuma hili ili waliojfanya wakubwaaa wapoteane.
 
Hua nikiangalia mabilioni yanayovunwa visiwa vya Muleba anzia kazi, Kibale, Bumbile, Mchangani, Kimoyomoyo na Mulumo, Lushonga, Kelebe, Goziba, Ghana, yaani watu wanapata maisha huko lakini wilaya ni wilaya ya ajabu, mna kahawa, ya kutosha lakini kwenye maendeleo Muleba imepitwa na wilaya ya Kasulu kwa waha. Yaani Muleba inahitaji miaka 20 kuwafikia Kasulu. Hua nasema Wahaya mnalaana ya asili.
 
Mna vanila inayouzwa kimagendo hadi Afrika Kusini lakini mpo mpo tu, mna magimbi ambayo huliwa Zanzibar hadi Comoro, mna maharage yanayoliwa Congo, mna udaga mweupe bora unaopendwa sokoni lakini bado Muleba haieleweki. Hapo hua nasema Wahaya mnalaana kabisa na hamjielewi.
 
Mnaitwaje maskini wakati mmekalia rasilimali za maana ambazo kuwavusha ni sekunde chache tu, leo wilaya kama Masasi, Mbinga, Kasulu ambazo zilikua level ya Muleba zimewapiga na kuwafikia. Hamuwezi tena, soko hamna, stand hamna, mpo mpo tu na ujinga wenu na kuchekacheka mara waitu na ujinga ujinga tu.
 
Picha ingependeza kuleta uhalisia wa kinachoongelewa. Nashauri piga icha Taa zilizowekwa na zilizotarajiwa kuwekwa katika mradi husika. Najua uchungu wako lakin njia rahis ya kulisukuma hili ili waliojfanya wakubwaaa wapoteane.
Hakuna sababu ya picha umeona kwanza halmashauri yao wengine wamejenga maghorofa wao wamejenga mfumo wa madarasa ndio makao makuu ya halmashauri yao yaani aibu tu
 
Mpaka hua najiuliza hawa wahaya wana akili sawasawa au ni wehu waliojikuta wanaishi tu muleba
 
Back
Top Bottom