Mukama, Lowassa wamchefua JK

Mukama, Lowassa wamchefua JK

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
MATAMSHI mazito yaliyotolewa wiki jana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, juu ya kuendeleza dhana ya kuwang'oa watuhumiwa wa ufisadi huku Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akitamba kushinda katika vita hiyo, yamemchefua Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Habari za uhakika zimebaini kuwa Rais Kikwete amesikitishwa na hali hiyo na inadaiwa kuwatumia ujumbe viongozi hao akitaka waache malumbano hayo kwa vile yalimalizwa kiustaarabu wakati wa vikao vya juu ya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma hivi karibuni.

Mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete amelithibitishia Tanzania Daima juu ya kutofurahishwa kwa Kikwete na malumbano hayo, ambayo amekiri kukiweka chama hicho katika mazingira magumu ya kufikia maamuzi yenye masilahi kwa chama.
"Ni kweli mwenyekiti amesikitishwa na matamshi ya Mukama na Lowassa, na ameagiza viongozi hao wakutane naye ili wazungumze juu ya hali hiyo," alisema mtoa habari huyo.

Taarifa za uhakika zimesema kuwa siku moja baada ya Lowassa kutamka maneno hayo huko Singida, viongozi wawili wa NEC, akiwamo waziri mmoja mwandamizi wakiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimpigia simu Mukama kumweleza kile alichosema mbunge huyo wa Monduli, na kumshauri atoe ufafanuzi kuhusiana kauli hiyo.

Novemba 27, mwaka huu, Lowassa akiwa mjini Singida alitoa matamshi mazito akidai kuwa siasa za Tanzania ni za ovyo ovyo na zinafanywa kwa lengo la kuwachafua watu akiwamo yeye.

Lowassa aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mjini Singida, alisema amekuwa akihusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi, ili asifikie malengo aliyojiwekea maishani, lakini anaamini kuwa atashinda kwa maombi ya viongozi wa dini.

Siku mbili baadaye, Novemba 29, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari kuwa vita ya kuwang'oa watuhumiwa wa ufisadi iliyopewa jina la kujivua gamba, iko pale pale na kwamba wanaozunguka nchi nzima wakijitangaza kusafishwa wanajisumbua.

Mukama katika maneno yanayodhihirisha kumlenga Lowassa, alisema kuwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma, wiki jana havikumsafisha mtu, badala yake viliamua watuhumiwa wa ufisadi washughulikiwe kwa kufuata taratibu na kanuni za chama.

"Kama kuna watu wanapitapita huko na kusema Kamati Kuu imewasafisha hiyo ni hulka yao…" alisema Mukama, kauli iliyochukuliwa na wachambuzi wa masuala ya siasa wanaofuatilia kwa makini matukio makubwa yanayotokea ndani ya CCM kwamba yalimlenga Lowassa ambaye ndiye kiongozi pekee wa chama hicho wa ngazi ya juu aliyekuwa katika ziara mikoani.

Mukama bila kutaja jina la mtu alisema viongozi wanaotakiwa kujiondoa wenyewe ndani ya siku tisini walizopewa awali, wanajulikana kwa vile jamii imekosa imani nao kutokana na aina ya matendo yao kiuongozi.

Akifafanua kauli hiyo, mtendaji huyo mkuu wa CCM alisema: "CCM imeonekana imehama kutoka kwa wanachama na kuwa ya matajiri. Katika siasa kuna kitu kinaitwa mtazamo wa kijamii na kipimo kimoja kinachotumika ni je, wenzako wanakuonaje? Kama katika watu 10, sita wanasena hufai kuwa kiongozi, unaitwa aliyekataliwa."
"Yupo ambaye hatajwi kwa chochote, si mazuri ama mabaya, hiyo inaitwa kutengwa na jamii, huyo pia hafai kuitwa kiongozi," alisema Mukama.

Mukama alisema NEC iliamua kukasimu madaraka yake na kuagiza kamati ya maadili ishughulikie watuhumiwa hao, na hatua zilizochukuliwa zitafikishwa katika vikao vya juu kwa maamuzi ya mwisho.
 
Mukama aache unafiki nakumbuka aliwahi kumpinga Nape wakati fulani kuwa hakutumwa na chama wala chama hakikutaja majina leo anasema mafisadi wanajulikana.
 
Viongozi aina ya Mukama,Nape,Membe watakiona cha moto 2015
 
[ Novemba 27, mwaka huu, Lowassa akiwa mjini Singida alitoa matamshi mazito akidai kuwa siasa za Tanzania ni za ovyo ovyo na zinafanywa kwa lengo la kuwachafua watu akiwamo yeye.

Siku mbili baadaye, Novemba 29, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari kuwa vita ya kuwang’oa watuhumiwa wa ufisadi iliyopewa jina la kujivua gamba, iko pale pale na kwamba wanaozunguka nchi nzima wakijitangaza kusafishwa wanajisumbua.

Mukama bila kutaja jina la mtu alisema viongozi wanaotakiwa kujiondoa wenyewe ndani ya siku tisini walizopewa awali, wanajulikana kwa vile jamii imekosa imani nao kutokana na aina ya matendo yao kiuongozi.

Huu mradi unaendeshwa KISAYANSI zaidi

Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe
 
Siasa uchwara (RA), siasa ovyo ovyo (EL), bado tutasikia mengi zaidi.
 
utafikiri hawa viongozi wa CCM ni mataahira, au wanahisi wanaongoza watu mataahira, au vyote kwa pamoja, kwamba wao viongozi wa CCM wanajijua kuwa ni mataahira na wanajua watu wanaowaongoza ni mataahira na vyama vinavyoshindana nayo (vyama vya upinzani) navyo ni mataahira.
 
utafikiri hawa viongozi wa CCM ni mataahira, au wanahisi wanaongoza watu mataahira, au vyote kwa pamoja, kwamba wao viongozi wa CCM wanajijua kuwa ni mataahira na wanajua watu wanaowaongoza ni mataahira na vyama vinavyoshindana nayo (vyama vya upinzani) navyo ni mataahira.
Na wewe uko group gani la mataahira.
 
Liandaliwe pambano la masumbwi kati ya lowasa na mukama wazichape apatikane mshindi then atakayepigwa afunge domo lake!!
 
wahariri wanatia huruma siku hizi, inawezekana hata wakilala na wake zao wanaona sura ya lowassa imelala pembeni inasubiri zamu

pambafffffffff
 
Ni heri kukaa kimya kuliko kujipambanua kuwa uko pamoja na Membe ambaye kila dalili kuwa ameshindwa kimkakati na sasa anategemea mbeleko ya Dr Dr Dr Dr Dr amsafishie njia. Viongozi wasio wabunifu kama JOKA LA MDIMU ambao wameshindwa hata kubuni mbinu zao za kujiingiza Ikulu tuwakatae kama ukoma kwani wakiingia ikulu hawataweza kubuni mbinu za kuliendeleza taifa, watabakia kulipana fadhila na kutubakisha katika hizi shida tulizonazo za Dr Dr Dr. Say no to Bernard Membe
 
Siasa za kuvuana magamba zimebaki kuwa uchwara kwani hata muasisi nashindwa kumuita ameasisi siasa uchwara kwa maana anashindwa kusimamia alichokiasisi!!!!
Na mwisho JK hana uwezo wa kumfukuza Lowasa, JK anakuwa kama mzazi ambaye mtoto akinyea kiganja huwezi sema utakikata kiganja hicho bali kukisafisha!!!
Na ndivyo ilivyo kinachofanyika saizi ni kumsafisha Lowassa indirect.
 
.......Mukama angekuwa anayasema haya huku jamii nayo ikimchukulia kuwa hana upande, lingekuwa jambo la busara, lakini kwa kufanya haya kwa manufaa ya Membe, yule nyoka wa mdimu, ni heri akae kimya, hsme on him..
 
Back
Top Bottom