Mukama amdanganya Kikwete kuhusu umiliki wa JF, wamiliki wa JF hawa hapa

Status
Not open for further replies.
He does not deserve any credit! He should have gone to school......no excuse!

Kwa anayoyafanya Kubenea, basi ni afdhari hakwenda shule (kama kweli hakwenda as you claim), kuliko kama angekwenda na kuishia kuwa kama waandishi wengine wauzao taaluma zao kupalilia mafisadi njia za mafanikio
 
Jesuit:ccm ikifa na Bakwata imekufa.sasa wamiliki wa jf wamewekwa hadharani natumai jk atasema wametumwa na baba zao walio ccm,kumbe laa ni suala la sisi dot.com kuamua kuupata utawala mpya wenye muelekeo wa maendeleo kwa wananchi wa tanzania.Mabadiliko ni muhimu katika maisha.sasa ni wakati wa kukipa ridhaa chama kingine
 
Tuna shukuru kwa kutujuza kumbe CDM wamevamia tu kwa kuhamasishwa na Slaa,ndio maana wako kwa staili ya Kuzomea hapa JF kila Thread wao wanaichukulia kichadema chadema tu! Useless!

Useless wewe au nani?hatujajua hapo una maanisha nini.
 
Jesuit,

Vipi Mkuu? Kubenea alitembeza ubabe wake kwa Mwanamke gani aliye karibu na wewe?

Naona unamchukia sana tu bila kuwa na ushahudi wowote.

Ukiona Mwanaume anabwabwaja ovyo basi ujuwe ni vitu vitatu tu: Sex, Power and Money.

Nafahamu kuwa Kubenea huwa kuna mambo anachemka na kuonekana kama Mpuuzi fulani hivi lakini huwa ana malengo yake. Mfano aliposema Mtanzania au Mwakalinga ni Mwanafunzi wakati jamaa kamaliza shule zaidi ya miaka 10 huko nyuma na kumwita KIJANA wakati jamaa kashavuta miaka 40.

Pamoja na mapungufu yake, huwezi kumwita MJINGA. Hii inaanza kunipa imani kabisa kuwa na wewe unaweza kuwa moja ya wale watu waliohusika kumwagia ACID/Tindikali na kisa KAWAMEGEA. Pole sana Mkuu kama ntakuwa nimekutonesha kidonda cha ..............

Hii habari ni nzuri sana. Kumbe Mtani wangu Malecela WIlliam ni Chadema la NGUVU? Ni Vuvuzela la Slaa kama wengine wanavyosema? Sasa hili TAWI la CCM hapo NY ni Chadema au CCM? Au yeye ni Kibaraka aliyetumwa na Slaa/CDM kuja kuivuruga CCM huko majuu?

Ukweli ni mmoja, Dr. Slaa kweli ni Vuvuzela na tangu ameanza kupiga honi (piii Piiii) CCM hawaelewani.....

Dr Slaa, umewashika pabaya, hebu ongeza LIST zaidi ili waanze kutoboana macho.
 
Mhh sina jibu, jibu ni hili hapa kutoka kwa W.Malecela,

"Mimi si mwanachama wa CHADEMA, mimi ni mwanachama mwaminifu wa CCM.
Na kwamba sasa yuko mbioni kufungua tawi la chama (CCM) mjini Washington D.C.

Tatizo la watu wa ccm hawataki kusoma, badala yake wanakuja na ripoti za kuokoteza mitaani, mimi ni mwanzilishi wa Jf, mimekuwa huko tangu 2006..." mwisho kunukuu.

Ni maneno ya William Malecela, moja ya wamiliki wa JF (mtoto wa John Malecela).

Ooookaaaay!
Sasa naanza kupata chanzo cha chokochoko ya ccm kuhusu JF, uwepo wa W. Malecela wanafikiri anatumiwa na kundi la baba yake kuishambulia ccm kama walivyojaribu kumziba mdomo Mama Anne Kilango.

Kweli mfa maji haishi kutapatapa badala ya kujibu kero au tuhuma zinazowekwa hadharani badala yake wanatafuta nani kasema wakimuona ndio mchawi wao.

Mie naona hiyo taarifa ya Mukama kwa jk imepotoshwa makusudi ili waonekane hawawajui wamiliki wa JF ili wapate cha kuwashambulia na isionekane ni siasa za visasi.

Kaaaazi kwelikweli!
 
JF Adminstrators mnaweza kuitolea ufafanuzi hii story..?? Kwasababu discussion ikiendelea hivi..upotoshaji utaendelea kuwa mkubwa.
 
Tuna shukuru kwa kutujuza kumbe CDM wamevamia tu kwa kuhamasishwa na Slaa,ndio maana wako kwa staili ya Kuzomea hapa JF kila Thread wao wanaichukulia kichadema chadema tu! Useless!

Hata wewe umevamia kama hujui kama ni haki yako kuingia na kuchangia mawazo. Wewe vp bana!
 
Tuna shukuru kwa kutujuza kumbe CDM wamevamia tu kwa kuhamasishwa na Slaa,ndio maana wako kwa staili ya Kuzomea hapa JF kila Thread wao wanaichukulia kichadema chadema tu! Useless!

wewe mwenyewe umevamia maana sijaona jina lako kwenye wamiliki! Ukidhani wenzako ni wajinga unawezajukuta wewe ni mpumbavu!
 
Hivi Kikwete naye jamani hawezi hata siku moja kuproove hivi vitu jamani? simple just one ring to Brela na atapata kila kitu, hahahahahahaha Kazoea huyo Kudanganywa na wanajua kabisa ni mvivu wa Kufuatilia mambo ndo maana humdanganya...Shame on You Mr Kiwete....
 
Ripoti ya Mukama kwemda kwa JK inautaja mtandao wa Jamii forum kuwa unaundwa na vijana kutoka CHADEMA.
Ripoti hiyo iliondaliwa na Wilson Mukama pamoja na Prof. Eginald Mihanjo wa St.Jones University -Dodoma.

Kwa mujibu wa Brela, JF inamilikiwa na Jamii Media Company namba. 66333.

Wanaomiliki wakiwa ni:
Steve Diallo (ndugu wa Anthony Diallo) hisa 40, Maxence Melo hisa 250, Mike Mushi hisa 250, Dickson Charles hisa 40, Lameck Mussa hisa 40, Mbaraka Islam (mwandishi wa habari) hisa 100 na William Malecela hisa 40, huyu ni mtoto wa John Malecela anayeishi washington -Marekan.

Ripoti ya mukama ndiyo inayotumiwa na JK kuwafukuza mafisadi El, RA na AC.

Source:
Mwananahalisi April 27. 2011

Si na wao waanzishe.
 
He does not deserve any credit! He should have gone to school......no excuse!

Samahani ndugu, labda mwenzetu uliyekwenda shule ili na sisi tupate lakuiga kutoka kwako kwa kukosa kwetu shule, ningeomba unijuze haya machache; je una mafanikio gani hapa duniani mpaka leo hii kumzidi kubenea ambaye hajakwenda shule, hiyo ni kuanzia pesa, ukurugenzi na umaarufu, ningependa unifafanulie hapo juu.
Pili ningependa unifahamishe katika usomi wako je umewahi kuvumbuwa nini? hii naamanisha yaani umewahi hata kuvumbuwa sindano?
Nitashukuru mr educated kama utaweza kunisaidia maswali yangu madogo ya kijinga lakini nitafurahi ukinijibu.
 
Mhh sina jibu, jibu ni hili hapa kutoka kwa W.Malecela,

"Mimi si mwanachama wa CHADEMA, mimi ni mwanachama mwaminifu wa CCM.
Na kwamba sasa yuko mbioni kufungua tawi la chama (CCM) mjini Washington D.C.

Tatizo la watu wa ccm hawataki kusoma, badala yake wanakuja na ripoti za kuokoteza mitaani, mimi ni mwanzilishi wa Jf, mimekuwa huko tangu 2006..." mwisho kunukuu.

Ni maneno ya William Malecela, moja ya wamiliki wa JF (mtoto wa John Malecela).
Wasiwasi wangu watasema Mzee Malecela anamtumia mtoto wake kuichafua CCM kupitia JF,hakika CCM wameshindwa kusoma ishara za nyakati,kwanini William aisiichafue CCM hapo nyuma wakati baba yake alipofanyiwa mtima nyongo aje leo ndio kupitia JF aanze kuichafua CCM,familia ya Mzee Malecela siamini kama wanaweza ichafua CCM,hao ni sawa na akina Makongoro,wamezaliwa na kukulia kwenye vyama vya TANU na CCM,wao sio watu wa kuja kwenye CCM
 
Ripoti ya Mukama kwemda kwa JK inautaja mtandao wa Jamii forum kuwa unaundwa na vijana kutoka CHADEMA.
Ripoti hiyo iliondaliwa na Wilson Mukama pamoja na Prof. Eginald Mihanjo wa St.Jones University -Dodoma.

Kwa mujibu wa Brela, JF inamilikiwa na Jamii Media Company namba. 66333.

Wanaomiliki wakiwa ni:
Steve Diallo (ndugu wa Anthony Diallo) hisa 40, Maxence Melo hisa 250, Mike Mushi hisa 250, Dickson Charles hisa 40, Lameck Mussa hisa 40, Mbaraka Islam (mwandishi wa habari) hisa 100 na William Malecela hisa 40, huyu ni mtoto wa John Malecela anayeishi washington -Marekan.

Ripoti ya mukama ndiyo inayotumiwa na JK kuwafukuza mafisadi El, RA na AC.

Source:
Mwananahalisi April 27. 2011


Kweli mwanahalisi kiboko, ila hapo kwenye RED ndio nimechoka kabisa. INVISIBLE tunakuomba jitokeze kutufafanulia hili sisi tukiwa kama member source yetu nzuri ya habari lazima iwe ni hapa hapa na sio nje ya hapa. PLEASE invisible do needfull.
 
hivi kwani wanaopost hizi post zetu humu jamvini ni OWNERS au ni sisi WANANCHI ambao tuna HASIRA?

Tungependa kupost kwenye MICHUZI BLOG pia, sema tukipost WANAZIFUTA...sasa sisi tufanyeje?....atleast hapa JF wanajitahidi kuwaachie watu wawe huru.

UKWELI ni kwamba si tunapost kwenye kila blog.....ila hizo nyingine zinachemsha kwa sababu wanafuta post zetu, sio kwa sababu ya OWNERS!
 
Chama cha Magamba mimi kwa kweli kinanikera sana na sirikali yake, Yani wao kuwaweka hadharani wamiliki wa makampuni Hewa yanayoliingizia taifa hasara hawawezi kutokana na wao kuwa washiriki, ila kuropoka vitu visivyolihusu taifa wala kuliingizia taifa hasara zaidi ya faida (kama kuwataja wamiliki wa JF) ndio wanaweza.

Me nadhani, nyoka kujivua gamba tu haitoshi maana anabakia nyoka yuleyule.

Kilichobaki ni kwamba nyoka ajivue nyama na damu yote mwilini ili afe na azaliwe chatu (Chadema) atakayelipeleka taifa hili katika nchi ya ahadi, maana kila kitu tunacho hatuna watenda kazi tu
 
Wadau: Naona Mukama kaingia kwa kasi ya ajabu ya uchovu wa kufikiri. Ameanza kazi kwa kuchukuwa maneno ya mitaani na kumpelekea bosi wake JK akisema eti ndiyo ripoti halisi!



Mukama amdanganya Kikwete


Ripoti ya "kikosi kazi" kilichoundwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete kutathmini uchaguzi mkuu uliopita, imejaa udanganyifu.

Kikozi kazi kiliongozwa na Wilson Mukama ambaye hivi sasa ni Katibu Mkuu wa CCM na Prpfesa Eginald Mihanjo wa Chuo Kikuu cha St Jones cha Dodoma.

MwanaHalisi limegundua kuwa miongoni mwa yaliyodanganywa ni kuhusu umiliki wa mtandao wa jamii Forums (JF).

Imeelezwa kwamba ripoti ya Mukama inautaja mtandao wa Jamii Forums kuwa unaundwa na vijana wa Chadema.

Lakini uchunguzi wa MwanaHalisi unaonyesha kuwa mtandao huo hauna uhusiano wowote na Chadema.

Kwa mujibu wa nyaraka kutoka BRELA, JF inamilikiwa na kampuni ya Jamii Media Company Limited iliyosajiliwa 2 Julai 2008 na kupata hati Na. 66333.

Wanahisa wa kampuni hiyo ni Steven Diallo mwenye hisa 40, Maxence Malo (hisa 250) Mike Mushi (hisa 250), Dickson Charles (hisa 40) na Lameck Mussa mwenye hisa 40.

Wanahisa wengine ni mwandishi wa habari Mbaraka Islam mwenye hisa 100 na William Malecela, mwenye hisa 40. Yeye ni motto wa Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela.

Steve Diallo ni ndugu ya mjumbe wa CCM-NEC na mbunge wa zamani wa Ilemela (CCM), Anthony Diallo.

Rais Kikwete aliunda kikosi kazi muda mfupi baada ya kutoa hotuba ya kuadhimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM mjini Dodoma. Kikosi kilipewa jukumu la kufanya utafiti juu ya mambo ambayo yalisababisha CCM ishindwe kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliopita………

………………………..katika taarifa yake Mukama alisema vijana haoi (wamiliki wa Chadema) wanafanya kazi hatarishi "kwa chama chetu na serikali yake kwa kutoa taarifa nyingi za upotoshajio ambazo zinasomwa na watu wengi sana duniani, hasa vijana."………………………….

………….Gazeti hili lilpmtafuta Malecela anayeishi Washington, Marekani, kujua iwapo ni mwanachama wa Chadema alisema "Si kweli hata kidogo."

Alisema yeye ni mwanachama mwaminifu wa CCM na kwamba hivi sasa yuko mbioni kufungua tawi la CCM mjini Washington.

Alisema "Tatizo la watu wa CCM hawataki kusoma, badala yake wanakuja na ripoti za kuokoteza mitaani. Mimi ni mwanzilishi wa JF, nimekuwa huko tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006."

Kwa upande wake Maxence Melo anasema wakati mtandao huo unaanzishgwa mwaka 2006 kabla ya kuandikishwa 2008, kulikuwa na watu wengi sana, wakiwewmo vigogo wa CCM.

Anasewma miongoni mwa wanachama wa mtandao huo ni Nape Nauye, Hussein Bashe, na Khamis Kigangwalla.

Anasema mbali na wanachama hao wanaofahamika kwa majina yao wapo wanachama na viongozi wengi wa CCM wanaotumia majina ya bandia.

Naye Islam, mkurugenzi mwingine wa kampuni hiyo anasema "Hawa watu wameshindwa hata kwenda BRELA kutafuta nyaraka. Hayo yote yaliyosemwa na CCM hayana ukweli hata kidogo. Juio ni uchovu wa kufikiri………………….."

Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo.
 
Swali ni moja mbona nguvu kubwa sana inatumika kukana kumilikiwa na CDM? Kwani CDM ni tusi? Shame Kubenea leo anatuambia ukweli kuhusu JF unapatikana kwenye makaratasi ya BRELA huku akiendelea kumbana Rostam kuwa ni mmiliki wa Dowans wakati makaratasi hayo ya BRELA hayana jina la Rostam, sijui hii ni triple standard au ni kupenda kutumia ujinga wa wana JF.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom