Mukama amdanganya Kikwete kuhusu umiliki wa JF, wamiliki wa JF hawa hapa

Status
Not open for further replies.
NIMUONAVYO HUYU MALECELA MDOGO WA HUKO UGHAIBUNI NEW YORK

Nilikua namfuatilia vizuri sana tena kwa karibu mno huyu kijana mwenzetu Malecela Mdogo na nimegundua mambo yafuatayoa kwamba;

1. Ni Mtu wa kujishusha ajabu

(kila siku navutiwa na michango yake humu na hata kukiri kwake sawa tu MM Mwanakijiji hata kama kuna kutofautiana lakini kamwe hakuwahi kuonyesha upepo wa kuwa mmojawapo wamiliki wa JF.

2. Ni Mtu Mwenye Fikra Huru

Kila sentensi aitoayo wala haonyeshekusimamia saana mambo yapindishwe vipi ili huyu na au yule apate kufurahika. Anachoonyesha yeye ni kule kuruhusu FACTS zikajisimamie na kujieleza zenyewe tu hata kama Mwana-CCM na au Mwana-CHADEMA atanuna - brutally a liberal mind.

3. Uwezo wa Kujieleza ni ule wa Baba Yake

Ingawaje mimi ni miongoni mwa watu wengi sana tu JF niliyempinga sana Dada yake huyu bwana kupewa uteuzi ule na hata sasa bado napinga hilo, ila katika huyu bwana kwa muda mrefu ambayo nimepata kumfahamu nayo hapa JF nadhani ni rahisi mno kusamehewa nikisema kwamba kuna uwezekano mkubwa kajizaa mwenyewe Mzee Katapila mwenyewe kwa picha na ujana wa huyu kijana mwenzetu.

Wakati fulani mzee mmoja aliwahi kunichekesha saaaana kwamba katika taifa letu hili la Tanzania kuna watu wawili tu ambao hata kama ulikua umekasirika kuliko mnyama simba na hata kujichagulia kubeba mawe ukamponde nayo pindi atakapokuja kuwahutubieni wa watu mtajikuta mawe yakidondoka yenyewe tu PINDI TU MTAKAPOMPA JAPO KIJINAFASI KUJIELEZA - aliwataja watu hawa kuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na John Samuel Malecela.

4. Uwezo wa Kujikosoa na hata Kukosoa Kile Anachokipenda

Jaama eeehhh, ni lazima tukubali kwamba moyo wa binadamu siku zote haiko neutral katika swala lolote lile; ni kule ama kupenda au kuchukia tu. Na watu tunapendelea kuponda tunachokichukia na kulilamba lamba lile tunalolipenda. Lakini ahuyu ndugu pamoja na Mwanakijiji ni wale watu nadra wenye kuweza kuponda anachokipenda na kulamba anachokichukia alimradi mantiki na ukweli wa mambo unaelekeza hivyo.

Lakini yooote juu ya yooote Bwana Malecela Junior, wewe kwa kila rangi uipendayo ni mpenda haki na kwa bahati mbaya saaaana ni miaka mingi sana tangu haki kugeuka bidhaa hadimu inayouzwa na CCM tu kwa majonzi makubwa sana ya walalahoi.

Hivyo, hebu tafakari taratibu kama kweli hautoonekana A SQUARE PEG IN A ROUND HOLE kuendeleza harakati zako kwa kugonga Mlango CCM Ukuta usiosikiliza cha mtu???

Hebu usirudie kosa la kuwa Katapilla kutengenezea watu barabara ya ulaji wao binafsi ndani ya CCM huku vijana wenzako tukifa njaa bila ya wa kutukaribisha karamuni kwa kuwa si watoto wa wakubwa.

Njoo CHADEMA leo; chama ambacho hata wamachinga tu au wakulima wakisimama kusema husikilizwa kwa heshima zote mpaka kituo na bila kuingiziwa maneno ya kinafiki ambayo yamekua kama utamaduni wa CCM kama vile - 'yanazungumzika' kumbe wanamaanisha tu kwamba wewe chokambaya hujui waliko watu wa aina yako.

Hata hivyo pamoja na mimi kukupa shime hapa wala isichukuliwe kwamba sitoweza kutofautiana na wewe ki-mjadala pale panapobidi. Kheri!!

William kutokana na haya maelezo yako uliyoyatoa hapa baada ya kumjibu sikonge , haihitaji mtu kuwa na PHD kujua upeo wako, wewe jamaa nakupa big up sana , haya maelezo yamejitosheleza na ushauri mzuri sana umewapa hawa CCM sasa hivi naona wamepoteana njia huku wakiwa wamesahau kuwa ulishawapa taarifa kama hii, lakini ndugu yangu wewe hujui kuwa wafuasi wengi wa ccm ni wale wenzangu na mimi wa ndio mzee? % kubwa ya wafuasi wao wapo vijijini, na huo ndio mtaji wao, na hizi shule za kata zinazoibukia ndio kifo chao believe me, nakuhakikishia itafika wakati chama chenu kitapotea kabisaaa kwa sababu kila anayeelimika anakimbia ,na anayebaki ndani ya ccm ujue ana maslahi fulani(hapa sikuongelei wewe) nawaongelea vijana wengi ambao ndio wameajiriwa tu na sasa hivi wanatumia masaa manne au matano kwenda kazini kutokana na foleni,sasa huyu kijana utamwambia aje hapa JF kuitetea ccm akuelewe? kama mimi nikija hapa kuipigia debe then jioni nikiondoka kwenda nyumbani nakaa barabarani kwa mda wa masaa 4 na joto zaidi ya nyuzi 30 , mimi si nitakuwa taahira? kwa hiyo ndugu yangu ccm huu moto wameuwasha wenyewe na jinsi tunavyozidi kwenda mbele na jinsi vijana wengi wanavyozidi kupata elimu ndio ccm nayo itazidi kupotea na kudidimia , kinachotakiwa ni kuwasikiliza wananchi from the botom thats all, na kuwawajibisha watu thats all, mtu akifanya masikhara kazini anapigwa chini ,thats all
 
He does not deserve any credit! He should have gone to school......no excuse!

Oh... so u want to tell us that the guy has never been to school?! if that is true then he deserves more credit!!! maana angeenda shule basi pasingetosha, kwani angalau anathubutu! he might be one but to the TZans he is a million!
 
NIMUONAVYO HUYU MALECELA MDOGO WA HUKO UGHAIBUNI NEW YORK

Nilikua namfuatilia vizuri sana tena kwa karibu mno huyu kijana mwenzetu Malecela Mdogo na nimegundua mambo yafuatayoa kwamba;

1. Ni Mtu wa kujishusha ajabu

(kila siku navutiwa na michango yake humu na hata kukiri kwake sawa tu MM Mwanakijiji hata kama kuna kutofautiana lakini kamwe hakuwahi kuonyesha upepo wa kuwa mmojawapo wamiliki wa JF.

2. Ni Mtu Mwenye Fikra Huru

Kila sentensi aitoayo wala haonyeshekusimamia saana mambo yapindishwe vipi ili huyu na au yule apate kufurahika. Anachoonyesha yeye ni kule kuruhusu FACTS zikajisimamie na kujieleza zenyewe tu hata kama Mwana-CCM na au Mwana-CHADEMA atanuna - brutally a liberal mind.

3. Uwezo wa Kujieleza ni ule wa Baba Yake

Ingawaje mimi ni miongoni mwa watu wengi sana tu JF niliyempinga sana Dada yake huyu bwana kupewa uteuzi ule na hata sasa bado napinga hilo, ila katika huyu bwana kwa muda mrefu ambayo nimepata kumfahamu nayo hapa JF nadhani ni rahisi mno kusamehewa nikisema kwamba kuna uwezekano mkubwa Mzee Katapila mwenyewe kwa picha na ujana wa huyu mwenzetu.

Wakati fulani mzee mmoja aliwahi kunichekesha saaaana kwamba katika taifa letu hili la Tanzania kuna watu wawili tu ambao hata kama ulikua umekasirika kuliko mnyama simba na hata kujichagulia kubeba mawe ukamponde nayo pindi atakapokuja kuwahutubieni wa watu mtajikuta mawe yakidondoka yenyewe tu PINDI TU MTAKAPOMPA JAPO KIJINAFASI KUJIELEZA - aliwataja watu hawa kuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na John Samuel Malecela.

4. Uwezo wa Kujikosoa na hata Kukosoa Kile Anachokipenda

Jaama eeehhh, ni lazima tukubali kwamba moyo wa binadamu siku zote haiko neutral katika swala lolote lile; ni kule ama kupenda au kuchukia tu. Na watu tunapendelea kuponda tunachokichukia na kulilamba lamba lile tunalolipenda. Lakini ahuyu ndugu pamoja na Mwanakijiji ni wale watu nadra wenye kuweza kuponda anachokipenda na kulamba anachokichukia alimradi mantiki na ukweli wa mambo unaelekeza hivyo.

Lakini yooote juu ya yooote Bwana Malecela Junior, wewe kwa kila rangi uipendayo ni mpenda haki na kwa bahati mbaya saaaana ni miaka mingi sana tangu haki kugeuka bidhaa hadimu inayouzwa na CCM tu kwa majonzi makubwa sana ya walalahoi.

Hivyo, hebu tafakari taratibu kama kweli hautoonekana A SQUARE PEG IN A ROUND HOLE kuendeleza harakati zako kwa kugonga Mlango CCM Ukuta usiosikiliza cha mtu???

Hebu usirudie kosa la kuwa Katapilla kutengenezea watu barabara ya ulaji wao binafsi ndani ya CCM huku vijana wenzako tukifa njaa bila ya wa kutukaribisha karamuni kwa kuwa si watoto wa wakubwa.

Njoo CHADEMA leo; chama ambacho hata wamachinga tu au wakulima wakisimama kusema husikilizwa kwa heshima zote mpaka kituo na bila kuingiziwa maneno ya kinafiki ambayo yamekua kama utamaduni wa CCM kama vile - 'yanazungumzika' kumbe wanamaanisha tu kwamba wewe chokambaya hujui waliko watu wa aina yako.

Hata hivyo pamoja na mimi kukupa shime hapa wala isichukuliwe kwamba sitoweza kutofautiana na wewe ki-mjadala pale panapobidi. Kheri!!

- Ushauri mzito sana ndugu yangu nimeusikia sana, otherwise ahsante sana kwa maneno yako ya kutia moyo sana, ingawa mimi sijazoea sana nimezoea mawe! ha! ah! ha!, MUCH RESPECT MKUU SANA!

William @ NYC, USA.
 
Oh... so u want to tell us that the guy has never been to school?! if that is true then he deserves more credit!!! maana angeenda shule basi pasingetosha, kwani angalau anathubutu! he might be one but to the TZans he is a million!

- Wa-Tanzania siku zote tunatakiwa kumuheshimu sana Saeed Kubenea, I mean kutofautiana naye kihoja sawa ndio Demokrasia, lakini kumshusha hadhi sio sawa the man anajitahidi sana kwenda avenue zisizofikika, mpaka amemwagiwa Tindikali usoni, can you imagine ungekua ni wewe umemwagiwa, ungethubutu kuandika tena habari za uozo wa serikali kama anavyofanya baada ya kupona?

- I mean mpeni heshima japo kidogo kwa sababu Saeed anafanya ambayo sisi wengine hatuwezi, na anafanya kwa sababu ya taifa wala sio pesa, I know Saeed, sometimes tunapokwenda bongo tuwe tunawatafuta hawa watu na kuongea nao ili tuwajue wenyewe badala ya kuendelea kuwasikia kwa wengine tu na kwenye magazeti na hivyo kuishia kutoa hukumu zisizo wahusu kabisaa!!

- Much Respect!

William @ NYC, USA.
 
- Ahsante sana ndugu yangu, I mean wewe tunatoka mbaali sana na this game, na ninakuheshimu sana na samahani sana kama sikukuelewa niwie radhi sana, otherwise I mean Media waliponipigia simu majuzi they were very upfront kwamba waliowatuma kunipigia wamewaambia in advance kwamba kwangu watapa ukweli mtupu, and I did na kuwambia ukweli mtupu kama kawaida yangu hapa JF. Well, sikuitaka sana hii bragging right ya umiliiki wa hapa kuwa in public, lakini ninaamini kwenye maisha kila kitu hutokea kwa sababu, rohoni nina amani sana kuona utabiri wangu umekua kama nilivyotabiri 2005, nilimwambia wazi Waziri Sophia Simba kwamba kama CCM hawakuja hapa mapema, siku moja huuu mtandao utawatesa sana na watalia kama watoto wadogo, exactly what is happening now! and I am proud of that!
- Sasa cha muhimu ni sisi wote wananchi washiriki wa huu mtandao, kuulinda kwa nguvu zetu zote ili usiharibiwe na wapuuzi wachache ambao sio siri naona wamekua wengi sana siku hizi, tuwaelimishe ili waondokane na siasa za utumwa na again jamani tuuulinde sana huu matandao maana sasa umekua ni tatizo sana kwa watawala wetu wasiotaka kubadilika na wakati!

Mungu Aibariki Tanzania na Aibariki JF!

William @ NYC, USA.

Big up William!!!!! wewe ni mtu mkweli mno! yaani huna magamba wala manyoya!
 
Nami nisaidieni Eeh!! Niko bush (nchi yaTanganyika original) huku karibu na Burundi!! Mie mgeni jamvini!! Hivi kwani JF ilianzishwa ili imchachafye mwenyekiti wao wa ccm, na serikali yao tu? Mbona wanaipigia kelele Jf? Nadhani kila anaye jiunga humu anatarajiwa kuwa G. Thinker. Sasa hawa tulio logeka akili zetu na limwenge tumetoka wapi? Munisayidie! Ebhaga!!! Niko mwisho wa reli.
 
Hapo kaka Will nimekuelewa. Kweli mtandao umevamiwa! Kuna watu humu JF wameingia kwa fujo, na akili zao mgando. Tena wengi ni baada ya ati magamba kuvuliwa. Nawengine eti ni watumishi wa Mungu!! Sijui Mungu yupi!! Jf idumu daima.
 
Evi Mkama na hao ma-dr hawkujui BRELA? Mbona mjinga kama Kubenea anakujua?<br />
Mi naona haya ni kama ya kagoda, majina ya BRELA yanaweza yasiwe yanataja mmiliki halisi!
<br />

Kiumbe Mzito kama wewe unapata wapi Ujasiri wa kumtukana Kubenea?
Kubenea ni Mmoja kati ya Watz wazalendo na Majasiri na amefanya kazi nzuri katika Vita dhidi ya Ufisadi,Wewe unayejihesabu Mwerevu Umelifanyia nn Taifa Hili? Cocroach!!!
<br />
 
Samahani ndugu, labda mwenzetu uliyekwenda shule ili na sisi tupate lakuiga kutoka kwako kwa kukosa kwetu shule, ningeomba unijuze haya machache; je una mafanikio gani hapa duniani mpaka leo hii kumzidi kubenea ambaye hajakwenda shule, hiyo ni kuanzia pesa, ukurugenzi na umaarufu, ningependa unifafanulie hapo juu.<br />
Pili ningependa unifahamishe katika usomi wako je umewahi kuvumbuwa nini? hii naamanisha yaani umewahi hata kuvumbuwa sindano?<br />
Nitashukuru mr educated kama utaweza kunisaidia maswali yangu madogo ya kijinga lakini nitafurahi ukinijibu.
<br />
<br />

Matola,Achana nako hako kajamaa kanachoitwa Jesuit,kamejaa husuda na kenyewe ndiyo kapumbavu,Hv wewe Jesuit,Unapimaje Kiwango cha Elimu ambacho anacho kwa kuangalia Cheti? Kwa kuangalia wingi wa Page za Cv ya muhusika?
Unajua hata kama unachuki binafsi na Mtu kwa sababu za Kimaisha,ni busara kuhesabu maneno yako na kuyatafakari kabla hujasema,ona sasa,maneno yako yamekuacha Uchi!!

Kila Mtu anajua Umuhimu wa Mtu kwenda Shule,lakini ni Muhimu zaidi uwezo wa mtu kutumia Elimu yake kuboresha maisha yake na ya Jamii inayomzunguka!
Eg,Itatusaidia nini Ukiwa na Phd halafu ipo kwenye cheti tu wakati kichwani haipo,zitabaki Mbwembwe tu,mm nimesoma,Mimi Nimesoma!
In essence,JESUIT if u are really educated,u wont need to tell people,It will be obvious kupitia Maneno yako na Kazi zako za Mikono!
Ukiona ww unalazimika kuwaambia watu kama Umesoma na kwamba hawajui mpaka Useme ujue Ulienda shule na ukajibu maswali ya Mitihani lakini HAUJAELIMIKA!!

Mnazareti alisema "Kama haumniamini Mimi,Ziaminini KAZI zangu"

Kila Mtu asiye na hila anajua Kazi za Kubenea,kila Jumatano,tunaziona kazi zake,huthubutu kufika pale ambapo wengi hatufiki,kalamu yake Haipindishi kumpendeza Bwana Mkubwa,Huyu ndiye Msomi wa Kweli coz Elimu inapasa Kumkomboa mtu,kumfanya mtu awe Huru!!
Hao waliopata Elimu safi mbona wanafyata Mkia? Kubenea,on ths ground,is one of the most educated men in the world!!
NI jABALI,KIPANDE CHA MWANAUME,JASIRI MNO,MPAMBANAJI,MZALENDO!!
Kama umetumwa,waambie Kubenea Heshima yake Ipo Juu na Kazi yake iliyotukuka imepigwa Muhuri ndani ya Mioyo yetu cc Watz Wazalendo!!

I revere you Saed Kubenea,U are a true son of the land,endelea kuandika brother,Kazi Yako Imetukuka!!

Wewe Jesuit endelea na Vyeti vyako na MAJIVUNO yako,Uncircumcised Baboon!!
 
Katika kutoka kote, ndio katibu mkuu mpya anatoka hivyo? Its another Makamba in the making............
 
Nami nisaidieni Eeh!! Niko bush (nchi yaTanganyika original) huku karibu na Burundi!! Mie mgeni jamvini!! Hivi kwani JF ilianzishwa ili imchachafye mwenyekiti wao wa ccm, na serikali yao tu? Mbona wanaipigia kelele Jf? Nadhani kila anaye jiunga humu anatarajiwa kuwa G. Thinker. Sasa hawa tulio logeka akili zetu na limwenge tumetoka wapi? Munisayidie! Ebhaga!!! Niko mwisho wa reli.

Wewe wakike au wakiume?
Ahahahahaaa!! kitabu......mi hua nafunuafunua tu bhana.
 
tuna mwendo mrefu sana na watu wa "intelijensia"
ovyo kabisa
 
Tuna shukuru kwa kutujuza kumbe CDM wamevamia tu kwa kuhamasishwa na Slaa,ndio maana wako kwa staili ya Kuzomea hapa JF kila Thread wao wanaichukulia kichadema chadema tu! Useless!

wakati cdm wanavamia mlikuwa wapi? Kwa akili yako unadhani Slaa anaamasisha watu kuingia JF? Sijapata kumsikia hata siku moja. Mwisho mtasema hata wachangia mada kwenye radio& TV ni Cdm.
 
Hivi hakuna topic ya kukinenepesha chama chetu CHADEMA? kila saa ooh ccm hivi mara vile tuzungumzie challenges tulizonazo kwenye chama na nmna ya kuzimeet tuachane na vyama vingine. Mwishoni tutaonekana majuha. Swala la nani anamiliki jf halina msingi la msingi je chadema tunatumiaje social media kukiweka sawa chama chetu na nchi yetu kwa ujumla. Mbona hatuulizi wanaowekaeza wanapata faida gani kiuchumi au wanapata fund kutoka kutoka wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom