Mukama alia: Tutawaondoa tu mafisadi, hatuogopi

Mwisho wakila kiongoz mlafi na mwenyekupenda kujilimbikizia mali unakuja! Napata faraja na furaha kubwa kuujulisha umma wa Tanzania, kila Tsh1 iliyo ibiwa, ambayo nikodi ya watanzania lazima irudi. Mungu anaenda kufanya mambo makubwa kwa watanzania, anaenda kuinua viongoz watakao enda kuwatetea watanzania na sio matumbo yao. Mungu anaenda kufichua maovu yakila kiongozi alie itafuna Kodi ya watanzania. Mchakato umeanza na unaenda kwa kasi kubwa sana, Rais wetu mpendwa Kikwete Mungu kampiga upofu mkubwa na Mungu kamuachilia viongoz wasio ona ili wamshauri ujinga akapate kupotea, Umma wawa Tanzania lazima ujuwe huu nimpango Mungu aliuwandaa yapata miaka 100 kabla ya Uhuru wa taifa hili. Na hata wale wanapenda kumsikiliza Hayati baba wa Taifa Nyerere basi alikwisha kutabiri na sasa niwakati Mungu kwenda kuwajibu kila mlanguzi na muhujumu wa Taifa hili Postvly. Bila mpango kutimia kunahati hati kubwa ya Nchi hii kupigana vita. Watanzania mtaenda kushuhudia viongozi wawili wakubwa sana sana wakienda kupanda kizimbani nakujibu mashitaka yaupoteaji wa Trilions of money kwa kuruhusu Tax free kwa makampuni makubwa. Mungu anaenda kufanya muujiza mkubwa sana, Tayari Rais wa nchi hii amekwisha kuandaliwa, napenda kusema sio Lowasa,sio Chenge, sio Rose Migiro japo Rose ndie atakaye tumiwa kama upofu kwa viongoz wa juu ilikumuinua Rais wa kweli atakaye tengeneza mpango wa miaka 50 ijayo, Mungu anaenda kumuinua Rais wa ukweli atakaye rudisha thaman ya utu wa Mtanzania tangu kijijin mpaka mjini. Sii kamati kuu wala tumeyauchaguzi itamzuwia Rais huyu kuwa Rais, Mungu anaenda kurudisha thaman ya mtanzania maana KILIO CHA WATANZANIA KIMEMFIKIA MUNGU NAYEYE AMESHUKA KUTUOKOA. Asante Baba kwakujibu Maombi.
NOTE:Ukisoma posti hiyo jitahidi uisome kama wale wahubiri wanaohubiri kwa kelele na mzuka kisha utaona utamu wa alichokiandika jamaa
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo. Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

“Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi. Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo,” alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao. Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania. Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine. Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi na kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa. Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao. Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.

HabariLeo | Mukama-Mafisadi CCM lazima wavue gamba
 
Kufukuza au kutofukuza kunategemea maamuzi ya vikao vya chama kwa ngazi ya juu amekili Katibu Mkuu wa CCM. Mukama anakili pia ubadhilifu,na maozo mbali mbali ndami ya CCM yake. Baadhi ya watuhumiwa ufisadi niwajumbe kwenye maamuzi ya vikao ngazi za juu na wana nguvu za uwashawishi kwawajumbe wenzao. Bw Mukama na Nape watawaambia nini wananchi? Usitegemee miujiza watuhumiwa ndio waamuzi.
 
Mtaishia kupiga makelel tu humu ndani na unafki mwingi,CCM wanaona mbali sana,nyie mnadhani mabadiliko ni lazima yatoke huko mliko la hasha,ajenda yenu kubwa humu ndani ni unafki mtupu juu ya CCM,badala ya kutoa mawazo mbadala ya kuijenga CHADEMA ijiandae kuchukua dola nyie mmekaa kufanya unafki kama mademu wa maisha club wanaosubiri mabwana................I HATE YOU GUYS COZ KILA SIKU MAMBO YENU NI YALEYELE KULAUMU TU,AFU ASILIMIA KUBWA HUMU NI MACHALII,RUDINI MKALIME NDIZI MAKWENU....................GUYS SEEMS LIKE GAYS.
 
KAMA wanavyosisitiza mkama na nape kuwa mapacha lazima waondoke au waondolewe
Then inamaanisha kuwa lowassa akijiondoa au akafuuzwa ndani ya chama inakuwa amepoteza haki ya kuendelea kupata mafao kama waziri mkuu mstaafu.
je hapo inakuwaje wanajamvi??????????????????????????????????????????????????????????????????????????

hapo kwenye Red...ukome kabisa!! mstaafu!!??? kastaafia wapi??? chooni kwako??? EL ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa manufaa ya umma!!!
 
Nape alizunguka nchi nzima hadi Mwenyekiti wake alipochimbwa Biti mbele ya kikao cha NEC

Gumzo mjini ni utapeli na mazishi ya Chadema hata ufanyeje Ben kuibua topic hii haiwezi kufuta msiba unaowakabili mbele yenu.

Katika Uzi mmoja umeapia Kula na wanaosema ukweli sahani moja lakini nakuhakikishia kuwa huwezi na umechelewa Moto umeishaunguza maini.
Tafuteni kabati la kutunza hayo mafaili.
 
hata mh. Wasira aliota ndoto hii sikunyingi sana lakni haikutimia, kusubiria kifo cha cdm nisawa na mtu anayesubiri maji yapande mlima, utasubiri sana.
 
Mkama amedai lazima ataongoza jukumu la kuwaondoa mafisadi wanaotuhumiwa na chama chake, japo anasema mafisadi hao ni lafiki zake wa karibu! Eti watazuia matajiri kujipenyeza tena ktk chama. Amewabeza wanaosema anawaogopa mafisadi kwa kumaka"not me, never!". Lakini amekiri kubebeshwa mzigo mzito! Hapa alikuwa akiongea na magamba wadogo chuo kikuu Mzumbe.
ource: TBC
jee, ataweza?

Mnataka kunipa barua ya nini? Kwani wewe hujui nini kuhusu Richmond?
Lowasa akimchimba mkwara Kikwete!
Tokea atoe tamko hilo, ni zaidi ya miaka miwili sasa, aliondoka kwenye hiyo ofisi ya ukatibu mkuu, akiwa amesurrender, kwa kushindwa kuwang'oa hao mafisadi.

Ukweli ambao uko dhahiri ni kuwa ufisadi/rushwa na CCM, ni sawasawa na uhusiano wa uji na mgonjwa, pale unapoamua tu kumnyima uji mgonjwa, hapo utakuwa umetangaza rasmi kuyaondoa maisha ya huyo mgonjwa.

Vivyo hivyo kwa CCM, siku itapoamua kufumba macho na kuchukua uamuzi mgumu wa kuwang'oa mafisadi papa kwenye chama chao, ndiyo itakuwa the end of the story, kutambulika kwa CCM, kama chama tawala cha TZ, kwa kuwa ukweli ulio dhahiri ni kuwa CCM, inafadhiliwa kwa kiasi kikubwa na pesa chafu za mafisadi hao!!
 
Back
Top Bottom