Kwanza asante Mod kwa kunifungia baada ya kumuhusisha Nape na Achebe. Natoa shukrani kwa kuwa sikupewa muda wa kujitetea. Ili niweze kuthibitisha hoja.
Baada ya hapo Kichwa cha habari hapo juu chahusika.
Katika hali isiyo ya kawaida imefahamika kuwa Jey K anaweza nae akavuliwa gamba na chama katika kile kilichosemwa kusafisha chama dhidi ya "Mafisadi". Hii imetokana na kufaidi zile fedha za Kagoda mwaka 2005 kupitia swahiba wake yule mwarabu wa Tabora. Imefahamika hatua hiyo ikichukuliwa basi CCM yaani chama cha magamba kitakuwa kimejipendezesha mbele ya wananchi na kuweza kufaulu ule mtihani ujao wa 2015 ambao unatabiria labda CCM wanaweza pata "sup" kama sio "Carry". Imefahamika hofu hii ni dhidi ya Chama cha Magwanda.
Hofu hii itatoka endapo hawa mapacha wa"nne" yaani vijisent, Mmasai, Jey K na mwarabu wa Tabora watatoswa rasmi mwaka 2015 na si sasa kuepusha shari ndani ya chama.
Nadhani MOD hatanifukuza hapa JF. Halafu nashukuru wale mlionitetea kule ICU(Complaits thread).
Pamoja saaaana..!!