The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema yupo tayari kumsaidia Rais wa sasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kuendelea kubaki kuwa Rais na hatoruhusu kamwe aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila kuwa rais tena.
Kupitia mtandao wa X Muhoozi ameandika “Sitaruhusu Joseph Kabila awe Rais wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo tena.”
Hata hivyo amesisitiza kwa kumwambia (Kabila) “Unaweza kusahau kuhusu hilo”
Kuhusu Tshisekedi kuendelea kuwa Rais Muhoozi amesema “Kaka yangu mkubwa Mheshimwa Felix Tshisekedi ni Rais wa DRC na nitamuunga mkono kadiri inavyowezekana”
Ikumbukwe hivi karibuni Kabila alisema anarudi DRC na imeripotiwa kwa siku za karibuni ameonekana maeneo ya Mashariki mwa mji wa Goma ambao unakaliwa na waasi wa M23 jambo ambalo limeonekana kuleta wasiwasi kwa utalawala wa Tshisekedi kuwa huenda atataka tena kugombea Urais.