Muhongo Na Maswi Wachunguzwe na Kukamatwa Mara Moja

Drug-Czar

Member
Oct 27, 2014
16
39
Kati hali ya kushangaza, hawa viongozi wa zamani wa wizara ya nishati na madini wanagawa fedha nyingi tena mamilioni ili watetewe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Nikiwa mmoja wa watu ambao wameshawishiwa nafedha nyingi, nathibitsha kwamba hawa watu bila kuwakamata, nchi itayumba.

Bila kujua kwamba walimwendea rafiki yangu na kiasi cha Tsh. 25million, ambaye aligoma kuchukua hizo fedha haramu, Waziri Muhongo mwenyewe aliniijia kwanza tukiwa Dodoma na hata hapa Dar na kutaka kunipa Tsh. 25million ili niongee na chombo kimoja cha habari kumsafisha. Baada ya habari yao nzuri kuandikwa ningeongezewa Mil. Nyingine 15 hasa kamati ya PAC Ikishambuliwa. Bila kumung’unya maneno, mwingine aliyeongwa kiasi cha Million 14 na Maswi ni William Malechela almaarufu kama Lemutuzu.

Bwana Lemutuz amepewa kiasi hicho cha fedha ili kuwagawia vijana wanaofanya utetezi mitandaoni ambao yeye anawajua. Kada wao mwingine anayetembeza fedha kwenye viombo vya habari anafahamika kwa jina la Chief Kiumbe. Hawa watu wakamatwe. Ni huyu William Malechela ndiye aliyegawa fedha kwa vyombo mbali mbali za habari kipindi cha kashfa ya Kapuya
 
Alafu sasa wanatoa hiyo mihela watetewe kivipi wakati maazimio ya bunge yanasubiri utekelejazi tu wa le professer
 
Hakuna waziri mchapakazi kama Muhongo hapa Tanzania. JK atafanya kosa kubwa sana akimuondoa , watanzania tunamuhitaji sana Muhongo
 
Kuna mbwa mmoja alinipigia kunishawishi hilo eti anipe laki moja nikamuuliza Una akili?? akauliza why nikamjibu kwanini unatupa PESA kwa kazi za kijuha namna hiyo?

Wasichoelewa ni kuwa Kazi imekwisha na Jukumu la Rais ni kutekeleza maazimio ya bunge akiwa Kama sehemu ya bunge.....

Nilichogundua ni kwamba Muhongo na genge lake ni wapuuzi Sana wanaamini bado wana nafasi ya kugeuza upepo Wa ESCROW.....
 
Hii habari inaweza ikawa ya ukweli sana.. Ukiangalia mwazo kabisa W. Malechela alikuwa mtu wa mwanzo kuunga mkono kamati ya PAC kuhusu hawa wezi kuwajibishwa..Lakini gafla recently naona ameanza kuandika tofauti kabisa na mawazo yake ya mwanzo. Hata hivyo simshangai coz Watanzania wengi ndio tulivyo...ukichukulia zaidi jamaa hana aibu kabisa..!!
 
Kuna mbwa mmoja alinipigia kunishawishi hilo eti anipe laki moja nikamuuliza Una akili?? akauliza why nikamjibu kwanini unatupa PESA kwa kazi za kijuha namna hiyo?

Wasichoelewa ni kuwa Kazi imekwisha na Jukumu la Rais ni kutekeleza maazimio ya bunge akiwa Kama sehemu ya bunge.....

Nilichogundua ni kwamba Muhongo na genge lake ni wapuuzi Sana wanaamini bado wana nafasi ya kugeuza upepo Wa ESCROW.....

Muhongo hana kosa. Ni chuki binafsi tu za watu. JK hawezi kumuondoa tunamuhitaji Muhongo atulindie gesi yetu .
 
Hakuna waziri mchapakazi kama Muhongo hapa Tanzania. JK atafanya kosa kubwa sana akimuondoa , watanzania tunamuhitaji sana Muhongo

Muhungo anaweza akawa anahitajika zaidi kwenye academic, hapo nitakubali...Lakini kwenye uongozi na kusimamia rasilimali za nchi yetu tusahau..mkuu kama umevuta mshiko kajifikirie upya kumtetea huyu mtu na wenzake..acha maazimio ya bunge yafanye kazi..
 
Kwenye uongozi na kusimamia rasilimali nani anafaa?
 
Nimemwandikia Habinder Sigh Sethi na Ruge wanipe million 100 niwafanyie lobbing kwenye mitandao, niwaajiri na vijana ili kusafisha upotoshaji wanaofanyiwa, nangoja majibu.
 
hii dunia ina vituko sana.....aise
 
Kuna mbwa mmoja alinipigia kunishawishi hilo eti anipe laki moja nikamuuliza Una akili?? akauliza why nikamjibu kwanini unatupa PESA kwa kazi za kijuha namna hiyo?

Wasichoelewa ni kuwa Kazi imekwisha na Jukumu la Rais ni kutekeleza maazimio ya bunge akiwa Kama sehemu ya bunge.....

Nilichogundua ni kwamba Muhongo na genge lake ni wapuuzi Sana wanaamini bado wana nafasi ya kugeuza upepo Wa ESCROW.....
FaizaFoxy atakuwa mmoja wa waliopewa hizo fedha kwa ajili ya kuendesha kampeni ya kutetea hao wezi na wahujumu uchumi. Haiingi akilini watu wanatumia nguvu na rasilimali kubwa kuhakikisha uchafu na uhalifu waliofanya unageuzwa kuwa jambo halali machoni mwa umma wa Watanzania.

Jambo la kujiuliza ni kuwa; Hivi hao watu walizaliwa ama kuumbwa ili wawe MAWAZIRI ama MAKATIBU WAKUU? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema wazi kuwa; 'KWA KUTUHUMIWA TU INATOSHA KWA WEWE KUONDOKA KWENYE NAFASI UNAYOSHIKILIA KWANI TAYARI UMESHACHAFUKA NA HUNA IMANI MACHONI MWA WALE UNAOWAONGOZA'.

Nachelea kusema kuwa Mhe. Rais anachelewa kuwaondoa hao wahalifu na kwa kuendelea kuchelewa kuwaondoa ndivyo wanazidi kuharibu kinyume na matarajio yake.
 
Last edited by a moderator:
Muongo atupishe sisi wenye mitaji ya kutengeneza juice tuijenge nchi prof. Muongo kama muhongo hafai kua ktk system za serikali zinazofuata sheria
 
Mkuu asemacho ni kweli kina maswi wanatumia hela Sana kuhonga vyombo vya habari na social media ili kushawishi rais asiwachukulie hatua...

hao wanaopewa hela basi njaa itakuwa imewazidi!na hao wanaopewa hela kuja kuwapa watu hela humu mitandaoni wa njaaaa piaaa...tena maskini wa vikraa
 
Back
Top Bottom