Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 28,850
- 37,562
Kwa hyo waziri hawajibiki kwa bunge? Iweje wakati wa oparesheni tokomeza mawaziri waliwajibika kwa bunge bila kusubiri uamuzi wa mamlaka ya uteuzi wao? Au hizi sheria zikoje? Tundu Lissu nisaidie kwa hili tafadhari mimi ni bush lawyer kama makinda
Bunge halina mamlaka ya kumuondoa waziri wa kawaida isipokuwa waziri mkuu.muhongo anaposema bado ni waziri yuko sahihi.akina kagasheki walijiuzuru kwa agizo la rais kwa njia ya simu alipomuagiza pinda atoe taarifa bungeni.kwa kuwa muhongo hataki kujiuzulu atabaki waziri hadi rais amtimue.
Kwa kuwa Pinda yu salama..Pinda ndiye atakayejitahidi kuhakikisha Muhongo na wenzake wanaondoka ili mwezi January arudi Bungeni akiwa shujaa kwa kutekeleza maagizo ya Bunge na hivyo kuondoa kiwingu hiki "kwenye ile safari yake ya kimyakimya kwenda ikulu"
Kwenye hili JK atachagua kama aendelee na Muhongo bila Pinda au Pinda bila Muhongo.
Yeyote aliyecheza na Dr. Regnald Mengi mtu wa watu, mtetezi wa wanyonge nguvu ya umma haikumuacha salama.
Akawaulize wakina Wilson Masilingi na wenzake....
Napendekeza kuwe na JF classes; 1, 2. 3, 4 and 5, ili kila wahusika wa class fulani wachangie kwenye daraja lao. Vigezo viainishwe kutambua na ku-classify haya madaraja. Kuna watu humu, kwa mujibu wa argumentations katika mihango yao, ni dhahiri kuwa ni kiwango cha daraja la 5 lakini wanachangia katika hoja za daraja la kwanza, hivyo kufanya uchafuzi.
Pendekezo husika la Bunge linasema mamlaka ya uteuzi husika zishauriwe kuwajibisha wahusika..... wakati mamlaka hiyo bado hijashauriwa, ili ikubaliane au ikatae ushauri, wachangiaji JF daraja la 5 wanatangaza fulani amefukuzwa kazi ya uwaziri; amefukuzwa na nani?
JF daraja la 1 wanafahamu kuwa Prof. Muhongo bado ni Waziri wa Nishati na Madini kwa mujibu wa sheria za nchi.
Hata hivyo, sidhani iwapo mamlaka husika itakubaliana (soma give in) na shinikizo/ghiriba za akina Mengi & Co.
Hakuna Popote pale duniani bepari amepata kutetea wanyonge, mtetezi wa wanyonge huwa hatajiriki, Mengi anatetea maslahi yake, migodi anayomiliki na Vitalu anavyotamani, thats it, amkeni Wabongo
Hakuna Popote pale duniani bepari amepata kutetea wanyonge, mtetezi wa wanyonge huwa hatajiriki, Mengi anatetea maslahi yake, migodi anayomiliki na Vitalu anavyotamani, thats it, amkeni Wabongo
Mengi asiisogelee kabisa gesi. Mengi ni bepari.mbinafsi, mnyonyaji wa Taifa
jamaa kachanganyikiwa.
Anaamini yeye bado waziri. Mwenye uwezo wa kumvua madaraka ni rais tu na siyo wahuni wa bungeni. Hawezi kubabaishwa na wahuni na wala rushwa. Yeye ni waziri na atabaki kuwa waziri hadi pale rais atakaposema basi...
Hapa dodoma watu wanamuona wazimu na hii jeuri yake ya kitoto.
Haamini kwamba bunge limemvua madaraka ya uwaziri
We utakuwa na tabia za kishoga mengi katokea wapi huku ukisikia muhongo ujuwe muongo kweli na ukisikia kubwa jinga ujuwe kubwa jinga kweli !!
Kamati haijamtaja sehemu yoyote ile
Kuwa amepewa mgao wa fedha zaidi ya kutakiwa kuwajibika kwa kuwa anasimamia sekta husika. Naamini
Kina zitto walisaka sana jina lake kwenye mgao wa hela wakakosa hahahaha! Wakaona waseme ye dalali yes ni dalali coz wazir gani asiyekutana na wawekezaji kwenye sekta yake mlitaka huyo seth aende akakutane na wizara ya jinsia na watoto? Eti alikutana naye kwenye ofisi ya umma! Sasa mlitaka akakutane naye hotelini! Wabongo wakiamua kukutafuta hata kama huna kosa watakumaliza tu! Ushauri wangu kwa MUhongo, nenda kafanye kazi huko walikokuwa wanakuthamini na kukupa tuzo kutambu mchango wako achana na wabongo tumejaa fitna na chuki!
Ukawa wakiongozwa na Mbowe wamehongwa na Serikali ndio maana wamekubali kufanya maridhiano ya KIJUHA.
Rais hawezi kumtimua mtu ambaye alimwachusha shughuli zake na kumuingiza kwenye mkenge wa kisiasa. Amini usiamini. Muhongo ataendelea kuchapa kazi kwa maendeleo ya Watanzania