Muhimu: Warithi wa Mwl. J.K Nyerere wapimwe kwa haki

kitambiheshima

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
452
Reaction score
116
Imezoeleka kusikia watu wakiwapima marais waliofuata baada ya Mwl. Nyerere kwa kuonesha kuwa kuwa wao si lolote ikilinganishwa na utendaji wa Mwalimu.

Sina ubishi juu ya kazi kubwa aliyoifanya Nyerere katika kuwaunganisha watanzania na kujenga misingi ya utu na amani ya taifa kwa ujumla. Aidha jitihada za mwalimu kuifanya Afrika ijitambue na kujikomboa kutoka katika makucha ya ukoloni, ni kazi ambayo haiwezi kubezwa hata kidogo.

Mwalimu kwa wakati wake alifanya yale aliyoyafanya kulingana na wakati na mahitaji ya jamii wakati huo. Mathalani, watanzania wakiwa milioni 16 Nyerere aliweza kuwapa elimu bure na afya bure. Wakati wa njaa watu walipanga foleni kupokea bulga na maziwa ya kopo bure.

Wakati wote Nyerere alihimiza amani miongoni mwa wananchi. Wakati huo hakukuwa na utitiri wa vyombo vya habari na mitandao. Kulikuwa radio Tanzania tu. Ilikuwa rahisi sana kwa Mwalimu kupenyeza jambo lolote kwa wananchi nao wakalipokea kama lilivyo na kuliamini. Hawakuwa na mbadala wa kulinganishia usahihi na umaantiki wa yale wanayoambiwa. Hali hiyo, ilichangia sana kumweka Mwl kwenye chati za juu.

Hata hivyo ninaamini Mwalimu alisoma alama za nyakati. Aligundua kuwa utawala wake ulikuwa unaelekea kwenye changamoto kubwa za mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii hivyo akaamua kung'atuka ili kupisha mabadiliko hayo.

Ndugu zangu tuliona jinsi Mwinyi alivyojaribu kuifungua Tanzania kiteknolojia, kisiasa na kiuchumi. Ni wakati wa Mwinyi watu walianza walau kuvaa mitumba badala ya kaniki. TV zilianza kumilikiwa na wananchi wakati wa Mwinyi. Kiujumla Mwinyi aliitoa nchi tongotongo. Hata hivyo zilijitokeza changamoto kama ilivyokuwa kwa Mwl, Mwinyi alizidisha uholela kiasi kwamba serikali ilikosa authority ya kiutawala. Watu binafsi walikuwa na nguvu kuliko serikali.

Kilikuja kipindi cha Benjamin Mkapa.ambaye aliifungua zaidi nchi kiuchumi. Ben alichagua uwekezaji wa wageni zaidi ya wenyeji baada ya kugundua kuwa.Watanzania wazalendo wengi wao si waadilifu (mifano ipo kwa viwanda mbalimbali ambavyo Mwalimu aliviweka chini ya usimamizi wa wazawa wakavifilisi hadi vikafungwa mfn Mutex, mashirika mengine ya umma). Hakuna ubishi kuwa kulikuwa na makosa fulanifulani ktk uwekezaji huo hasa kwenye mikataba. Lakini kwa kiasi kikubwa uwekezaji wa Ben uliiwezesha nchi kuwa na uwezo wa kulipa madeni na serikali kurudisha heshima ya kiuchumi . Changamoto ya idadi kubwa ya watu iliyoambatana na ushiriki mdogo katika uwekezaji wa ndani ukawa bado mtihani kwa serikali ya Ben.

Ameingia Kikwete nae amefanya yake mazuri mengi. Mfano Kikwete, ktk mazingira ya changamoto.ya miundombinu amefanikiwa kuiunganisha 3/4 ya nchi kwa mtandao wa barabara za lami, ametanua wigo wa haki ya kila mtanzania kupata elimu kwa kuongeza wingi wa shule za sekondari na vyuo vikuu. Ameruhusu uwekezaji wa sekta binafsi ambazo zimesaidia kupunguza tatizo la.ukosefu wa ajira kwa vijana. Amethubutu kuwaonesha watanzania kuwa mambo makuba kama mabadiliko ya katiba, vitambulisho vya taifa, mpambano dhidi ya uhalifu na ulinzi wa mipaka.yetu vinawezekana. Mambo hayo ameyafanya kwa ustadi mkubwa. Katika kipindi chake uhuru wa mtu kutoa maoni na uhuru kwa wapinzani wa serikali iliyoko madarakani umetolewa kwa zaidi ya 100'/,. Ikumbukwe kuwa Kikwete ametawala katika kipindi ambacho kikundi kidogo cha watu kilikuwa kimedhamiria kuhakikisha nchi haitawaliki. Kikundi hiki kilijidhatiti kwa misaada ya "wakubwa", lakini jamaa "alisimama".

Hivyo kwa maelezo hayo, niwaombe ndugu zangu watanzania tutende haki tunapowapima marais wengine wa tanzania tunapowalinganisha na Rais wa kwanza Mwalimu Nyerere. Tuwapime kwa kuzingatia changamoto za kila mmoja kwa wakati wake.
 
Ubora na uimara wa hawa viongozi wa nadhani uko wazi . Kiongozi bora kwa kaoni yangu ni kama ifuatavyo:

(1)Kiwete ni namba moja (Hii awamu yule mkurya sijui mzanaki asingeiweza,nchi imekua na wasomi wengi na matajiri wengi na kila mtu anataka maisha yake binafsi mazuri).Amekuta udini ukiwa umesambaa sana lakini anakabiliana nao kisayansi kuepusha vurugu kubwa
(2) Mkapa anashika nafasi ya pili japo alishindwa kuwa mvumilivu kwa wapinzani na kutumia nguvu kubwa na fedha nyingi kuwanyamazisha.
Huyu alipokosa mbinu mbadala za kikuza uchumi aliuza nyumba za umma na mashirka ya umma ili ajaze fuko la serikali.
(3) Mwinyi anashika nafasi ya tatu( ama kweli mzee ruksa aliitoa nchi hii kwenye lindi la umaskini na giza nene la kiuchumi. Tatizo lake naye alifumbia macho udini wa kiislam na Kiroma ambao tayari ukikua umejizatiti kisiri siri wakati wa Nyerere.
(4) Nyerere kulingana na wakati huo labda na kukosa raslimali watu wenye Elimu basi alifeli sana na chaajabu vyombo vya hbari havikuweza kabisa kumkoso zaidi ya kumsifia hata palealipokosea.Alijitahidi kuimarisha umoja wa watanzania alioukuta toka enzi ya mkoloni. Kama pangekua na ukabila wakati wa mkoloni basi wazee wa Dsm wasingemkaribisha kwa upendo na kumwamini sana.
Alishindwa kuondoa udini hasa Uroma upande wa bara na Uislam upande wa Zanzibar japo alisema serikali haina dini lakini aliendeleza utaratibu wa kutumia fedha za walipa kodi kuendesha shughuli za kidini chini ya balozi za Vatikani jambo ambalo lilipaswa lifanywe na waroma wenyewe,Hali inayotuletea usumbufu hadi leo
 
nyerere aliivuruga sana nchi..kikwete ndio rais bora kupita wote tanzania.. hongera sana mheshimiwa rais kwa kutuletea maendeleo ya ukweli tanzania tunakupenda sana watanzania. wanaokubeza ni wachawi na wanga wana mapepo na laana
 
Kheeri ukose mali,upate akiiiili,kwani elimu ni bahari haina mwishooosho!..

by Banza Stone,Ticha wa maticha - Elimu ya Mjinga!..

#TeamDhaifu !..

nyerere aliivuruga sana nchi..kikwete ndio rais bora kupita wote tanzania.. hongera sana mheshimiwa rais kwa kutuletea maendeleo ya ukweli tanzania tunakupenda sana watanzania. wanaokubeza ni wachawi na wanga wana mapepo na laana
 
Nyerere hakuna jema alilowafanyia Watanzania. Nyerere kawafanyia mema wakatoliki.

Kwanini Rais wa Watanzania awe mbarikiwa kuelekea Utukufu? Kwa sababu moja tu. Alikuwa kwanza ni Mkurusedi aliyedhalilisha na kutaifisha mali za wasiokuwa Wakatoliki. Alifunga na kuwapoteza wote wasiokuwa wakatoliki na waliompinga.

Wakati Afrika inaongelea kuungana, yeye alikuwa anaongelea na anashadidia kufarakana, mfano mzuri na ulio hai ni pale alipotoa kila support Biafra itengane na kuwa nchi pekee kutoka Nigeria. Jee hilo hulijui?

Namfananisha nyerere na panya anaeuma na kupuliza. Au nyoka mwenye ndimi mbili.

Nyerere kaiua Tanganyika, akaiacha Tanzania hohehahe, muflis mpaka benki kuu akaichoma moto, wizara ya mambo ya ndani akaichoma moto, muda mfupi kabla hajastaafu.

Ni uongo kuwa alifanya la maana kwa wananchi wote katika miaka 24 aliyotawala. Alifanya la maana kwa wakatoliki ambao kwa sasa wanahodhi ardhi kubwa baada ya Serikali.

Jee, lipi moja la maana alilofanya Nyerere kwa nchi yake? Usijibu, mimi nalijuwa. Ni kuwafanya wote wawe maskini kasoro kanisa katoliki.

Tanzania hii kuna tajiri zaidi ya kanisa katoliki? Labda Rostam?
 
exactly what i expected from you..
 
shukrani ya punda ni mateke kweli mzee yule kafa masikina kma hakuwa rais wa kwanza wa nchi hii kwa zaid ya miaka 25 akitetea nchi yake na watu wa Tanzania na Africa kwa ujulmla mungu atawalaan na kuwahukumu wanafiki wte hao akina kikwete na mwinyi na mkapa nani kawajenga mpaka wakafika hapo walipo udhani ni jitihada binafsi?
 
Hapa ni ukweli tu utatuweka huru regardless ukweli huo unawapenya kwa nguvu kiasi gani.

Ni lazima tukubali kuwa J. Kikwete ni jembe la majembe. Bila hekima, busara na maarifa ya Kikwete the nation was about to immerse into the deepest water.

Kuna.watu wanalazimisha kutokubaliana na ukweli kuwa hakuna mwenye uwezo wa kuchanga karata zake za kisiasa nchi hii, kwa ustadi kama Kikwete. Ukweli ndo huo!
 
shukrani ya punda ni mateke kweli mzee yule kafa masikina kma hakuwa rais wa kwanza wa nchi hii kwa zaid ya miaka 25 akitetea nchi yake na watu wa Tanzania na Africa kwa ujulmla mungu atawalaan na kuwahukumu wanafiki wte hao akina kikwete na mwinyi na mkapa nani kawajenga mpaka wakafika hapo walipo udhani ni jitihada binafsi?

Kaiwacha nchi masikini, yeye hajawahi kuwa masikini toka auache Urais, katazame Mwitongo halafu uniambie maskini anaishi hivyo? mpaka wahudumu wake wa nyumbani walikuwa ni ma sister wa Kikatoliki, hujui kwanini?
 
Kwa hiyo wewe Faizafoxy unataka kutuaminisha kwamba Nyerere alitaifisha mali za waislamu na kuacha za wakristo? Si kweli..

WEWE UNA CHUKI NAE TU.. Tena wewe ni mnafki sana..
Na utalaaniwa...
 
Nyerere alifanya kiini macho katika kutaifisha mashule, alitaifisha shule zinazomilikiwa na dini lakini akaziacha shule za seminari
.
 
Hivi katika kutaifisha shule, kuna shule ilitaifishwa ikiwa na msikiti?

Kama siyo angetaifishaje shule za seminary ili hali shule hizo zina makanisa?
ACHENI UNAFKI NYIE WAJUKUU WA KIJAKAZI.
 
Kaiwacha nchi masikini, yeye hajawahi kuwa masikini toka auache Urais, katazame Mwitongo halafu uniambie maskini anaishi hivyo? mpaka wahudumu wake wa nyumbani walikuwa ni ma sister wa Kikatoliki, hujui kwanini?

wewe umasikini unautadhama ktk nyanja ipi ivi maraisi wa kiafria hususani wa enzi za mwalimu unaweza kuwafananisha na mwl katika easilimali akina mobutu au bongo ni swa na mwl acha ukweli uwe ukweli bana
 
Ndiyo maana tunasema utaifishaji mashule ulikuwa ni fix tu!

wewe umasikini unautadhama ktk nyanja ipi ivi maraisi wa kiafria hususani wa enzi za mwalimu unaweza kuwafananisha na mwl katika easilimali akina mobutu au bongo ni swa na mwl acha ukweli uwe ukweli bana

Huyo Mwalimu hakuna chochote cha maana alichokifanya, alitawala kidikteta na aliwapoteza wote wenye akili.

Ni nini zaidi cha maana alichokifanya zaidi ya kuifanya hii nchi iwe maskini wa mwisho duniani. Tuulize tuliokuwepo wakati wake, naona wewe umejazwa ujinga kwa kudanganywa kuwa eti ni "mtakatifu".
 
Hivi katika kutaifisha shule, kuna shule ilitaifishwa ikiwa na msikiti?

Kama siyo angetaifishaje shule za seminary ili hali shule hizo zina makanisa?
ACHENI UNAFKI NYIE WAJUKUU WA KIJAKAZI.
Anaposema sote tutoe nguo za juu, kisha sisi tunabaki na vibikini na wengine mpaka ikulu inaonekana yeye mwenzetu kumbe ana bukta ndani imehifadhi utupu wake hapo umetuacha kwenye mataa.
 
Kaiwacha nchi masikini, yeye hajawahi kuwa masikini toka auache Urais, katazame Mwitongo halafu uniambie maskini anaishi hivyo? mpaka wahudumu wake wa nyumbani walikuwa ni ma sister wa Kikatoliki, hujui kwanini?
Ameandaliwa cheo kuitwa Mwenye heri
 
Back
Top Bottom